Wanaomlaki Salma wakanwa
Katika mkuano wa jana, Kinana pia alisema viongozi wa serikali wanaoshiriki mapokezi ya Mama Salma Kikwete ambaye ni mke wa mgombea urais wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, wanafanya hivyo kwa utashi wao na hawajaombwa na CCM.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Dk. Slaa kuilalamikia hali hiyo, na kuwaagiza wanasheria wa Chadema kumfungulia mashtaka Mama Salma.
Miongoni mwa madai yanayolalamikiwa na Dk. Slaa ni matumizi ya fedha za umma, yakiwemo malipo kwa viongozi hao wanaposhiriki ziara zake mikoani.
Ziara ya Mama Salma inatajwa kuwa ni sehemu ya kampeni za Uchaguzi Mkuu ambazo hata hivyo hazipo katika ratiba inayotambuliwa na Nec.
Jana, Kinana alilazimika kuwakana viongozi wa serikali wanaoshiriki mapokezi ya Mama Salma, kwa madai kuwa ziara zake (Salma) ni za kichama.
Alisema viongozi wa serikali wanaojiunga katika misafara ya Mama Salma mikoani, wakitumia magari ya serikali `wanajipendekeza' wenyewe na kwamba chama hakiwatumi kufanya hivyo.