Mtu wa Pwani,
Ngoma leo ilikuwa nzito sana. Mawaziri wote walikuwa kama wamenyewa mvua kwa jinsi mawe yalivyokuwa yanaishukia serikali. Kwa kifupi ni kwamba serikali imeanikwa hadharani. Point za maana nilizoziona kwenye report ni hizi:
Moja, Kamati Teule inasema kwamba Wizara ya Nishati na Madini ilipata kiburi kutoka juu na ndiyo maana ilifika mahali ilikiuka maamuzi ya Baraza la Mawaziri. Hapo ni MSABAHA ndo alikuwa anakomwa za usoni bila ya woga.
Kutokana na ushahidi wa kimazingira pamoja na mawasiliano kati ya Wizara ya Nishati na Madini na Waziri Mkuu, it seems kwamba Waziri Mkuu aliingilia huo mchakato na Wizara ilikuwa inafanya kazi kwa maelekezo ya Waziri Mkuu. Msabaha na Kazaura walijitetea kwamba huo mradi ulikuwa wa EL na RA (lakini maelezo hayo yako nje ya kiapo na hivyo kamati inayachukulia kama minong'ono).
Mwanasheria Mkuu wa Serikali hakujua lolote linaloendelea kwenye hiyo mikataba mibovu yenye 'UJASIRI WA KIFISADI", kwa hiyo nae ametakiwa awajibishwe.
PCCB wanatakiwa kubadilishiwa uongozi kwa kuwa report yao ilisema mambo yalikuwa poa wakati wao (Kamati) wamekuta kuna uozo, na hivyo PCCB imepoteza imani kwa wananchi.
Timu iliyoundwa na EL kwa ajili ya majadiliano ikiwakilisha serikali imetakiwa iwajibike (hiyo ni kamati ya makatibu wakuu wa Wizara ya Fedha, Nishati na Madini na pia Mwanassheria Mkuu wa Serikali).
Karamagi ametakiwa awajibike kwa kuendelea kutetea RDC pamoja na kujua kwamba lilikuwa ni bomu (Karamagi aliwatetea RDC mara baada ya kuingia Wizarani, nae ameangikwa msalabani).
Mamvi kapewa option ya kuchagua kusuka ama kunyoa. Kamati haijapendekeza lolote, bali wamesema kwamba kulingana na nafasi yake na ushiriki wake kwenye mchakato na jinsi ofisi yake ilivyoingilia swala hilo Kamati imesema ataangalia afanye nini kutokana na maudhui ya report.
Kamati imependekeza mikataba yote iwe wazi ili kuepuka madudu ya RDC. Na ishughulikiwe kikamilifu.
Hayo ndiyo niliyoyadaka kwa kifupi kutoka kwenye mapendekezo.