Sitta: Nipo tayari kwa hukumu yoyote CCM

Muulizeni kuhusu wabrazil..sitta nae msanii. Mtu mwenye namba yake amuuize kuhusu wa brazil walimpa nini..Hili ni swala la 2015. No one cares about mafisadi kiivyo. NI siasa tuu.
 
unaweza kumchukia mtu tu bila sababu au ukiwa na wasiwasi anaweza kuwa na madaraka unayoyatamani. ikitokea sababu yeyote inaweza kuirukia na kudai hiyo ndio sababu kumbe kivyako una lako jambo
 

Sio Sitta kukosa uPM?
 
Sasa Mkandara sijui ulitaka kushauri kwamba Sitta ajiondoe ccm au aache kukemea mabaya katika chama chake. Si mnasema change has to come from within? If so why are we discouraging those starting internal combustion that may bring about change?

Mgonjwa wa Ukimwi,

You can not bring changes from within by backing off, bali kwa kusonga mbele. Internal combustion unayoiongelea wewe ni kwamba fuel yake imeisha, so moto umezimika ghafla wakati watu tulikuwa tunasubiri kuona wakiendelea kuukoleza zaidi kwa kuongeza fuel. Alichofanya Sitta na wenzake kule kwenye vikao vya Bunge ni kwamba wame-surrender na wamekubali yaishe na huo ni ushindi kwa Lowassa & Co (mafisadi).

Yaliyotokea Bungeni ndiyo yaliyosababisha hadidu za rejea za Kamati ya Mwinyi zibadilishwe na kuongezewa muda. Ndiyo maana vikao vya CC na NEC vilikuwa vinasogezwa sogezwa ili kuona msimamo wa Bunge. Iwapo Bunge lingeendelea kukomaa, hapo ningekubali kwamba moto wa mabadiliko unaanzia ndani.

Leo hii Sitta na wenzake wakisimama wakasema wanapinga ufisadi na ilihali tumeona wameshindwa kuikomalia serikali kwenye utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu Richmond, watu wataendelea kuwaamini kwamba wanapingana na ufisadi?

Kusema ataendelea kukemea ufisadi, it is OK. Lakini hiyo ni sawa na mbwa anayebweka na ilihali hana meno ya kuuma. Mwisho wa siku wezi wakija wanapora na kuondoka zao. Sasa hivi akina Lowassa wataanza kusuka deals nyingine wakijua kwamba hao wapinga ufisadi hawana ubavu wa kuwashughulikia zaidi ya kulalamika kwenye magazeti na kusema wanasuluhishwa.
 
Hivi ni sababu zipi zinazopelekea Sitta kuwa described as kiongozi wa kundi la wana-CCM wanapoinga ufisadi?Hivi sio Sitta huyuhuyu aliesababisha Zitto Kabwe asimamishwe ubunge kwa muda kwa "kosa" la kueleza ukweli kuhusu Karamagi na Buzwagi?Au sio Sitta huyuhuyu aliyetishia kumburuza Dr Slaa kwenye vyombo vya sheria kwa "kosa la taarifa za kizushi kuhusu EPA"?

Binafsi namwona Sitta kama msanii flani aliyeibinafsisha ishu ya ufisadi kwa manufaa yake ya kisiasa ilhali hakuna ushahidi wowote kuwa uumini wake katika mapambano dhidi ya ufisadi.

Magazeti yetu nayo yameingia mkenge na kuendelea kum-describe kama kinara wa kundi linalopinga ufisadi.Uhasama wake na hao mafisadi hausababishwi na utetezi wa maslahi ya taifa bali maslahi binafsi.
 

I think we shouldn't reduce Bunge's power's to Sitta's. Sitta, as an individual has come out to condemn ufisadi irrespective of NEC decision that appears to warrant victory to Lowassa & Co. I think change is innevitable if we could have as many Sittas as possible within CCM.
 
Makamba ampaka mafuta Sitta kwa mgongo wa chupa
Exuper Kachenje:Mwananchi


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Spika wa Bunge Samuel Sitta yuko huru kuendeleza mapambano ya ufisadi kwa kuwa kufanya hivyo si kosa.

