Sitta: Katiba mpya izuie rais kubeba familia yake

Sitta: Katiba mpya izuie rais kubeba familia yake

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
666
Reaction score
426
WAZIRI wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amewasihi Watanzania wazuie katiba mpya isitoe rais dikteta na mwenye kutumia madaraka vibaya kwa kuinufaisha familia yake au jamaa walio karibu naye.

Sitta amesema analiona taifa linaelekea kwenye hatari kubwa, kwamba baadhi ya viongozi wanahangaika kuingiza mambo binafsi yenye maslahi ndani ya rasimu ya katiba mpya badala ya kuangalia utaifa.

“Hawa wanaoingiza mambo yao binafsi si watu wazuri kwa taifa letu, tukiwaacha waendelee na mchezo wao katiba mpya itakuwa chungu sana kwetu,” alisema.

Sitta alisema Watanzania wanatakiwa kutengeneza katiba nzuri itakayomzuia rais atakayechaguliwa kuwa mroho na kutumia madaraka yake kuinufaisha familia yake au jamaa walio karibu naye.

Kiongozi huyo alitoa onyo hilo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Taifa la Vijana la Rasimu ya Katiba mpya unaotarajia kumalizika kesho.

Sitta alisema misingi ya utawala bora ndiyo silaha kubwa ya kuhakikisha viongozi wanaochaguliwa hawafanyi kazi kwa udikteta au masilahi binafsi.

“Nawasihi ndugu zangu tusikubali katiba mpya ijayo ikachezewa na wajanja wachache maana tukifanya hivyo kuna hatari tukatengeneza rais na serikali ya kidikteta” alisema.

Alisema kwa muda mrefu Tanzania imekuwa na historia ya kufuata misingi ya utawala bora hivyo ni vizuri jambo hilo likaendelezwa.

Sitta alibainisha kuwa katiba ni muhimu kwa mustakabali wa Tanzania na lazima wananchi wajenge utamaduni kuiheshimu na kuilinda huku wakiwaepuka watu wanaotaka kuwania madaraka kwa masilahi binafsi.

“Tunahitaji kiongozi mwenye kujali masilahi ya Watanzania, hatuhitaji yule mwenye kujali tumbo lake au la familia yake, haya yote yatafanikiwa kama tutaweka vipengele kwenye katiba yetu itakayowabana watu wa aina hiyo,” alisema.

Muundo wa Muungano
Waziri Sitta alisema rasimu ya katiba mpya ilenge kupunguza gharama za uendeshaji wake kwa sababu Watanzania ni masikini na wanahitaji maendeleo.

Alibainisha kuwa hakubaliani na mapendekezo ya rasimu ya katiba mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya uwepo wa mawaziri 15 kwenye Serikali ya Muungano ilhali mambo ya Muungano yapo saba.

Aliongeza kuwa wabunge 150 na mawaziri 15 wa Serikali ya Muungano ni kutapanya fedha za walipakodi wanadidimia kwenye lindi la umasikini.

“Wananchi wanahitaji maendeleo, tujikite kupunguza matumizi na mbwembwe mbwembwe zisizo na tija kwa taifa,” alisema.

Alisema nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikisuasua kupiga hatua kwenye maendeleo kwa kuwa fedha nyingi zinatumika kwenye uendeshaji wa serikali badala ya kupelekwa katika sekta zenye kuwainua kiuchumi wananchi.

Apinga marais watatu
Sitta alipendekeza kuwa kama muundo wa serikali tatu unaopigiwa debe na baadhi ya watu utafanikiwa ni vema vyeo vya marais wawili wa Zanzibar na Tanganyika vikafutwa ili kuiepusha nchi kuwa na marais watatu.

Alisema nchi mbalimbali zitaicheka Tanzania kama itakuwa na marais watatu ambao wote inaweza ikatokea wakakutana nje ya nchi.

“Tutakuwa watu wa ajabu sana huko kwa wenzetu, yaani sisi masikini halafu tuna marais watatu? Hizi gharama tunazotaka kumtwishwa mwananchi za nini?” alihoji.

Alisema kama kutakuwa na serikali tatu ni vema kukawepo na rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wengine wakapewa majina mengine kama Makamu wa Rais au Waziri Mkuu.

Sitta aliongeza kuwa hapingi muundo wa serikali tatu, bali hakubaliani na hoja ya uwepo wa marais watatu.

Aliongeza kuwa hoja ya kutaka marais hao watatu inashabikiwa na wenye uroho wa madaraka, wanaodhani inaweza kuwa njia rahisi kwao kufikia malengo yao ya kisiasa.

“Kuna watu wana kiu kubwa ya kuitwa mheshimiwa rais, ndiyo maana wanapigia debe uwepo wa marais watatu, nawaona ni wabinafsi tu hawana jambo jingine,” alisema.
 
Kuhusu Raisi kuibeba familia yake, hii imekaa vip jamani? Any Reference?
 
Kuhusu Raisi kuibeba familia yake, hii imekaa vip jamani? Any Reference?

We huna reference? Ulichelewa wapi ukapitwa?hujui kuwa Salma ni MH president wa wanawake na Riz ni rais wa vijana mapapaa tanzania? Umewhi kuuona msafara wa salma wewe? Full jwtz,ffu,uwt,migambo nk,uliwahi kuona hayo kwa Mama sitti mwinyi?
 
