Sitta atofautiana na Warioba juu ya kubadilisha Rasimu ya Katiba mpya

Sitta atofautiana na Warioba juu ya kubadilisha Rasimu ya Katiba mpya

Huu ni mkanganyiko... Wariiba alitoa maoni kwa wananchi na wabunge poa ni wawakilishi wa wananchi

Tatizo kubwa

Asilimia kubwa ya wabunge ni wawakilishi wa vyama na si wananchi.
 
Kina Warioba walitembea na kuongea na wananchi na hivyo kutuletea Rasimu hiyo. Hawa wajumbe wamekusanya maoni ya wanaowawakilisha? Wameyakusanyaje?

Kwa namna fulani naona mantiki ya Jaji Warioba. Kama wajumbe hawa wanaweza kubadili hoja ya msingi (bila hata kuwauliza kwanza wananchi), tume ya Jaji Warioba ilikuwa haina maaana. Kina Warioba wasingepoteza resources and muda wao kuzunguka na kukusanya maoni ya wananchi, ikiwa maoni hayo kumbe yangeweza kuletwa na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba!

Mkuu nakubaliana na wewe. Wanadai watu 350000 waliohojiwa na tume ya Warioba ni wachache! sasa nini maana ya sampling? ukubwa na udogo wa sampling unategemea mambo mengi lakini makubwa mawili ni fedha na muda, sasa wenzao nchi zingine tume zimepewa muda wa kutosha na gharama. Hivyo wangehakikisha hayo basi tume ingepanua sampling yake lakini mwisho wa siku ni kwamba bado haingeweza kuhoji waTZ wote. Pili wanazungumzia wajumbe wa bunge maalumu kuwa wawakilishi wa wananchi, hapa kuna mambo mawili: Moja wamechaguliwaje kuwakilisha hao wananchi? pili wapi walikutana na wananchi na kupata misimamo yao? Tume ya warioba ilikutana na wnanchi na kuchukua maoni ya wengi na kuyaweka kwenye rasimu, sasa hawa wajumbe wa bunge maalumu walikutana lini na wananchi wao? Mathalani CCM wanaposema wanataka serikali 2 au CUF/CDM seriakli 3 walikwenda kwenye mashina na kuhoji wanachama wao? Je katiba ni ya watanzania ( 2-4 milion) walioko kwenye vyama au ni ya watanzani wote 45 mil?
 
Mwenzenu hesabu zimenishinda, hivi watu 350,000 na watu 626 wapi ni wengi kama tunataka kufuata maoni. 350,000 walitoa maoni kwa hiari ya mioyo yao, hawa wengine walitangulia kudai posho. Kati yao nani mwenye moral authority ya kudai kuzungumza kwa niaba ya watanzania. 350,000 wanakaa nchi nzima hawa 626 kiasi kikubwa wanaishi Dar japo hudai wanawakilisha watu wa mikoani. Muda ndio utaweza kusema kipi ni kweli.
 
Umeambiwa haya ni maoni ya watu laki tatu tu siyo ya watanzania wote hivyo si mawazo ya wote lazima yabadilishwe pale itakapofaa.

So, unafikiri watu mia sita ni wengi kuliko watu laki tatu? Kwani watu mia sita walioteuliwa na Rais ndio wanawakilisha mawazo ya Watanzania wote? Kwa mfano, wewe unawakilisha Watanzania gani hao? Kama suala ni mawazo ya Watanzania wote, let's go for direct democracy. Kila Mtanzania aulizwe mawazo yake kwa kila suala la kikatiba. Hata ukifanya hivyo, si kila Mtanzania atatoa mawazo yake. Ni utaratibu gani utumike kupata mawazo ya wote?
 