Katibu Mkuu Yusuf Makamba aliliambia gazeti hili jana kuwa anayepigana na ufisadi ni mtu safi.

Alisema hayo alipozungumza na gazeti hili kuhusu kauli ya Spika Sitta kwamba yuko tayari kwa hukumu yeyote itakayotolewa na Chama chake, CCM endapo msimamo wake wa kupinga ufisadi, rushwa na maovu ndani ya chama hicho, utaonekana kuwa kosa.

"Anayepigana na rushwa, anayepigana na ufisadi au maovu, ni mtu safi," alisema Makamba.

Alisema sio kosa wala uvunjifu wa katiba kwa mwanaCCM kupinga ufisadi kwa kuwa hii ni moja ya sera za Chama Cha Mapinduzi.

"...Ukiniuliza msimamo wa Chama nitakwambia mapambano dhidi ya rushwa na maovu ni sera ya CCM," alisema Makamba na kuongeza:

"Hata kanuni za chama zinasema hivyo. Katika ahadi za mwanachama, ahadi ya sita inasema, 'Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa na huo ndio msimamo wetu,"

Alisisitiza "Yeyote anayepigana na rushwa, anayepigana na ufisadi ni mtu mwema. Rushwa ni adui wa haki."

Makamba alipuuza msimamo wa baadhi ya wanaCCM wanaopinga vita ya rushwa akisema haina maana. "Watu gani wanasema hivyo? umeniuliza msimamo, nimekupa. WanaCCM wote wanaapa 'Sitatoa wala kupokea rushwa' na huo ndio msimamo wetu CCM kwamba, rushwa ni adui wa haki,"alisema.
 

Mkuu wangu, nadhani nimetumia muda kuzubgunzia ile mifano ya Sitta ktk kuhalalisha aloyafanya. Mifano yake hailingani kabisa na hili sakata la Mafisadi ndani ya chama..
Na sintashtuka mshipa akisema amekubali kushindwa na yaishe! kwa sababu anachodai kugombea na ataendelea kugombea ndicho kilichowapatanisha.
.
Ebu fikiria kwa makini swala zima, ikiwa chanzo cha mgogoro wake na hawa jamaa ni kuwaita Mafisadi, kuwakemea na kutaka waondolewe ktk (chama) kanisa lao. Leo kumefanyika suluhu iweje tena yeye aendelee kupiga kelele hali upatanisho wao ni pamoja na kumkataza yeye asipige kelele za kuwaita mafisadi?..
Leo tunaambiwa CCM hawatazungumzia tena swala la Richmond na yeye ni kinara wa kuhakikisha halizungumziwi iweje yeye tena awe wa kwanza kumlaani shetani?.

Alichotakiwa kufanya ni maamuzi ya haki na kuwatendea haki wananchi na wanachama wa CCM....Yeye kama kiongozi hicho kitabu chake cha dini (katiba ya chama) kinamwabia nini? Ikiwa katiba inamwambia kuiba ni haramu, iweje kiongozi wa juu kama yeye akubali makosa yaliyofanywa na viongozi wenzake yaishe hivi hivi kwa suluhisho ambalo linawaweka viongozi hao ktk ngazi ya kuendelea kuiba...hayo maafikiano kikomo cheke ni wapi?..kifupi kama umemsoma vizuri makubaliano yao ni katika kutokuita Koleo ni Kolea, bali Koleo liitwe kijiko..kelele atazipiga lakini kwa kuita koleo ni kijiko, na hakika Wadanganyika wengi tutaamini.

Unajua mkuu wangu siku zote kuna watu humu waliwaita hawa wapiganaji kama ni zuga na wasanii nilipinga sana maneno hayo na kuomba sote tuwaunge mkono na kuwa nao pamoja ktk vita hii, lakini haya majibu ya Sitta na kikao kizima cha chama yameniondoa nguvu kabisa ya upatikanaji wa haki nchini na pengine kudharau kabisa maamuzi ya viongozi ktk swala ambalo litakigharimu chama na pengine uchaguzi mzima..
Maamuzi haya yatafungua ukurasa mpya wa hoja magazetini na ktk kila vyombo vya habari. binafsi sielewi kabisa kilichomkuta Sitta..Nina hakika wananchi wengi wameshtushwa na maamuzi hayo tofauti na yeye alivyofikiria..