We huna reference? Ulichelewa wapi ukapitwa?hujui kuwa Salma ni MH president wa wanawake na Riz ni rais wa vijana mapapaa tanzania? Umewhi kuuona msafara wa salma wewe? Full jwtz,ffu,uwt,migambo nk,uliwahi kuona hayo kwa Mama sitti mwinyi?
labda timu nzima ya watoto kukaa magogoni, wengine inabidi wabaki bagamoyo
 
Safi sana six..hawa watu wanatafuna nchi utazania sio watanzania,yaani wao ni kuloot kila kukicha.mtoto analoot,mama anatumia vibaya..baba yeye ndio kabisaa,kazi kukenua meno na kutalii ulaya kila kukicha...kwa sasa anajiandaa kwenda kumpongeza mwana mfalme mpya. pheeeeew!
 
Huyo sitta anawivu wa madaraka tu hana mpya wala nini kwa sababu Jk kamwaga usipika .
 
Nchi kuwa na marais watatu ni kichekesho. Hata hawa wawili ilikuwa kichekesho tu. suluhisho ni kuwa na rais mmoja

Zenji atawale Gavana na tz bara Atawale Gavana Kama ilivyo kule USA kisha Raisi mmoja tu tena aishi Dodoma kinyume na hapo Muungano utaendelea kulalamikiwa milele
 
Huyu mzee unafiki utammaliza!
Sasa amedakia issue ya ufisadi wa mabilioni ziara za wakubwa hapa nchini.
Huyu mzee inabidi awaache ccm akajenge chama chake cck!
 
Viongozi wa Tanganyika na Zanzibar ama waitwe mawaziri wakuu au magavana, hiyo itaondoa utata kwenye tafsiri. Mawaziri wa serikali ya muungano wasizidi 8, kwa maana ya waziri katika kila jambo la muungano pamoja na mawaziri wawili wakaazi kutoka kwa washirika wa muungano kila mmoja. Waziri atakayeshughulika na sarafu na benki kuu kwa maana ya waziri wa fedha ndio huyo huyo atakayekua waziri wa ushuru wa bidhaa na maduhuli yatokanayo na mambo ua muungano. Rasimu haijasema kwamba lazima mawaziri wawe 15 ila imesema wasizidi.
 
Kuhusu Raisi kuibeba familia yake, hii imekaa vip jamani? Any Reference?

Nini hukuelewa? Jaribu hii; Baba ni M/kiti wa Chama, Salma na Riz1 wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama, Waziri X?.ni Shemeji yake, Mkuu wa wilaya? huko wilaya ya mkoani Tanga ni Mshikaji wake, nk nk nk
 
Ubinafsi ndo dhambi inayoitafuna nchi hii,binafsi si mulaum six kwakuwa alichosema ndo ukweli kama unabisha wewe ni mnafiki na mungu hapendi wanafiki.nchi kuwa na maraisi watatu ni kichekesho hawa waliopo kila siku kuomba nje,na madeni ndo yanazidi,na serikali ndo nazid kufilisika hadi mnataka tulipe kodi za line za simu.
Mim ninavyojua watu wawili mnapoungana manake mnataka kuwa na nguvu ya pamoja,ili iwe rahis kupambana na changamoto za kiuchumi,kijamii na kisiasa,lengo likiwa ni kupunguza gharama za maisha nakusonga mbele kiuchumi,na ustawi wa jamiii husika.
Sasa kwa nini kulazimisha muungano wakati haulet nafuu ya maisha kwa wananchi walio wengi kama vipi zanzibar ijitegemee na tanganyika ijitegemee ubaki ujirani kama nchi zingine.
 
Huyo sitta anawivu wa madaraka tu hana mpya wala nini kwa sababu Jk kamwaga usipika .[/QUOT
inawezekana kweli kama binadamu akawa na wivu wa mdaraka na kwakuwa anasifa zote za kutawala si dhambi,mana alichosema hapa ni ukweli mtupu au kwako ni uongo?
Lakin kama kweli ulichosema kuwa alimwagwa uspika basi ni kwa sababu yakusimamaia ukweli
tatizo nchi hii wengi hawapendi ukweli na huu ndo unafiki ambao mungu hapendi.
Lakin lazima kutambua kuwa penye ukweli uongo hujitenga na haki ya mtu haipotei bure itacheleweshwa tu.
 
wivu huondosha hekima....Tanzania ndiyo itakuwa nchi ya kwanza dunia familia ya rais isihumiwe na Ikulu.
 
Nchi kuwa na marais watatu ni kichekesho. Hata hawa wawili ilikuwa kichekesho tu. suluhisho ni kuwa na rais mmoja

Saa nyingine huwa napata shida sana kuwaelewa hawa viongozi wa ccm, yaani nakosa jata niwafananishe na nini, yaani Sitta anazingumzia utawala wa kifamilia wakati yeye yuko bungeni na mke wake, hata kuna wakati yeye akiwa spika mke ni waziri na alikuwa amamuwekea kifua najeyi yake isihojiwe na wabunge,
hawa ccm wamezeeka kama chama chao, hadi wanavikana vivuli vyao RIP chama cha zamani
 
Huyo sitta anawivu wa madaraka tu hana mpya wala nini kwa sababu Jk kamwaga usipika .

Wivu unaweza kuwa wenye kutoa chachu kwa ajili ya maendeleo ama kudumaza. Kama ni kwa ajili ya maendeleo inabidi upewe nafasi hata kwa kulazimisha
 
Back
Top Bottom