SITTA na CCM wameanza tayari kukiuka kanuni BMK

SITTA na CCM wameanza tayari kukiuka kanuni BMK

Babu Kijana

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2013
Posts
587
Reaction score
276
Jamani wanajamvi Tundu Lisu kahoji bungeni leo juu ya tangazo kuwa Rais atahutubia bunge baada ya Warioba kuwasilisha rasimu bungeni kuwa ni kinyume na kanuni zilizopitishwa, na pia wabunfe watapata siku 3 za kuzungumza na kuchangia lolote baada ya hapo. Kwa mtazamo wangu hapo ccm wanajiandaa kutoka nje ya ajenda ili kutumia muda huo kuharibu mawazo ya watu na kuchomeka ajenda zao za serikali mbili.

Kwa hili wapinzani na wananchi tusitegemee katiba ya maoni yetu bali ya ccm, Sitta ameanza kuonyesha uccm mapema tu na huko tuendako hali itakuwa mbaya zaidi.
 
Acha woga kupata katiba ni mpaka watu wazungumze na kufika mwafaka haya mengine hofu zenu tu.
 
Daaah hata mimi nimeshangaa. Siku tatu kusema chochote???
 
Shida uking'atwa na nyoka hata jani likikugusa unaruka!

  • A%20S%20confused.gif

Lissu kama kawaida yake hata jambo limeeleweka yeye lazima achomeke hoja yake,, Sitta c yule mliyemzoea aliyewapa ujiko cdm sasa amelitambuwa kosa
 
Lissu alishiriki kutunga hizo kanuni za bunge maalumu la katiba kwa hyo hajafanya kosa kumkumbusha sitta kuwa anazikeuka hizo kanuni ila kama kawaida ya sitta katia maneno matatu na busara za hapa na pale bs wanaccm wakamalizia na makofi yao kumpa support fundi samwel.
 
Bunge la Katiba limetumia wiki tatu na mabilioni ya pesa za posho kuandaa kanuni, halafu kanuni hazizingatiwi mapema hivi?????!!!!! Shame on you Sitta, you have stepped off on the wrong foot! Lazima Warioba azungumze baada ya ngonjera za KINAFIKI zilizozoeleka za Kikwete,"Tuwaze juu ya Utaifa", huku moyoni anataka kura za wazi kuwadhibiti CCM. Baada ya Presentation ya Warioba, inatakiwa ianze kazi moja kwa moja, na siyo kurudi nyuma tena kusikia habari za Fast Jet!!!!!
 
Lissu kama kawaida yake hata jambo limeeleweka yeye lazima achomeke hoja yake,, Sitta c yule mliyemzoea aliyewapa ujiko cdm sasa amelitambuwa kosa

Kanye ulale hujui unachoongea
 
Sitta ni mnafiki sana basi tu watu wanampenda na,kumshabikia pasipo kuangalia matendo yake
 
Sitta ni mnafiki sana basi tu watu wanampenda na,kumshabikia pasipo kuangalia matendo yake

sijawahi kumuamini mwanaccm hata kidogo.pamoja na kumpenda na kumheshimu sana mwl., ukweli ni kwamba nilianza kumuamini alipokufa.MY MOTTO IS; NEVER TRUST A CCM MEMBER UNLESS DEAD
 
Kama walishindwa kutuletea vazi la taifa pamoja na kutumia mamia ya mamilioni ya wapiga kura, je wataweza kutuletea katiba mpya?
 
kwa hiyo huyo SITTA kasemaje baada ya kukumbushwa na lissu kwamba anaenda kinyume na kanuni?
 
Lissu kama kawaida yake hata jambo limeeleweka yeye lazima achomeke hoja yake,, Sitta c yule mliyemzoea aliyewapa ujiko cdm sasa amelitambuwa kosa

si bure mkuu unaham njoo kalenga usuguliwe
 
Kwa hili la katiba hamna ubabe zaidi ya mezani usiwe na hofu kijana wa nchi
 
Sitta ni mnafiki sana basi tu watu wanampenda na,kumshabikia pasipo kuangalia matendo yake
Na bado mie nina wasiwasi hata kile kikanuni cha uwazi/siri lazima sitta atatupiga bao, ntamkumbuka Mkosamali alivopayuka juzi kwa bunge kupitisha kanuni mbovu...
 
Magwanda hamuishi kuja na hoja muflis.

Siku tatu kwa watu 629 ni nyingi?
 
Back
Top Bottom