Sitta amcharukia Jaji Mkuu


Ndugu yangu Ngekewa. Mambo mengi yanayofanyika hapa nchini yanahitaji kujitolea zaidi. Kauli ya kejeli iliyotolewa na Speaker wa BUnge sijaiona. Kama kauli ya "Na hapa watasema naingilia Mahakama, Potelea mbali" ndio kauli ya kejeli, basi nadhani kejeli inabadilika maana. Maana nijuavyo mimi maneno hayo si kejeli bali ni sawa na kusema "Basi acha wachukulie hivyo".

Ndugu yangu, sheria ingekuwa inafuatwa vizuri (inavyotakiwa), malumbano kama haya yasingekuwa na nafasi. Ni kweli kabisa kuwa sheria zinaanza kutozingatia maana ya kuundwa kwake. Inawezekanaje sheria iwe na manufaa kwa mtu mmoja mmoja bila kujali haki sawa kwa wengine (ambao wanaweza kuwa wengi) na mtu atakaelizungumzia hilo aonekane anaingilia mamlaka ya Mahakama? Uingiliaji gani huo wa mamlaka ambao umefanyika baada ya mahakama kuamua? Nadhani uingiliaji ungekuwa wakati/kabla ya mahakama kufanya maamuzi, tungeweza kusema mahakama imeingiliwa na kuwa na haki ya kulaumu uingiliaji huo. Ila kama Mahakama inaelekea kufanya maamuzi yasiyo na mantiki yoyote (yasiyo make any sense) sidhani kama huo ni uingiliaji wa mahakama zaidi ya kulaumu utendaje wake. Mahakama ni zetu kama zilivyo kwa Majaji na Mahakimu wengine. Tunayo haki (na hasa kwa kupitia Bunge letu) kulalamika tunapoona kuwa haki iliyotarajiwa kutolewa na mahakama zetu inatolewa visivyo na hata kusifia endapo tunaona haki inatolewa ipasavyo. Tusizoee kusifiwa tu, tukubali kukosolewa ili tuwe bora zaidi. Majai wanaanza kuelekea kufikiri kuwa Mahakama ni mali yao binafsi. Inawezekanaje kuwa hivyo?
 
Ni uozo mtupu, lakini bora bunge - humo kuna baadhi ya watu makini.

Watu makini wapo kwenye mihimili yote mitatu ila ni wachache sana na wamemezwa na watu wenye ubinafsi na uroho kiasi kwamba hawa wachache hawavumi....
 
Akitoa taarifa hiyo bungeni leo mjini hapa, Sitta alionyesha kulaumu baadhi ya uamuzi ambao umekuwa ukitolewa na mahakama na kusema kwamba unatoa fursa kwa mtu mmoja kuliko jamii nzima, jambo linaloumiza.

Kwanza sentensi sahihi inatakiwa kuandikwa kama "... baadhi ya maamuzi..." unapoandika neno baadhi unaongelea wingi, na wingi wa uamuzi ni maamuzi, hakuna kitu kama "baadhi ya uamuzi"

Kama muandishi hawezi kuandika Kiswahili kizuri nitaamini vipi kwamba anachoandika ni sahihi?

Tukienda kwenye maada, Spika Sitta anaposema mfumo wa mahakama unatoa fursa kwa mtu mmoja kuliko jamii nzima anamaanisha kwamba hana imani na wanamahakama, hususan majaji, kutoa maamuzi kwa mujibu wa sheria? Ina maana Spika hawaamini majaji kama wanyambulishi wa sheria? Ukiangalia kiundani hata hao wabunge nao si mtu mmoja mmoja? anataka kuturudisha Ugiriki ya zamani ambapo wananchi wa mji-nchi walikutana na kufanya maamuzi pamoja?

Spika Sitta kama kawaida yake amejionyesha tena kutokuwa mtu makini.Mara hii anataka kutengeneza mgongano wa kikatiba.
 

