Sitta ameshaahidi kuendeleza mapambano na mafisadi hata bila kuwa Spika wa bunge. Hili bila shaka alikusudia kulifanya akiwa mbunge wa kawaida kwa njia ya kuihoji serikali. Lakini sasa kwa kuchaguliwa kuwa Waziri anajikuta mahali pa kuulizwa yeye maswali na kuyajibu.
Serikali iliyopo leo ndiyo ile ile aliyoitikisa jana akionesha kuwa imejaa mafisadi. Sasa ni sehemu ya serikali hiyo. Kuendelea kuitikisa akiwa waziri humo ndani kwa ndani ni sawa na kusukuma gari ukiwa wewe mwenyewe uko ndani yake, unaabiri. Simply impossible.
Sasa kwa dhamiri yake Sitta itafanyaje kama kweli anataka kuitii? Maamuzi mengi ni dhahiri yatapingana na dhamiri yake, naye atalazimika kuyatetea, mfano ni bei ya bati iliyokubalika EAC. Option ni moja tu, KUJIUZULU uwaziri na kurudi bungeni kama muuliza maswali. Ushujaa huo ataumudu?