Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo sitta anawivu wa madaraka tu hana mpya wala nini kwa sababu Jk kamwaga usipika .
Sitta amtukana JKikwete,Mama Salma,Rithwan
WAZIRI wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amewasihi Watanzania wazuie katiba mpya isitoe rais dikteta na mwenye kutumia madaraka vibaya kwa kuinufaisha familia yake au jamaa walio karibu naye.
Sitta amesema analiona taifa linaelekea kwenye hatari kubwa, kwamba baadhi ya viongozi wanahangaika kuingiza mambo binafsi yenye maslahi ndani ya rasimu ya katiba mpya badala ya kuangalia utaifa.
"Hawa wanaoingiza mambo yao binafsi si watu wazuri kwa taifa letu, tukiwaacha waendelee na mchezo wao katiba mpya itakuwa chungu sana kwetu," alisema.
Sitta alisema Watanzania wanatakiwa kutengeneza katiba nzuri itakayomzuia rais atakayechaguliwa kuwa mroho na kutumia madaraka yake kuinufaisha familia yake au jamaa walio karibu naye.
Kiongozi huyo alitoa onyo hilo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Taifa la Vijana la Rasimu ya Katiba mpya unaotarajia kumalizika kesho.
Sitta alisema misingi ya utawala bora ndiyo silaha kubwa ya kuhakikisha viongozi wanaochaguliwa hawafanyi kazi kwa udikteta au masilahi binafsi.
"Nawasihi ndugu zangu tusikubali katiba mpya ijayo ikachezewa na wajanja wachache maana tukifanya hivyo kuna hatari tukatengeneza rais na serikali ya kidikteta" alisema.
Alisema kwa muda mrefu Tanzania imekuwa na historia ya kufuata misingi ya utawala bora hivyo ni vizuri jambo hilo likaendelezwa.
Sitta alibainisha kuwa katiba ni muhimu kwa mustakabali wa Tanzania na lazima wananchi wajenge utamaduni kuiheshimu na kuilinda huku wakiwaepuka watu wanaotaka kuwania madaraka kwa masilahi binafsi.
"Tunahitaji kiongozi mwenye kujali masilahi ya Watanzania, hatuhitaji yule mwenye kujali tumbo lake au la familia yake, haya yote yatafanikiwa kama tutaweka vipengele kwenye katiba yetu itakayowabana watu wa aina hiyo," alisema.
Muundo wa Muungano
Waziri Sitta alisema rasimu ya katiba mpya ilenge kupunguza gharama za uendeshaji wake kwa sababu Watanzania ni masikini na wanahitaji maendeleo.
Alibainisha kuwa hakubaliani na mapendekezo ya rasimu ya katiba mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya uwepo wa mawaziri 15 kwenye Serikali ya Muungano ilhali mambo ya Muungano yapo saba.
Aliongeza kuwa wabunge 150 na mawaziri 15 wa Serikali ya Muungano ni kutapanya fedha za walipakodi wanadidimia kwenye lindi la umasikini.
"Wananchi wanahitaji maendeleo, tujikite kupunguza matumizi na mbwembwe mbwembwe zisizo na tija kwa taifa," alisema.
Alisema nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikisuasua kupiga hatua kwenye maendeleo kwa kuwa fedha nyingi zinatumika kwenye uendeshaji wa serikali badala ya kupelekwa katika sekta zenye kuwainua kiuchumi wananchi.
Apinga marais watatu
Sitta alipendekeza kuwa kama muundo wa serikali tatu unaopigiwa debe na baadhi ya watu utafanikiwa ni vema vyeo vya marais wawili wa Zanzibar na Tanganyika vikafutwa ili kuiepusha nchi kuwa na marais watatu.
Alisema nchi mbalimbali zitaicheka Tanzania kama itakuwa na marais watatu ambao wote inaweza ikatokea wakakutana nje ya nchi.
"Tutakuwa watu wa ajabu sana huko kwa wenzetu, yaani sisi masikini halafu tuna marais watatu? Hizi gharama tunazotaka kumtwishwa mwananchi za nini?" alihoji.
Alisema kama kutakuwa na serikali tatu ni vema kukawepo na rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wengine wakapewa majina mengine kama Makamu wa Rais au Waziri Mkuu.
Sitta aliongeza kuwa hapingi muundo wa serikali tatu, bali hakubaliani na hoja ya uwepo wa marais watatu.
Aliongeza kuwa hoja ya kutaka marais hao watatu inashabikiwa na wenye uroho wa madaraka, wanaodhani inaweza kuwa njia rahisi kwao kufikia malengo yao ya kisiasa.
"Kuna watu wana kiu kubwa ya kuitwa mheshimiwa rais, ndiyo maana wanapigia debe uwepo wa marais watatu, nawaona ni wabinafsi tu hawana jambo jingine," alisema.
WAZIRI wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amewasihi Watanzania wazuie katiba mpya isitoe rais dikteta na mwenye kutumia madaraka vibaya kwa kuinufaisha familia yake au jamaa walio karibu naye.
Sitta amesema analiona taifa linaelekea kwenye hatari kubwa, kwamba baadhi ya viongozi wanahangaika kuingiza mambo binafsi yenye maslahi ndani ya rasimu ya katiba mpya badala ya kuangalia utaifa.
Hawa wanaoingiza mambo yao binafsi si watu wazuri kwa taifa letu, tukiwaacha waendelee na mchezo wao katiba mpya itakuwa chungu sana kwetu, alisema.
Sitta alisema Watanzania wanatakiwa kutengeneza katiba nzuri itakayomzuia rais atakayechaguliwa kuwa mroho na kutumia madaraka yake kuinufaisha familia yake au jamaa walio karibu naye.
