Sitasahau hiii
Umeenda nyumbni kwa mtu alafu unakutana na
toto sumbufu balaa amjawai kuonana lkn
limeshakuzoea..... Unakuja mwenyewe labda
umechomekea shati nini!! linaanza kukurukia
rukia mala linakuvuta shati mpaka linachomoka...
Mama yake anabaki we junior embu muache
ancle.... Basi unafika unakaa sebureni linaanza
kukusumbua mala likupige kibao cha kushitukiza
ulikua unaangalia zako mbele kwenye tv mala
linakudandia mapajani... Unajibalaguza kuliambia
aya nenda kwa mama.. Linakutemea mate usoni
na mama yake anacheka tu na kukwambia
nakwambia leo utakoma mimi uwa nayafinya
kisiri siri sasa unakuta umeletewa chai na
maandazi toto lipo mbeke yako linakuangalia
linataka kuokota andazi kwakua unaona mikono
yake michafu unaamua kulimegea kipande
halitaki linataka zima... Ujakaa vizuri limemwaga
chakula kwa hasira.. Masaa yanaenda kwenye tv
muda wa habari... Lenyewe linataka kuweka
cartoon... Linaaza kulia kwa nguvu mamake
anasema aya embu liwekeeni ma cartoon yake
kipindi icho wewe unatamani lipigwe balaa...
Ujakaa sawa unashangaa umepigwa na remote
kichwani unageuka kwa hasira unakuta toto
linacheka.... Ngoja niishie hapa ila kama upo ivyo
na mtoto wako watu hawapendi ujue