Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 42
Pamoja na kukubaliana nawe kuwa haikustahili kwa Jaji Mkuu kutumia njia aliyotumia lakini tunavyoelewa kuwa uongozi ni busara na sio jazba na kejeli.
Sawa Spika amemkejeli Jaji Mkuu kwa kutekeleza yale ambayo yeye Sitta na Wenzake wameyatunga na kuyakabidhi kwa Jaji mkuu ayatekeleze nani mkosa hapa. Huyu alieyetekeleza yale aliyoambiwa ayatekeleze au yule aliyoyatunga na kuamrisha yatekelezwe?
Aidha ubabe ndio kigezo cha uongozi? Sitta anakurupika kwa ubabe huku tukijuwa kuwa huyu Bwana ndiye mwenye wajibu wa kututungia sheria zitakazotulinda sisi hana uwezo wa kurekebisha makosa anapokumbushwa,sasa wananchi tukimbilie wapi?
Ninachoona mimi ni kuwa huyu Mzee sasa anaelekea katika udikteta na kujichukulia maamuzi mikonono mwake. Tuangalie mifano kule Zanzibar Wajumbe wa Baraza kutoka upinzani kila wanapofukuzwa Barazani hukimbilia mahakamani na juu ya siasa za kule hawa wajumbe hushinda na Spika hutekeleza maagizo ya mahakama. Sitta hakuwa na haja ya kutumia lugha ya kejeli kwani kwa upande mmoja yeye ana uwezo wa kuzuia au kurekebisha hayo anayoona kuwa ni mapungufu kwa kufuata SHERIA NA KATIBA au anataka tuelewe kwa vile yeye ni kiongozi wa kutunga sheria basi habanwi na sheria? Do we need to read between the lines ili kufahamu nini Jaji Mkuu anakisema?
Ndugu yangu Ngekewa. Mambo mengi yanayofanyika hapa nchini yanahitaji kujitolea zaidi. Kauli ya kejeli iliyotolewa na Speaker wa BUnge sijaiona. Kama kauli ya "Na hapa watasema naingilia Mahakama, Potelea mbali" ndio kauli ya kejeli, basi nadhani kejeli inabadilika maana. Maana nijuavyo mimi maneno hayo si kejeli bali ni sawa na kusema "Basi acha wachukulie hivyo".
Ndugu yangu, sheria ingekuwa inafuatwa vizuri (inavyotakiwa), malumbano kama haya yasingekuwa na nafasi. Ni kweli kabisa kuwa sheria zinaanza kutozingatia maana ya kuundwa kwake. Inawezekanaje sheria iwe na manufaa kwa mtu mmoja mmoja bila kujali haki sawa kwa wengine (ambao wanaweza kuwa wengi) na mtu atakaelizungumzia hilo aonekane anaingilia mamlaka ya Mahakama? Uingiliaji gani huo wa mamlaka ambao umefanyika baada ya mahakama kuamua? Nadhani uingiliaji ungekuwa wakati/kabla ya mahakama kufanya maamuzi, tungeweza kusema mahakama imeingiliwa na kuwa na haki ya kulaumu uingiliaji huo. Ila kama Mahakama inaelekea kufanya maamuzi yasiyo na mantiki yoyote (yasiyo make any sense) sidhani kama huo ni uingiliaji wa mahakama zaidi ya kulaumu utendaje wake. Mahakama ni zetu kama zilivyo kwa Majaji na Mahakimu wengine. Tunayo haki (na hasa kwa kupitia Bunge letu) kulalamika tunapoona kuwa haki iliyotarajiwa kutolewa na mahakama zetu inatolewa visivyo na hata kusifia endapo tunaona haki inatolewa ipasavyo. Tusizoee kusifiwa tu, tukubali kukosolewa ili tuwe bora zaidi. Majai wanaanza kuelekea kufikiri kuwa Mahakama ni mali yao binafsi. Inawezekanaje kuwa hivyo?