Well doMkuu RECTA, wanasheria mara zote wanajiita "learned brothers"(au sistres for that matter) lakini huwawanajisahau kuwa sheria ni ya jamii.
Kama sheria hailindi maslahi ya jamii basi sheria hizo zinakosa tafsiri yenye mantiki inayo faa.
Mfano wa Morogoro kuhusu EWURA ni mfano mahsusi ambapo makhakama imetereza tena vibaya!
Akitokea muuaji aliyethibitika na akawahikufungua stay ya kufunguliwa mashtaka basi mahakama yetu inaelekea ita kubaliana na hilo!
Kuna mfisadi/majambazi mengi yanayotumia mianya katika sheria zetu kucheza na haki za watu.Mahakama inalijua hilio kama si kushirikiana na watu hao.
Hivi karibuni jirani yangu mwenye uwezo alimpiga jirani yetu mwingine.Yeye akakimbilia Polisi/mahakamani Kawe kuwa ndiye aliyepigwa.
Kwa ujanja wa kupewa kitu kidogo hakimu akpanga tarehe kwa kificho, tarehe ambayo alihakikisha mshtakiwa hakuwepo.
Kwa mshangao mshitakiwa akaja kubebwa msobe msobe na askari na kupelekwa Segerea.
Hapa wananchi wakailaumu sana mahakama pamoja na hakimu yule.
Haya ndiyo mapungufu ambayo yanaipunguzia sana mahakama hadhi yake mbele ya jamii.
 

Mahakama zetu nazo zimejaa rushwa, haki haitendeki kwa watu wasionacho. baadhi ya mahakimu na majaji wamesahau proffession yao kwa kupenda rushwa.
Muhimili huu nao una matatizo makubwa jamii imewekwa kati haina pa kukimbilia.
 
 
Viongozi wote wa serikali ya tanzania nikiwa na maana ya mihimili yote mitatu hawawezi kusemana maana wao wanaongoza kila mtu sehemju yake kuburunda pamoja na kuwa makosa ya mahakama yanaonekana zaidi kwa watu wa kawaida.
 
Mhakama ni chombo cha umma ambacho inatakiwa kifanye kazi kitaaluma kwa kufuata sheria. Bunge ni chombo cha umma kinachotakiwa kuwa sauti ya umma. Bunge huwekwa madarakani na wananchi na Bunge lisipotekeleza yale wanayotaka wananchi huchapwa kiboko na wananchi kupitia kura.

Nani anayesimamia utendaji wa mahakama na kuiadibisha inapokosea? ... HAWA NI MIUNGU??? Siku zote mahakama imekuwa mbele kujijengea ngome za kuilinda dhidi ya kuingiliwa. Lakini maamuzi ya mahakama yanaonwa na umma na ni lazima umma ung'ake unapoona mahakama inapotoka. Hivi ni nani wa kuisema mahakama kama siyo wananchi kupitia kwa Bunge lao?

Mahakama inatakiwa ifanye uamuzi kwa kufuata sheria, huku ikijua kuwa sheria hizo zimetungwa ili kulinda maslahi ya umma!! Umma usiporidhika na maamuzi ya mahakama unayo haki ya kui-angalia kwa macho mawili. Hivi kwenye mfano wa mafuta; ikiwa wataalam wa mafuta wamesema haya mafuta ni machafu, mahakama walitumia utaalam gani kuruhusu mafuta machafu kuendelea kuuzwa?

Ni kweli hata bunge lina makosa yake, lakini kwa hili la mahakama kupotoka bunge ndo sauti pekee inayotakiwa kutoka. Bunge ni sauti ya umma, au tumesahau?

HAPA SPIKA ANAFANYA KAZI YAKE HALALI TULIYOMUAJIRI KUIFANYA NA ANASTAHILI PONGEZI.
 
Last edited:
Leo, Spika wa Bunge Samuel Sitta aliamua kuanzisha mjadala ambao kwetu sisi tunauona hauna maslahi, tija wala manufaa kwa Watanzania ambao kuna mambo mengi ya msingi ambayo si Bunge tu, bali viongozi wanapaswa kuyafanyia kazi.

Spika Sitta aliamua kujibu, tena kwa maneno ya kejeli ya ‘Potelea mbali’, hatua ya mhimili mwingine wa Dola, Mahakama, kulalamikia hatua ya mhimili huo wa Bunge unaoongozwa na Sitta, kuingilia kazi za Mahakama.


MKUU WA MEDANI NAKUBALIANA NAWE ILA JANA NILISHUHUDIA NAMNA SAMWELI SITTA ALIVYOFANYA DHARAU KAMA ILIVYOANDIKWA HAPO JUU, KAMA CJ ALIMUONA AKIONGEA JANA, JK NAYE BASI UTAKUBALIANA NA HUYO MHARIRI MKUU FMES, IT WAS UHUNI WA SAIGONI TYPICALLY, WABUNGE WALIANZA KUMPIGIA MAKOFI GHAFLA WALISITA KUMPIGIA MAKOFI. JANA AMEDHARIRISHA SANA.