Kiongozi huyo alitoa onyo hilo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Taifa la Vijana la Rasimu ya Katiba mpya unaotarajia kumalizika kesho.
Sitta alisema misingi ya utawala bora ndiyo silaha kubwa ya kuhakikisha viongozi wanaochaguliwa hawafanyi kazi kwa udikteta au masilahi binafsi.
Nawasihi ndugu zangu tusikubali katiba mpya ijayo ikachezewa na wajanja wachache maana tukifanya hivyo kuna hatari tukatengeneza rais na serikali ya kidikteta alisema.
Alisema kwa muda mrefu Tanzania imekuwa na historia ya kufuata misingi ya utawala bora hivyo ni vizuri jambo hilo likaendelezwa.
Sitta alibainisha kuwa katiba ni muhimu kwa mustakabali wa Tanzania na lazima wananchi wajenge utamaduni kuiheshimu na kuilinda huku wakiwaepuka watu wanaotaka kuwania madaraka kwa masilahi binafsi.
Tunahitaji kiongozi mwenye kujali masilahi ya Watanzania, hatuhitaji yule mwenye kujali tumbo lake au la familia yake, haya yote yatafanikiwa kama tutaweka vipengele kwenye katiba yetu itakayowabana watu wa aina hiyo, alisema.
Muundo wa Muungano
Waziri Sitta alisema rasimu ya katiba mpya ilenge kupunguza gharama za uendeshaji wake kwa sababu Watanzania ni masikini na wanahitaji maendeleo.
Alibainisha kuwa hakubaliani na mapendekezo ya rasimu ya katiba mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya uwepo wa mawaziri 15 kwenye Serikali ya Muungano ilhali mambo ya Muungano yapo saba.
Aliongeza kuwa wabunge 150 na mawaziri 15 wa Serikali ya Muungano ni kutapanya fedha za walipakodi wanadidimia kwenye lindi la umasikini.
Wananchi wanahitaji maendeleo, tujikite kupunguza matumizi na mbwembwe mbwembwe zisizo na tija kwa taifa, alisema.
Alisema nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikisuasua kupiga hatua kwenye maendeleo kwa kuwa fedha nyingi zinatumika kwenye uendeshaji wa serikali badala ya kupelekwa katika sekta zenye kuwainua kiuchumi wananchi.
Apinga marais watatu
Sitta alipendekeza kuwa kama muundo wa serikali tatu unaopigiwa debe na baadhi ya watu utafanikiwa ni vema vyeo vya marais wawili wa Zanzibar na Tanganyika vikafutwa ili kuiepusha nchi kuwa na marais watatu.
Alisema nchi mbalimbali zitaicheka Tanzania kama itakuwa na marais watatu ambao wote inaweza ikatokea wakakutana nje ya nchi.
Tutakuwa watu wa ajabu sana huko kwa wenzetu, yaani sisi masikini halafu tuna marais watatu? Hizi gharama tunazotaka kumtwishwa mwananchi za nini? alihoji.
Alisema kama kutakuwa na serikali tatu ni vema kukawepo na rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wengine wakapewa majina mengine kama Makamu wa Rais au Waziri Mkuu.
Sitta aliongeza kuwa hapingi muundo wa serikali tatu, bali hakubaliani na hoja ya uwepo wa marais watatu.
Aliongeza kuwa hoja ya kutaka marais hao watatu inashabikiwa na wenye uroho wa madaraka, wanaodhani inaweza kuwa njia rahisi kwao kufikia malengo yao ya kisiasa.
Kuna watu wana kiu kubwa ya kuitwa mheshimiwa rais, ndiyo maana wanapigia debe uwepo wa marais watatu, nawaona ni wabinafsi tu hawana jambo jingine, alisema.
Mke wa Rais je? tujue wajibu wake na mipaka!!
unataka uniambie ndivyo michelle obama anavyofanya kwa mumewe kama festileideee wa waamerika? ha ha haWajibu wa mke wa rais ni kukaa home na kuhakikisha mume wake anakula vizuri na kupata nafasi ya kupumzika.. Na vile vile kuiangalia familia yake kwa kuwa mumewe hatakuwa na muda wa kutosha kutokana na majukumu makubwa ya kuliongoza ya taifa.. Hicho ndicho alichokifanya mama Maria.. Hawa wa kisasa unawaona muda hata hawana.. mashindano yako kwenye dubious taasisi..
mume kiguru na njia, mke naye kiguru na njia velevile sasa hata mila za ndoa sijui zinatekelezwa vipi?Wajibu wa mke wa rais ni kukaa home na kuhakikisha mume wake anakula vizuri na kupata nafasi ya kupumzika.. Na vile vile kuiangalia familia yake kwa kuwa mumewe hatakuwa na muda wa kutosha kutokana na majukumu makubwa ya kuliongoza ya taifa.. Hicho ndicho alichokifanya mama Maria.. Hawa wa kisasa unawaona muda hata hawana.. mashindano yako kwenye dubious taasisi..
mume kiguru na njia, mke naye kiguru na njia velevile sasa hata mila za ndoa sijui zinatekelezwa vipi?
unataka uniambie ndivyo michelle obama anavyofanya kwa mumewe kama festileideee wa waamerika? ha ha ha
umenena mkuu, binafsi nilikuwa sijajua namna ya kumwelezea huyu mtu. :A S thumbs_up:Binafsi huwa namuona Mh Sitta kama muimba taarabu tu. Ni mtu wa vijembe na wa kulia na malalamiko mengi. Sio mtu wa action yeye ni kuropoka tu kila kukicha. Ajifunze kuchukua hatua kama kiongozi na sio kupiga vijembe kama anaimba taarabu. Hafai kuwa kiongozi mkuu wa nchi.
Kuhusu Raisi kuibeba familia yake, hii imekaa vip jamani? Any Reference?