SITTA: Serikali tatu ni kujitafutia ulaji.

....kuwa na mawazir 15 tu watakaokuwa wanashughulikia mambo 7 tu ya muungano
Ndo hiki ambacho na mimi nakiuliza, mawaziri 15 wa Muungano wanashughulikia mambo 7, kwa vipi?

Halafu Kilimo, kwa mfano, sio jambo la Muungano, maji, ufugaji, sio jambo la Muungano, kwa hiyo kukiwa kuna njaa msimuulize Rais, hayamhusu! Kituko.

Mambo ya Nje, kwa mfano, ni jambo la Muungano, Rais ataenda kwenye vikao vya UN, lakini zikianza topic za FAO au UNESCO itabidi Rais atoke nje ya kikao, kwa sababu Kilimo wala sayansi na utamaduni wala watoto (UNESCO) wala afya (WHO) hayamhusu, hatujamtuma! Akienda UN tunataka aingie vikao vya Security Council, UNHCR, wakimbizi, etc. kwa saab wakimbizi na uraia na mipaka inamhusu.

Sasa, wote tunajua tunapokwenda UN mambo ya security council sisi vi nchi vilivyo kwenye ukingo wa dunia huku ni watazamaji tu, kwa saab hatuna hata viwanda vya kutengeza visu, hata wangesema kuanzia sasa tupigane kwa majambia tu, nuclear weapons marufuku bado yasingetuhusu, kwa hiyo kule UN yanayotuhusu sisi ni agenda za kuchimba visima, madawati ya UNESCO, mambo ya vyandarua vyandarua na chanjo za dege dege na electrolytes za utapiamlo. Lakini hayo sio maswala ya Muungano, Rais akienda huko asiyaongelee!

Akidharau hayo mantiki, hayo makubaliano, akaenda UN akaingia vikao vya FAO na UNESCO na WHO basi huku nyuma tunalianzisha tena, amepoka madaraka ambayo hayapo kwenye enumerated powers. Maandamano kwa kwenda mbele, migomo, minong'ng'ono, mabomu, machozi, vitu vyenye ncha kali, tunarudi pale pale, problem unsolved!

In fact the problem is beyond unsolved, it is unsolvable. Huwezi kuwa na nchi ya watu milioni 45 wakaungana na kisiwa cha milioni moja ushee halafu mkataka kubaki na uwiano sawa wa madaraka.
 
mzee wetu inaonekana kwenye vikao rasmi maoni yake hayapewi uzito na ndo maana anatafuta majukwaa ya kutolea maoni yake.
 

Hoja ni iliopo ktk rasimu, sasa yeye Sita alipaswa kutuambia ni jinsi gani ataadress issues za muungano mathalani mgawanyo wa rasilimali na sovereignty ya nchi washirika kwa kutumia present structure au muungano wa serikali 1!
 
kwani muungano ni lazima - tuaweza kuwa na mahusiano ya kama ya marekani na japani kama hofu ni ulinzi. ondoa hiyo kitu kila nchi ichambue gharama zake ikiwa huru
 
zama zake zimeisha na zimeshidwa apumzike aache nchi yetu....huo muungano wao mbona unamigogoro kishenzi ...mbona nchi maskikni kama walikua wazuri...???
 
Kipindi cha uongozi wake yapo mengi tu aliyotakiwa kuyasimamia alipokuwa kama kiongozi sasa naona bora tu aachane na siasa akapumzike maana hatoyaweza tena kwa kuwa hawa viongozi atakaokuwa anawashauri hawatachelewa kumwambia kuwa anafikiri kwa kutumia Masaburi
 
...Hatutakuwa na katiba yenye misingi ya mawazo binafsi,bali tutakuwa na katiba yenye sauti ya watanganyika wote..
 
Tuheshimu maoni yake, ndiyo maana ya demokrasia. Tumpinge kwa hoja, na si kwa matusi na kejeli.
Samuel Sitta anataka serikali mbili ili kupunguza ulaji. Yuko tayari kuunga mkono seikali mbili, ya Tanzania na Tanganyika ili mzigo wa muungano uhamie Zanzibar?
 
Kumjadili Sitta ni kupoteza muda wetu muhimu tu!!
 
Naona hamtaki kuumia akili kumuelewa sitta, actually mim namuunga mkono...ni kwamba inabidi kimoja kikubaliwe either serikali 2 ambayo madaraka makubwa yatakua kwa tz bara kama ilivyo sasa kwasababu ya uwingi wa rasilimali watu na vitu au muungano uvunjwe coz hatuwezi kuumiza vichwa kwa vijitu mil 2 na nusu wkat sisi tupo mil45 na tuna kila kitu...kwani ni lazima znz iwepo?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 

Kama Zanzibar wameweza kuiongoza serikali yao kwa kipindi chote hicho pamoja na kwamba ipo ndani ya muungano. Tanganyika itashindwaje kuiongoza serikali yake ikiwa ndani ya muungano?

Anasahau kuwa Tanganyika ina rasilimali, watu pamoja na mali nyingi kuliko visiwani.

Anatafuta cheap populariy.................... ngoja kama hatanyang'anywa kadi ya chama soon!
 