“Hapa watasema pia naingilia mahakama…potelea mbali,” alisema Sitta bungeni Dodoma leo. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Bunge, tamko la Bunge litatolewa leo baada ya kipindi cha maswali na majibu.




Hapa Mh. Spika tayari amekwisha pre-empty tamko la bunge, maana amelisemea msimamo bunge kabla halijatoa tamko, kazi ipo![/QUOTE]
 
Alichofanya Jaji Mkuu ni sahihi.

- Alichofanya huyu Jaji ni kutufahamisha wananchi kwamba hana nguvu kisheria, au hajui nguvu zake kisheria. Jaji wa mahakama kuu anakwenda kulalamikia Spika kwenye majukwaa ya siasa?

- What a shame, mimi siku zote ninamuona huyu Jaji nilifikiri wamo kumbe ni wale wale magoi goi! Bunge litawaingiliaje Judicial kama sio uzembe wa Mahakama? Pamoja na kwamba vyombo vitatu vikuu vya taifa vinatakiwa kuwa balanced, bado Judicial ndio wanaotakiwa kuwa na the edge, kama alivyosema the author wa hii system Mzee Madison, kwamba mahakama ni chombo cha kusimamia haki za minority katika taifa against the mighty power ya bunge na executive, na akaonya kwamba mahakama siku zote lazima iwe macho sana kwa sababu siku zote ni rahisi sana kwa bunge na executive kuungana against mahakama na hasa wananchi.

Kuingiliwa kwa mahakama na bunge kama anavyolia Jaji Mkuu wetu ni uzembe wake yeye mwenyewe, either kwa kutokujua sheria au kwa kuwa fisi, yaani muoga wa wanasiasa, na watu kama Spika wataendelea ku-take hiyo advantage mpaka tutyakapopata Jaji Mkuu anayejua maana hasa ya nguvu ya sheria katika taifa.

Jaji Mkuu wa taifa hatafuti power yake kisheria kwenye majukwaa ya siasa, that is exactly tunachoita a pure nonesense!
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kabisa mahakama inashindwa kuheshimu sheria za taasisi nyengine ,nimeona katika nchi nyengine zilizoendelea baraza la maji na taasisi zingine huwa zinasheria zake na ukizivunja inabidi zichukue mkondo wake ,kitu kimoja ambacho taasisi hizo hapa kwetu zinashindwa kufanya ni wakati pale zinapomkamata mhusika bila ya kumtilisha saini pamoja na mhuri wa kampuni iliyokamatwa kwa ushahidi wa kuwa amekamatwa,ikipatikana hilo taasisi kama hizo akina EWURA hazina haja ya kwenda mahakamani ni kuona sheria yake inafuatwa na ikishindikana kufuatwa ndio hiyo ewura IMFIKISHE MHUSIKA MAHAKAMANI KWA USHAHIDI ule wa kumtilisha saini mhusika pale alipokubali kuwa alitenda kosa.Kuna Nchi unalipishwa fedha kwa kutupa takataka hovyo na hifikishwi mahakamani ila haya yatakamilika wananchi watakapokuwa na ID au National ID.
 

.......Nafikri CJ alikuwa sahihi kusema vile katika hadhira ile..........ni kawaida kabisa kwa kiongozi wa taasisi katika majumuisho yake kwenye hadhira kama ile kuonyesha mafanikio na mapungufu...............HAKUNA TATIZO
..............in short hapa Spika kachemka..............kwa hadhi yako bwana Sita huo ni utovu wa nidhamu kwa taaluma uliyonayo................tena lugha uliyotumia yaonyesha KIBURI.........sijui cheo ndio kinakuwewesesha............au.........

Ushauri mdogo kwa Spika.......siku nyingine kumbuka kuwa ukiulizwa jambo hukatazwi kusema........."NO COMMENT".........

tumeshuhudia kesi za ajabu nyingi na maamuzi mengi ya ajabu mahakamani..........worldwide...........endapo mshitaki/mshitakiwa anakuw ahajaridhika..........na hukumu thats its not the end of the world..........unakata rufaa.............whats the fuss!

Ndg Spika.....don't waste our money and time kujadili jambo lisilo na msingi......i.e. malumbano yasiyo na kichwa wala miguu......damn!
 
