Jamani wanajamvi Tundu Lisu kahoji bungeni leo juu ya tangazo kuwa Rais atahutubia bunge baada ya Warioba kuwasilisha rasimu bungeni kuwa ni kinyume na kanuni zilizopitishwa, na pia wabunfe watapata siku 3 za kuzungumza na kuchangia lolote baada ya hapo. Kwa mtazamo wangu hapo ccm wanajiandaa kutoka nje ya ajenda ili kutumia muda huo kuharibu mawazo ya watu na kuchomeka ajenda zao za serikali mbili.
Kwa hili wapinzani na wananchi tusitegemee katiba ya maoni yetu bali ya ccm, Sitta ameanza kuonyesha uccm mapema tu na huko tuendako hali itakuwa mbaya zaidi.