Umeambiwa haya ni maoni ya watu laki tatu tu siyo ya watanzania wote hivyo si mawazo ya wote lazima yabadilishwe pale itakapofaa.
Kama hayo maoni ni ya watu 300,000, sasa hao wabunge 621 wamekusanya lini maoni ya wananchi milioni 40 kwenda kuwasemea huko Bungeni! Kwa sababu, Wabunge wa JMT na Wawakilishi kazi yao tuliyowatuma ilikuwa ni kutunga sheria na kuisimamia Serikali. Masuala ya Katiba nani amewapa Madaraka ya kutuwakilisha kama siyo kuchakachua sheria?
 
Hatuwezi kufata maoni ya watu laki tatu wakati nchi inawatu milioi 45 kamwe hatukubali.

kwa hiyo ni halali kufuata maoni ya wabunge wa Bunge Maalum la Katiba 629 kuliko maoni ya wananchi 350,000. Jaribu kutafuta uwiano ni sampuli ipi inayowakilisha wananchi walio wengi kati ya wabunge na hao wananchi waliotoa maoni kwa tume ya Warioba.
 
hivi rasimu ina tatizo gan had ijadiliwe na hao wachumia tumbo walioko dodoma? wananch wameshatoa maon yao kwann tusiipigie kura ya kuipitisha iwe katiba!? sion umuhimu wa watu kuka dodoma kula kodi yetu halaf watuharibie maon yetu!
 
hivi rasimu ina tatizo gan had ijadiliwe na hao wachumia tumbo walioko dodoma? wananch wameshatoa maon yao kwann tusiipigie kura ya kuipitisha iwe katiba!? sion umuhimu wa watu kuka dodoma kula kodi yetu halaf watuharibie maon yetu!
 
Umeambiwa haya ni maoni ya watu laki tatu tu siyo ya watanzania wote hivyo si mawazo ya wote lazima yabadilishwe pale itakapofaa.

Sasa kwanini walipoteza muda na pesa za walipa kodi kuunda tume ya Warioba kama walijua mawazo yao watayatupa kama hayawapendezi? tungeanza na kura ya maoni hapo ndio wangejua mawazo yetu wananchi sio watulete mambo yao ya misimamo ya kivyama,Nani amewaambia hao wajumbe 621 ndio wamechukua mawazo yetu?ni mbunge gani anaweza kusimama kifua mbele na kusema niliitisha mikutano ya wananchi wangu kwenye jimbo na haya ndio mawazo waliyonituma?
 
Asilimia kubwa ya wabunge ni wawakilishi wa vyama na si wananchi.

wabunge wanachaguliwa na wananchi kutuwakilisha bungeni... ule utumbo unaouona mule ni reflection ya sisi watanzania

vyama ni conduits tu

kwahiyo sie ndio majinga kabisa
 
wabunge wanachaguliwa na wananchi kutuwakilisha bungeni... ule utumbo unaouona mule ni reflection ya sisi watanzania

vyama ni conduits tu

kwahiyo sie ndio majinga kabisa

Mkuu, mbona iko wazi kabisa wabunge baadhi kupitia ccm wanapigania maslahi ya chama? Kilichoandaliwa na tume ya Warioba ndio maoni ya wananchi walio wengi.
 
Katiba ndio she ria mama. Bunge ndio mhimili wa kutnga she ria. Jamani hata mnashindwa kulitambua!!! Kweli Tanzania ina safari ndefu
 
Mkuu, mbona iko wazi kabisa wabunge baadhi kupitia ccm wanapigania maslahi ya chama? Kilichoandaliwa na tume ya Warioba ndio maoni ya wananchi walio wengi.

ni kweli, na huo ndio upuuzi wetu, kwenye kura tunawapigia, wakiwakilisha chama tunalalama

kwenye kampeni si unaona kabisa huwa tunachagua nini??? tena na picha zipo wazi (maana hukawii kuniambia leta picha!!)

tunavuna tulichopanda, hao ndio wawakilishi wa wananchi.... JK anao wachahce sana hapo na hata hao aliwachagua kuwakilisha vikundi mbalimbali

tujialumu wenyewe na sio mtu mwingine yeyote
 
Back
Top Bottom