Kuna tofauti sana ya majukumu ya spika na Jaji, Spika yuko kwenye political-related post, wakati Jaji yuko moja kwa moja kwenye professional.

Kama swala la kuingilia mahakama basi ni kawaida sana kwa binadamu, tunapenda kuhukumu-na ndio maana wako majaji na mahakimu kuhakikisha haki inatendeka.

Jaji anataka kugeuka kuwa kama Pilato-kuwa powerless? Pilato aliuliza ile kadamnasi mnataka nani afunguliwe Yesu au Baraba? jamii ilisema Baraba-Pilato akaisikiliza jamii! japo alikuwa na uwezo wa kupinga, leo hii inavyoelekea jaji anataka kusikiliza jamii inasemaje na yeye afanyaje..KAA KIMYA, WEWE TUPUUZIE TU, WANAOPUUZIA VIJIMANENO WANAKUWA TRUE PROFESSIONALS, WANAOSIKILIZA SIKILIZA JAMII INASEMAJE, WENGI HAWANA HAKIKA WANAFANYA NINI! mwishowe mtaomba maji mnawe!

Jaji mkuu, anatakiwa awe mkimya na mpole, kama ANAAMINI KUWA WAO WAKO CLEAN, over the time watajijengea heshima, professionals are not for public attention, professionals hufanya maamuzi na mambo hata kama jamii itakasirika, lakini siyo kutaka kuifurahisha jamii, kulia mbele jamii kuwa bunge linaingilia mahakama inashangaza, sasa swali je na nyie MMEINGILIKA?? how??

kama mmefanya kazi yenu kwa taratibu na ethic zinazotakiwa jamii itajua tena,

mimi ni civil engineer, kila siku tunalaumiwa tunafanya kazi vibaya, lakini kila siku majengo yanajengwa! when professionals turns professionalism to politics basi tumekwisha.

Kesho Sita, akikamatwa kwa kuzushiwa uongo maana yake mko tayari kumpeleka jela hata kama hana hatia, kwani anaingilia mahakama!

Jaji mkuu amulikwe nadhani amelianzisha mwenyewe

waandishi, wahabari mpo??
 
Mwaka 1951, katika mji wa Toeka, Kansas Linda Brown aliongozana na baba yake Oliver L Brown kwenda kujiandikishwa katika shule ya jirani ambako watoto wenzake walikuwa wanasoma. Maombi yake yalikataliwa kwa vile yeye alikuwa mweusi na ile shule ilikuwa ya watu weupe. Baba yake, Oliver, akajiunga na wazazi wenzake weusi 12 ambao nao watoto wao walikataliwa kujiunga na shule za watu weupe, kuifungulia mashtaka Bodi ya Education ya Topeka kupinga kanuni zake za ubaguzi katika masuala ya elimu. Kesi hiyo iliitwa Brown v Board of Education of Topeka na ilisimamiwa na wakili mweusi aliyeitwa Thurgood Marshall. Kesi ilienda mpaka Supreme Court ya Marekani. Uamuzi wa Mahakama Kuu ulikuwa ni dhana ya separate but equal ilipingana na Katiba kwa sababu haiwezekani usawa ukapatikana chini ya dhana hii. Uamuzi huu ndiyo ulioashiria mwisho wa ubaguzi wa rangi katika elimu Marekani kote. Mwaka 1955 Dada Rosa Parks alipokataa kumpisha mtu mweupe akae kwenye kiti chake, uamuzi huu, ulichangia katika kumaliza ubaguzi wa rangi katika mabasi ya umma.

Mwaka 1970, Norma L McCorvey ("Jane Roe") alifungua kesi dhidi ya Henry Wade aliyekuwa Distict Attorney wa Dallas County, Texas. Kesi ilihusu haki ya Norma ku'abort' mtoto wake na ilijulikana kama Roe v Wade. Mwaka 1973, Mahakama Kuu ( Supreme Court) ya Marekani iliamua kuwa sheria nyingi za marekani zinazomzuia mwanamke ku'abort' mimba yake zilipingana na haki yake ya chini ya Katiba ya Marekani. Uamuzi huu ndiyo ulio legalize abortion marekani.

Mifano kama hii iko mingi. Hivi karibuni, ni Mahakama Kuu hiyo hiyo iliyoamua kuwa kumnyonga mtoto ni kinyume na Katiba ya Marekani. Ninachotaka kusema kusema kuwa mara nyingi haki ( justice) kwa mwananchi inapatikana mahakamani na sio kwenye bunge. Bunge lingeachiwa, pengine ubaguzi wa rangi ungeendelea kwa muda mrefu marekani kwa sababu wabunge wengi walikuwa weupe na wengi wao wabaguzi. Wabunge hawa waliwakilisha majimbo ambayo majority ya wapiga kura walikuwa wabaguzi. Hawa kama walitaka kuendelea na ubunge wao bila shaka walitakiwa kutetea fikra na imani ya wapiga kura zao. Mahakama Kuu ni tofauti. Wao hawajibiki kwa yeyote kwa hiyo wanachoangalia ni haki basi. Hawatoi uamuzi kwa vile utawafanya kuwa popular au kulinda maslahi yao. Ndiyo maana hata kwetu, ni vigumu sana kwa hata Rais kumfukuza kazi jaji.

Kitu kingine cha msingi ni kuwa Mahakama Kuu inatoa uamuzi wao kutokana na kesi iliyo mbele yao. Mahakama haiwezi kama ilivyopendekezwa na wengine kumfungulia mashtaka Spika. Lakini ni Mahakama hii iliyotoa uamuzi kupinga fee za juu mno zilizowekwa kwa wale waliotaka kupinga matokeo ya uchaguzi. Mahakama iliamua kuwa fee hizi ziliendana kinyume na haki ya mwananchi chini ya katiba ya nchi yake. Ni Mahakama hii hii ndiyo iliyotoa uamuzi kusema kuwa ni haki ya mwananchi kugombea ubunge bila kuwakilisha chama chochote cha siasa (independent candidate). Uamuzi ambao serikali unautilia mikwala mpaka leo. Maamuzi haya yalitokana na kesi zilizopelekwa na wananchi wenye uchungu. Hivi kuna mtu anayeamini kuwa maamuzi kama haya yangeweza kupatikana katika bunge letu la sasa?

Kabla ya kumtupia lawama ni lazima tujiulize ni wangapi katika sisi ambao tumewapelekea kesi ambazo zilipinga sheria za kigandamizi? Si ni wakina Mtikila peke yao wenye ujasiri huo? Na hata akifanya hivyo, wengi wetu tunamuona chizi.

Tofauti na Spika, Jaji Mkuu hana jukwaa formal la kusemea yale aliyoyasema. Hawezi kuamka katikati ya kesi na kutoa malalamiko yake. Alichofanya ni kututetea sisi na kutukumbusha kuwa kuna njia mbadala ya kudai haki zetu za kikatiba. Sasa kwa kufanya hivi, tunambeza kweli? Kweli hatujipendi.

Amandla........
 

Ndugu yangu Fundi Mchundo, uliyoyasema hapo juu ni sahihi kabisa. Ila naomba nitofautiane na wewe kidogo, hasa katika maneno yako niliyoyawekea 'Bold" hapo juu.

Ni kweli kwamba Mahakama ilitoa uamuzi kusema kuwa ni haki ya mwananchi kugombea ubunge bila kuwakilisha chama chochote cha siasa (independent candidate). Katika maelezo yako ya awali, umezungumzia Mahakama za Marekani zilivyofuata Katiba ya nchi katika kutoa maamuzi. Vile vile Katiba yetu inatamka wazi kuwa mtu yeyote atakaeomba kuchaguliwa katika nafasi ya Rais na Ubunge, atatoka katika chama cha siasa kilichosajiliwa kisheria. Je, huoni kuwa mahakama ilitakiwa kufuata Katiba yetu katika kutoa maamuzi?

Mimi ningependa sana Katiba ibadilishwe na itoe uhuru zaidi wa kuchaguliwa kuliko ilivyo sasa. Lakini, kwa sasa, kuchaguliwa bila kuwa na chama ni kinyume cha Katiba na haitafanyika. Hivyo ni vyema Bunge likabadilisha kipengele hicho cha Katiba (walau kwa nafasi za Ubunge) ili kiendane na kipengele kingine cha Katiba hiyo hiyo kinachotoa haki ya kila mtu kupata fursa ya kuchagua na kuchaguliwa bila ubaguzi. Sababu kubwa ya kufanya mabadiliko hayo ni kuweka usawa kati ya wananchi kuchagua kiongozi wanaemtaka bila kuchaguliwa na chama chochote cha siasa ama kikundi kidogo cha watu (ambacho kinapunguza haki hiyo ya kuchagua na kuchaguliwa, kikatiba).
 


