Sitta: Nitagombea Uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu naamini kuwa nina sifa za kutosha

Sitta: Nitagombea Uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu naamini kuwa nina sifa za kutosha

Simuungi mkona Sitta hadi nijue ana msimamo wa serikali ngapi.. Mbili, tatu au moja. Msimamo wangu ni serikali moja

Umesahau tuu.Sita huyu huyu ndio alisemaga hakuna nchi duniani ina maraisi watatu .
 
Hapo kamera za bunge(cctv) ziimarishwe,mzee wa vijisenti anaweza akamwaga tena unga kwenye ukumbi usiku wa manane.
 
Six hana lolote lengo lake ni kujiimarisha kwenye kinyanganyiro cha urais 2015. Ccm wakimkubali sawa na kula matapishi. Akiwa spika aliidhallisha serekali yake ya ccm. Msimkubali wapo watu wenye sifa za kutosha. Mwanzilishi wa ccj anachotaka ni urais lakn achore hapo chini bora tumpe Silaa.
 
6 is th right # but ccm watatengeneza zengwe ili kumkwamisha
 
chenge pamoja na makashfa machafu yote anataka nafasi nyeti kama hii.kwani akiendelea pandu kificho kuna tabu gani
 
Umesahau tuu.Sita huyu huyu ndio alisemaga hakuna nchi duniani ina maraisi watatu .

Siyo kazi ya spika kuamua Serikali ziwe ngapi. Ni kazi ya wajumbe na wabunge. Ila kama tukisema tunahitaji spika ni wazi Sita ana sifa zilizotukuka na ana uzoefu pia. Mimi ninaamini ana uwezo wa kuwatendea haki wote bila kujali U-chama ila anaweza kuangalia kama hoja hazivunji kanuni za bunge.

Ukizingatia kuwa ni yeye tu mwenye uwezo na sifa bila kusahau uzoefu na uwezo binafsi nadhani itakuwa ujuha tu kama hatapewa nafasi hiyo. Naamini akipewa hata wapinzani watampa kura zao. Guys tunahitaji spika atakayeendesha bunge kwa haki na uadilifu. Hatuhitaji spika wa CCM au CHADEMA
 
Wote! Nasema wote Sitta na Chenge hawafai kuwa kufikiriwa kwenye nafasi hiyo!
Kumfikiria mtu kama Chikawe ni aibu sana na kuwadhalilisha common wananchi!

Inashindikana nini kumpata Spika ambaye hatokani na chama cha siasa hasa CCM?
 
Wana JF wote na wapenda Demokrasia Tanzania,

Tunajua kile kinachoendelea mpaka sasa kule Dodoma. Kwamba Bunge la Katiba mpya limeshaanza na wiki hii wanategemea kuchagua Mwenyekiti wa Bunge ambaye ataendesha vikao vyote kwa siku 60-80 zilizobakia.

Kuna watu 2 wanaopigiwa upatu kutaka kuwania nafasi hii nao ni Mhe. Samwel Sitta aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa aliyeondolewa kwa mizengwe ya kwamba ili aendelee kuwa Spika alitakiwa awe Mwanamke kitu ambacho hakikuwezekana na nafasi ikaenda kwa Bi Anne Makinda!

Kwa safari hii ya kutaka kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge hili muhimu na la Kihistoria kwa Watanzania Mhe.Sitta ametangaza nia ya kugombea nafasi hii.Kama kawaida ya CCM mizengwe ilishaanza ya kumpiga madongo huku mbaya wake Mhe. Andrew Chenge(MB-Bariadi Magh.)akitaka naye kugombea nafasi hiyo muhimu.

Namheshimu Andrew Chenge kama Mbunge wa Wanyantuzu huko Usukumani lakini katika hili la kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge la Katiba namtaka Chenge akae pembeni hatatufaa. Andrew Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakti wa Awamu ya 3 ya Utawala wa Ben Mkapa. Kila Mtanzania ana kumbukumbu ya Mikataba mibovu ya Wawekezaji na Ununuzi wa Ndege ya Rais na Rada. Tunajua Chenge alikutikana na kiasi cha Tshs. 2 Bilioni kwenye offshore Akaunti huko New Jersey na akadai kuwa hivo vilikuwa vijisenti tu!!!!

Kwa sifa hizi za Andrea Chenge kumpa nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge la Katiba ni kutaka kutowatendea haki Watanzania lakini pia itakuwa ni aibu kwa dunia kuruhusu mtu anayetuhumiwa kwa UFISADI kuwa Mwenyekiti wa Bunge linaloenda kutunga Katiba ambayo ni sheria mama. Kwa mtazamo huo ama Chenge atachukua hiyo nafasi hataweza kuvumilia sheria na taratibu zilizomo kwenye Rasimu ya Katiba mpya hasa zenye kugusa mambo ya Ufisadi na Ubadhirifu wa Fedha za Watanzania!!!!

Namaliza kwa kusema kuwa Mhe. Samweli Sitta ndiye anayefaa kuwa Mwenyekiti wa Bunge hili la Katiba kwa wakti huu.Hatutaki kusikia ngonjera za ma-CCM za kutaka kupindisha taratibu ili kuweka Mwenyekiti wao ambaye watamwendesha kwa remote-control. Hii Katiba ni ya Watanzania na siyo ya CCM pekee!

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom