Ndo hiki ambacho na mimi nakiuliza, mawaziri 15 wa Muungano wanashughulikia mambo 7, kwa vipi?....kuwa na mawazir 15 tu watakaokuwa wanashughulikia mambo 7 tu ya muungano
Halafu Kilimo, kwa mfano, sio jambo la Muungano, maji, ufugaji, sio jambo la Muungano, kwa hiyo kukiwa kuna njaa msimuulize Rais, hayamhusu! Kituko.
Mambo ya Nje, kwa mfano, ni jambo la Muungano, Rais ataenda kwenye vikao vya UN, lakini zikianza topic za FAO au UNESCO itabidi Rais atoke nje ya kikao, kwa sababu Kilimo wala sayansi na utamaduni wala watoto (UNESCO) wala afya (WHO) hayamhusu, hatujamtuma! Akienda UN tunataka aingie vikao vya Security Council, UNHCR, wakimbizi, etc. kwa saab wakimbizi na uraia na mipaka inamhusu.
Sasa, wote tunajua tunapokwenda UN mambo ya security council sisi vi nchi vilivyo kwenye ukingo wa dunia huku ni watazamaji tu, kwa saab hatuna hata viwanda vya kutengeza visu, hata wangesema kuanzia sasa tupigane kwa majambia tu, nuclear weapons marufuku bado yasingetuhusu, kwa hiyo kule UN yanayotuhusu sisi ni agenda za kuchimba visima, madawati ya UNESCO, mambo ya vyandarua vyandarua na chanjo za dege dege na electrolytes za utapiamlo. Lakini hayo sio maswala ya Muungano, Rais akienda huko asiyaongelee!
Akidharau hayo mantiki, hayo makubaliano, akaenda UN akaingia vikao vya FAO na UNESCO na WHO basi huku nyuma tunalianzisha tena, amepoka madaraka ambayo hayapo kwenye enumerated powers. Maandamano kwa kwenda mbele, migomo, minong'ng'ono, mabomu, machozi, vitu vyenye ncha kali, tunarudi pale pale, problem unsolved!
In fact the problem is beyond unsolved, it is unsolvable. Huwezi kuwa na nchi ya watu milioni 45 wakaungana na kisiwa cha milioni moja ushee halafu mkataka kubaki na uwiano sawa wa madaraka.