Kinyambiss
JF-Expert Member
- Dec 2, 2007
- 1,374
- 73
Muulizeni kuhusu wabrazil..sitta nae msanii. Mtu mwenye namba yake amuuize kuhusu wa brazil walimpa nini..Hili ni swala la 2015. No one cares about mafisadi kiivyo. NI siasa tuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chanzo kikuu cha uhasama wala si Richardmonduli ni Uspika Msekwa baada ya kuukosa uspika aliondoka kwa kinyongo akaanza kuwatumia wanamtandao bungeni ionekane six hawezi kazi alipotokea Richardmonduli six akasema hamadi kibindoni Mungu anipe nini na yeye akaanza kumtumia Richardmonduli kuwamaliza wanamtandao hiyo ndiyo sinema lakini steringi mkuu ni Msekwa, EL na RA wanaingia kwenye sinema hii kwa sababu tu ni wahusika wakuu wa Richmond vingevyo bado uhasama ungekuwepo kati ya Msekwa na Sitta.
Sasa Mkandara sijui ulitaka kushauri kwamba Sitta ajiondoe ccm au aache kukemea mabaya katika chama chake. Si mnasema change has to come from within? If so why are we discouraging those starting internal combustion that may bring about change?
Mgonjwa wa Ukimwi,
You can not bring changes from within by backing off, bali kwa kusonga mbele. Internal combustion unayoiongelea wewe ni kwamba fuel yake imeisha, so moto umezimika ghafla wakati watu tulikuwa tunasubiri kuona wakiendelea kuukoleza zaidi kwa kuongeza fuel. Alichofanya Sitta na wenzake kule kwenye vikao vya Bunge ni kwamba wame-surrender na wamekubali yaishe na huo ni ushindi kwa Lowassa & Co (mafisadi).
Yaliyotokea Bungeni ndiyo yaliyosababisha hadidu za rejea za Kamati ya Mwinyi zibadilishwe na kuongezewa muda. Ndiyo maana vikao vya CC na NEC vilikuwa vinasogezwa sogezwa ili kuona msimamo wa Bunge. Iwapo Bunge lingeendelea kukomaa, hapo ningekubali kwamba moto wa mabadiliko unaanzia ndani.
Leo hii Sitta na wenzake wakisimama wakasema wanapinga ufisadi na ilihali tumeona wameshindwa kuikomalia serikali kwenye utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu Richmond, watu wataendelea kuwaamini kwamba wanapingana na ufisadi?
Kusema ataendelea kukemea ufisadi, it is OK. Lakini hiyo ni sawa na mbwa anayebweka na ilihali hana meno ya kuuma. Mwisho wa siku wezi wakija wanapora na kuondoka zao. Sasa hivi akina Lowassa wataanza kusuka deals nyingine wakijua kwamba hao wapinga ufisadi hawana ubavu wa kuwashughulikia zaidi ya kulalamika kwenye magazeti na kusema wanasuluhishwa.
Kwa hiyo mzee Mkandara unataka kutoa suluhisho gani hapa? Nimejaribu kukusoma mara kadhaa bila kuambulia mantiki.
Nijuavyo mimi kanisa ni la watu na wanaoweza kulibadirisha ni waumini wake, wanaoweza kubadirisha imani za kanisa ni waumini wake na sio vinginevyo. Sitta ni miongoni mwa waumini wa kanisa lake (CCM) wanaoweza kuchochea mabadiriko, ni miongoni mwa watu wanaoweza kubadiri imani ya kanisa lake.
Sasa Mkandara sijui ulitaka kushauri kwamba Sitta ajiondoe ccm au aache kukemea mabaya katika chama chake. Si mnasema change has to come from within? If so why are we discouraging those starting internal combustion that may bring about change?
soma post no 1#Sitta anadanganya.je yuko tayari kufukuzwa chama?
Hilo ndilo jibu ukisoma vizuri maneno yake six nafikiri yalikuwa yanatoka moyoni.soma post no 1#
Hilo ndilo jibu ukisoma vizuri maneno yake six nafikiri yalikuwa yanatoka moyoni.
