Wana JF wote na wapenda Demokrasia Tanzania,
Tunajua kile kinachoendelea mpaka sasa kule Dodoma. Kwamba Bunge la Katiba mpya limeshaanza na wiki hii wanategemea kuchagua Mwenyekiti wa Bunge ambaye ataendesha vikao vyote kwa siku 60-80 zilizobakia.
Kuna watu 2 wanaopigiwa upatu kutaka kuwania nafasi hii nao ni Mhe. Samwel Sitta aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa aliyeondolewa kwa mizengwe ya kwamba ili aendelee kuwa Spika alitakiwa awe Mwanamke kitu ambacho hakikuwezekana na nafasi ikaenda kwa Bi Anne Makinda!
Kwa safari hii ya kutaka kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge hili muhimu na la Kihistoria kwa Watanzania Mhe.Sitta ametangaza nia ya kugombea nafasi hii.Kama kawaida ya CCM mizengwe ilishaanza ya kumpiga madongo huku mbaya wake Mhe. Andrew Chenge(MB-Bariadi Magh.)akitaka naye kugombea nafasi hiyo muhimu.
Namheshimu Andrew Chenge kama Mbunge wa Wanyantuzu huko Usukumani lakini katika hili la kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge la Katiba namtaka Chenge akae pembeni hatatufaa. Andrew Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakti wa Awamu ya 3 ya Utawala wa Ben Mkapa. Kila Mtanzania ana kumbukumbu ya Mikataba mibovu ya Wawekezaji na Ununuzi wa Ndege ya Rais na Rada. Tunajua Chenge alikutikana na kiasi cha Tshs. 2 Bilioni kwenye offshore Akaunti huko New Jersey na akadai kuwa hivo vilikuwa vijisenti tu!!!!
Kwa sifa hizi za Andrea Chenge kumpa nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge la Katiba ni kutaka kutowatendea haki Watanzania lakini pia itakuwa ni aibu kwa dunia kuruhusu mtu anayetuhumiwa kwa UFISADI kuwa Mwenyekiti wa Bunge linaloenda kutunga Katiba ambayo ni sheria mama. Kwa mtazamo huo ama Chenge atachukua hiyo nafasi hataweza kuvumilia sheria na taratibu zilizomo kwenye Rasimu ya Katiba mpya hasa zenye kugusa mambo ya Ufisadi na Ubadhirifu wa Fedha za Watanzania!!!!
Namaliza kwa kusema kuwa Mhe. Samweli Sitta ndiye anayefaa kuwa Mwenyekiti wa Bunge hili la Katiba kwa wakti huu.Hatutaki kusikia ngonjera za ma-CCM za kutaka kupindisha taratibu ili kuweka Mwenyekiti wao ambaye watamwendesha kwa remote-control. Hii Katiba ni ya Watanzania na siyo ya CCM pekee!
Naomba kuwasilisha.