Mheshimiwa Recta huo ni mfano mwingine wa mahakama zetu kutoa maamuzi ya ajabu ajabu.Ndiyo maana hata serikali haitaki kuyatekeleza sababu inayaona ni maamuzi ya ajabu ya kipuuzi ambayo hayaangalii kwa upana katiba.Mtu kaangalia kipengele kimoja tu cha katiba huyo akaibuka na hukumu.Tena hakuwa mmoja lilikuwa jopo la majaji.

Nadhani majaji wapandishwe vyeo kwa kuangalia maamuzi yao katika kesi mbalimbali badala ya kuangalia idadi ya miaka waliyokaa wakiwa wamevaa majoho kwenye viti vya hukumu za ajabu ajabu kama hizo.

Sasa serikali ikimcharukia jaji mkuu ikisema uamuzi huo wa mahakama uliotolewa na huyo jaji wa kuruhusu wagombea binafsi ulikuwa wa ajabu ajabu kwa kuwa ulikiuka katiba inayotaka watu wagombee kupitia vyama itakuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama?

Nafikiri jaji mkuu na majaji wenzie inabidi waanze kututhibitishia wananchi kuwa kweli wao ni learned brothers and sisters vinginevyo tutaendelea kuwacharukia bila chembe ya huruma wala lugha nyepesi za kidiplomasia ambazo wangependa Spika azitumie anapowasema wakikosea.
 

Huu si uamuzi wa ajabu ajabu. Katiba zote haziko perfect lakini katika kila Katiba kuna kile kinachoitwa haki ya msingi. Ni wajibu wa Mahakama kuitafsiri wakiangalia haki kwa raia wote wa JMT. Vipengele vinapopingana basi wanatoa tafsiri yao ya kipi ndio kipewe kipaumbele. Kwenye hii ishu Mahakama ilikuwa inaangalia haki ya msingi ya raia wa Tanzania kugombea nafasi yeyote anayotaka. Hiki kipengele kinazuia hiyo. Kwa hali hiyo maamuzi ya Mahakama yalikuwa yanamaanisha kuwa hiki kipengele kinafunikwa na hiyo haki ya msingi. Hiki kipengele kiliwekwa ili kulinda maslahi ya sehemu ya jamii na si jamii yote. Sasa kilichotakiwa ni serikali kukata rufaa na kusema kuwa hiki hakipingani na haki ya msingi ya raia wa JMT. Mbona wanasita kufanya hivyo?

Amandla.....
 

Ni sahihi kabisa Mkuu FM. Kipengele kinachozua mgombea kushiriki uchaguzi kama kibinafsi, kinamnyima mwananchi haki ya msingi. Ila tujue kuwa kipengele hicho kipo na ni sehemu ya Katiba hiyo hiyo. Kipengele kinachoruhusu mtu yeyote kuchaguliwa kikiungana na kipengele kinachotaka mtu huyo awe ametoka katika chama fulani cha siasa chenye usajili wa kisheria, kinafanya vipengele vyote viwe sahihi na kamilifu. Ila, usawa wa wananchi wote kuchaguliwa bila mipaka unapungua kwa kipengele hicho cha pili (mgombea kutoka chama cha siasa).

Katiba ndio sheria kuu kuliko zote hapa nchini. Mahakama, Bunge, Serikali, Taasisi zote na hata wananchi wa kawaida wanatakiwa kuishi Tanzania kikatiba. Hivyo hakuna chombo chochote kilicho juu ya Katiba. Kumbuka, kuna sheria fulani fulani ambazo hutungwa/hurekebishwa na mahakama. Ila sheria hizo zinatakiwa zitungwe/zirekebishwe kwa kuzingatia Katiba ya nchi (Hii ndio sababu Jaji Mkuu wa JMT hana mamlaka katika mahakama za Zanzibar. Kwakuwa wao pia wana Katiba yao).

Endapo itathibitika kuwa sheria zilizotungwa/kurekebishwa na mahakama zinapingana na Katiba, sheria hizo huwa batili mara moja. Mahakama kote duniani (ambapo Katiba hueshimiwa), hufanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba. Katiba ndio iliyounda Mahakama, hivyo ni lazima Mahakama pia ziheshimu Katiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…