Mengi tumeongea wengine wametoa mifano ya chama kama kanisa nawauliza kwani muumini kuhama au kufukuzwa kanisani ndio ku solve tatizo jibu si kweli ni kulifanya hilo kanisa liwe na waumini waoga wanafiki Sitta hatakiwi aondoke mule hivyo ndio kuomaa kwa chama na mwanachama
mnataka kila mpinga ufisadi aondoke CCM wabaki kina nani kwa sababu wakitoka au six akitoka kwa mazingira tuliyonayo Tanzania hatapata nafasi ya kusikilizwa kama aliyonayo sasa akiwa bado ndani say awe upinzani wengi mtamgeuka na kuanza kumwambia anapiga kelele kwa sababu ni mpinzani kazi yake ni kupinga chochote kama wanavyoambiwa kina Slaa
mimi bado nina imani na six ingawa ana mapungufu yake lakini amelibadili bunge kwa kipindi kifupi wabunge wengi wa CCM hawakutarajia na hawajakuwa tayari kupokea mabadiliko wamezoea bunge la chama kimoja serikali ilizoea kila hoja yake ikiletwa bungeni inapita bila kupingwa mabadiliko haya ndiyo yanamfanya Sitta aonekane kama anakisaliti chama na serikali tatizo hili limetukumba hata sisi tuliokuwa tunalilia mabadiliko bungeni hatukumbuki miaka mitano iliyopita bunge lilikuwaje
wengi tunataja matokeo ya bunge la 18 lililopita hatuangalii mazingira mazima yaliyopelekea hadi hoja ya Richmond ikapita hatujiulizi hii hoja imetoka wapi na lini zaidi ya miaka mingapi sasa imepita imefanya karibu serikali ivunjike hadi PM kujiuzuru kitu ambacho hakijawahi wala kutegemewa kutokea
imagine lingekuwa bunge la mwaka 2000 la Msekwa sijui kama tungekuwa bado tunaongelea habari ya Richmond nafikiri wengine tungekuwa tumesahau yes kaonyesha weakness lakini bado tumpe credit yake ukilinganisha na maspika waliomtangulia
Sio Sitta kukosa uPM?
Nimesema siku zote kwamba mtu ama kiongozi yeyote anayekubali kupeana mkono na Shetani basi huyo sii kiongozi..
Mi sielewi ni imani ipi anayozungumzia Mzee Sitta?.. Huyu Lowassa na Rostam hawa kwa pamoja ni muumini wa chama CCM. Wote wako kanisa moja, wana imani moja wanachotofautiana ni vitendo vyao, hivyop Upatanisho pekee ambao unaweza kuleta maana ni pale huyu Sitta atakapo kataa uongozi wa hawa watu ndani ya kanisa lake..
Mfano wake wa Katoliki/Protentant au Karume na Seif hii ni mifano dhaifu sana kwani hawa watu wanatengana kiimani kwanza, tafsiri ya imani zao ktk kumjenga binadamu zinagongana na hawaelewani kiimani. Kwa hiyo tunachoona kwao ni suluhu baina ya imani mbili tofauti kuweka amani baina yao.. Yaani kifupi amini unachoamini nami nitaamini nachoamini usiwalazimishe watu wangu kufuatana imani yako. lakini ktk swala la Sitta, hii ni suluhu ya waumini wenyewe wenye imani moja ambao kati yao kuna wale wanaokiuka maadili ya imani tangulizi. Kupinga kwa Sitta ndani ya imani hiyo hakuwezi kuwasaidia wauumini wala kuwalinda dhidi na vitendo dhalimu vya hawa viongozi.
Hivyo basi suluhu ya mzee Sitta ni ktk kukubali yaishe, wameshinda wao!...ni suluhu inamhusu yeye binafsi au chama (kanisa) na sii kwa maslahi ya upatanisho wa imani mbili tofauti wananchi bali upatanisho wa matendo..in other word, shake hand with a devil, kwani unaweza kumlaani shetani kanisani lakini ukaendeleza ushetani nje ya kanisa!
Lawama zote nazipeleka kwa baba wa Taifa, marehemu mwalimu Nyerere ambaye alirithisha madaraka ya nchi yetu kwa wahuni! Haya nayoyasikia leo ni uhuni mtupu..Na matokeo yote ya Ufisadi na uharamia nchini umetokana na mwalimu mwenyewe kukabidhi nchi yetu watu wasiofaa kabisa kuwa viongozi...Kikwete hawezi kubadilisha kitu na hakuna kiongozi yeyote anayeweza kubadilisha hali hii issipokuwa kiongozi dikteta kama Kagame ambaye aliwaxhalaza bakora kwanza Wahutu na Watusi hadi wakaweka akili, wakanyooka kisha ndio akaweza kuiendeleza nchi... kinyume cha hapo tusahau na haihitaji elimu ya juu sana kuelewa.
Na nasema hivi, haitatokea kiongozi yeyote ambaye ataweza kuirudisha nchi yetu ktk mstari pasipo kuwa Dikteta.. na hakika kura yangu nitampa..
Wakati wa kudanganyana umekwisha!..Iwapo imani ya Sitta ni kuukashifu Ufisadi kanisani wakati akijua fika kwamba kanisa lake mwenyewe linaendesha sala za kumshirikisha shetani sijui atachoweza kukemea ni kitu gani..