Hoja ya wabunge2 ni ulaji kweli,lakini serikali3 hakuna ulaji hapo ni kutokana hali halisi wa wazanzibar wengi wanaamini serikali3 ndiyo wanaweza kupata zanzibar huru
 
Alivyokuwa kwenye mkutano huko kanda ya Ziwa alisikitika sana kuona kwenye rasimu mpya ya katiba imeruhusu serikali tatu naye kwa kukurupuka akasema sasa nini maana ya serikali tatu yaani nchi moja itakuwa na marais watatu?Lol hapa kaniacha hoi kabisa huyu ndio Waziri na aliyekuwa Speaker wa Bunge before.

Kasema kwenye Ilani ya CCm hakuna serikali tatu,kasema sie kama CCM ilani yetu inatambua serikali mbili ambazo ni ya Zanzibar na ile ya Muungano sasa basi kama kweli yeye kama waziri na mtu mzima mwenye akili timamu je hiyo nchi nyingine ambayo iliunganika na Zanzibar na kuform serikali ya Muungano iko wapi?

Bora angesema hii rasimu ni nzuri kwa kuwa sasa hata watoto wadogo watafahamu ni nchi gani ziliunda serikali ya Muungano na sio kusema ati ilani ya Ccm inasema serikali mbili,Binafsi nataka kumwambia Huyu mzee Samuel Sitta kwamba katiba inayokusudiwa sio ya CCM kama yeye anavyofikiria wajua unaweza kumuona mtu mzima kavaa suti na mvi kibao ukasema huyu ana busara lakini kumbe ni kopo yupo yupo tu kwa maslahi yake binafsi.

Katiba si mali ya CCm,Chadema,Liberal Cuf,NCCR na vyama vingine katiba ni ya wote walio na chama na wasio kuwa na vyama,ni ya wazee,watoto,wamama,wadada,wakaka,wagonjwa wa akili,nk.

Tunasema Muungano ulipatikana na nchi mbili ambazo ni Tanganyika na Zanzibar so now what we need ni kuona serikali ya Tanganyika ikirudi so moja kwa moja hata mtu wa kutoka Marekani au Ulaya anafahamu kuna Tanganyika na Zanzibar the waliunganika na kuwa na serikali ya Umoja na kuna mambo ambayo hayahusu Muungano so kila upande unajiamulia nini ufanye lakini likija swala la muungano basi linashughulikiwa na Muungano.We need to see Tanganyika.

Hakuna kulala tutakomaa hadi kieleweke Wazanzibar wenzangu this is the time hakuna kurudi nyuma.
 
Lakini8 jambo ambalo linasikitisha ni kwamba hii rasimu imepata kigugumizi kutamka Tanganyika na kuendelea Tanzania Bara. Kama unavyohoji, ni nchi ipi hii iliyoungana na Zanzibara hata kupatikana Tanzania? Hii haihitaji elimu ya chuo kikuu. Serikali ya Tanganyika is a must. Aidha, ni lazima ifahamike kuwa Katiba siyo mali ya chama cho chote bali ni ya nchi. Sasa ukimsikia kiongozi wa ngazi ya juu kama huyu mzee anasema CCM haitaki unashindwa kushangaa. Tatizo ninaloliona kuwa hii ya Katiba haikuwa na wala haiko kwenye manifesto ya CCM. Kwa maana hii pengine ilisadikika kuwa CCM ingeweza kuingilia mchakato wa kuandaa rasimu na kuhakikisha kuwa aina ya muungano ulioko haubadiliki lakini sasa baada ya kutoka imekuwa ni tofauti kabisa na matarajio. What next? Kilichobaki ni kuona ni kwa jinsi gani ya kuboresha hiyo rasimu lengo likiwa ni upatikanaji wa serikali ya TANGANYIKA.
 
Mia kwa mia tunataka serikali ya TANGANYIKA IRUDI na sio eti TANZANIA BARA lol!!jina gani hili.Watanzania tunataka serikali ya TANGANYIKA,TANGANYIKA na si vinginevyo.
 
Hakuna mnafiki kama huyo sita duniani! Mbona hajashangaa nchi moja kuwa na maraisi wawili kama ilivo sasa?..kwani nchi gani pia inamarais wawili kwa mpigo duniani?
 
SAMUEL SITA AMEJIANDAA KUGOMBEA URAIS WA TZ, SASA NYIE MWASEMA AGOMBEE URAIS WA TANGANYIKA ? mNATAKA KUMPUNGUZIA ULAJI MZEE ??????// TANGANYIKA HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE ?...........................................HOOOOOYEEEEEEEEEEEEEEEEEE, na UHURU................? KAZI YA TANU . TUNATAKA TANGANYIKA YETU.
 

kuungana kwa serikali mbili hakumaanishi ni lazima kuwepo na serikali tatu.
 
Unaposema kuwa hakuna nchi yenye maraisi watatu doniani pia tambua kuwa hakuna nchi yenye marais wawili ila Tanzania. Kama tuna wawili tayari inatushinda nini kuwa na watatu au hata zaidi ukitaka kuongeza na wa Pemba huru?
.
 
CCM wanajaribu kupotosha eti serilkari tatu ni kuongeza gharama, wakati wanahofia kula yao inaelekea kuyeyuka.
Mimi binafsi nataka serikari tatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…