Sumbalawinyo
JF-Expert Member
- Sep 22, 2009
- 1,282
- 248
6 Amefutwa machozi lakini macho yake bado mekundu wizara aliyopewa haimrudishii heshima aliyokua nayo kwa kulinda heshima yake angekataa hiyo post
hivi kabla hawajatangazwa.....huwa wanaambiwa kwanza?...
Hakustahili kuwa kwenye baraza!
Hilo nalo nenoSitta ameshaahidi kuendeleza mapambano na mafisadi hata bila kuwa Spika wa bunge. Hili bila shaka alikusudia kulifanya akiwa mbunge wa kawaida kwa njia ya kuihoji serikali. Lakini sasa kwa kuchaguliwa kuwa Waziri anajikuta mahali pa kuulizwa yeye maswali na kuyajibu.
Serikali iliyopo leo ndiyo ile ile aliyoitikisa jana akionesha kuwa imejaa mafisadi. Sasa ni sehemu ya serikali hiyo. Kuendelea kuitikisa akiwa waziri humo ndani kwa ndani ni sawa na kusukuma gari ukiwa wewe mwenyewe uko ndani yake, unaabiri. Simply impossible.
Sasa kwa dhamiri yake Sitta itafanyaje kama kweli anataka kuitii? Maamuzi mengi ni dhahiri yatapingana na dhamiri yake, naye atalazimika kuyatetea, mfano ni bei ya bati iliyokubalika EAC. Option ni moja tu, KUJIUZULU uwaziri na kurudi bungeni kama muuliza maswali. Ushujaa huo ataumudu?
MAFISADI wamemfanyia kweli tena Mhe Sitta!!!!
Kwa heshima zote EAC si wizara bali ni Idara mojawapo katika Wizara ya Mambo ya Njee. Kawekwa pale strategically ili:
(1) ASIPATE mwanya wa kushughulika na mambo yatakayomfanya aendelee kuvutia kwetu sisi Wananchi kwa sababu hiyo wizara wala haitugusi, pia
(2) ni kumkomesha huko kwa sababu Idara hiyo ya EAC siku zote haina bajeti, programu wala mashirika ya kusimamia.
(3) Kumfunika mdomo na dhana ya 'Jukumu la Pamoja kwa Baraza la Mawaziri' kusudi akose uwanja mmpana wa kukemea bali kutumikia MAFISADI. Ndio hivyo kapatikana mtego wa pili tena!!!
Anyway, kibendera kitakwepo kwenda kijijini na kaulinzi.