Tatu, Labda muhimu zaidi angekaa kimya kama Kikwete, tubakie kudhania hili ama lile...kwani sasa yaonyesha wazi kabisa kwetu ya kuwa yale yote alokuwa akituhumiwa yeye kama ni mtu anayetaka kukigawa chama ni ya kweli, na ili upatikane msamaha kwake na hao kundi lake kutovuliwa Unachama basi wakae kimya kabisa kuhusiana na swala la Richmond!..Je kukaa kimya na kutojadili tena swala la Richmond ndio kupiga kelele kupi kwingine!
Kundi la Lowassa ni wakosa na kundi lake Sitta (wapiga kelele) ni wakosa vile vile...hakuna saint baina yao!
 
soma post no 1#
Hilo ndilo jibu ukisoma vizuri maneno yake six nafikiri yalikuwa yanatoka moyoni.

Mengi tumeongea wengine wametoa mifano ya chama kama kanisa nawauliza kwani muumini kuhama au kufukuzwa kanisani ndio ku solve tatizo jibu si kweli ni kulifanya hilo kanisa liwe na waumini waoga wanafiki Sitta hatakiwi aondoke mule hivyo ndio kuomaa kwa chama na mwanachama

mnataka kila mpinga ufisadi aondoke CCM wabaki kina nani kwa sababu wakitoka au six akitoka kwa mazingira tuliyonayo Tanzania hatapata nafasi ya kusikilizwa kama aliyonayo sasa akiwa bado ndani say awe upinzani wengi mtamgeuka na kuanza kumwambia anapiga kelele kwa sababu ni mpinzani kazi yake ni kupinga chochote kama wanavyoambiwa kina Slaa

mimi bado nina imani na six ingawa ana mapungufu yake lakini amelibadili bunge kwa kipindi kifupi wabunge wengi wa CCM hawakutarajia na hawajakuwa tayari kupokea mabadiliko wamezoea bunge la chama kimoja serikali ilizoea kila hoja yake ikiletwa bungeni inapita bila kupingwa mabadiliko haya ndiyo yanamfanya Sitta aonekane kama anakisaliti chama na serikali tatizo hili limetukumba hata sisi tuliokuwa tunalilia mabadiliko bungeni hatukumbuki miaka mitano iliyopita bunge lilikuwaje

wengi tunataja matokeo ya bunge la 18 lililopita hatuangalii mazingira mazima yaliyopelekea hadi hoja ya Richmond ikapita hatujiulizi hii hoja imetoka wapi na lini zaidi ya miaka mingapi sasa imepita imefanya karibu serikali ivunjike hadi PM kujiuzuru kitu ambacho hakijawahi wala kutegemewa kutokea

imagine lingekuwa bunge la mwaka 2000 la Msekwa sijui kama tungekuwa bado tunaongelea habari ya Richmond nafikiri wengine tungekuwa tumesahau yes kaonyesha weakness lakini bado tumpe credit yake ukilinganisha na maspika waliomtangulia
 

Luteni, haya maneno mazito mno na uchambuzi wake umetulia...you are a great thinker in my opinion.
 
Sio Sitta kukosa uPM?

Nafikiri cheo alichonacho Sitta ni kizito na chenye heshima kuliko huo uPM, uPM ni one man shoo siku yeyote aliyekuweka pale na si baraza la mawaziri akishauriwa vibaya usiku na mamusapu umekwenda na maji lakini spika lazima bunge lipige kura na three quarters ya wabunge lazima ikubali
 

Mwaka 2015 nitachukua formu na kuomba nipewe na nina imani kubwa ya kupewa! baada ya hapo nitakamilisha kazi moja tu ya kuleta maendeleo hapa Tanzania. Lakini watu wakorofi, wabinafsi na maadui wa maendeleo ya NCHI YETU WATASALIMU AMRI. LET US KEEP PRAYING!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…