SITTA: Serikali tatu ni kujitafutia ulaji.

SITTA: Serikali tatu ni kujitafutia ulaji.

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2009
Posts
16,508
Reaction score
11,897
Amesema hayo katika mahafali ya wanachuo!Kazungumzia suala la wabunge 2 kila jimbo haliwezikani.Pia ma rais 3 katika nchi moja haiwezekani watanzania wasikubali.Kama kawaida yake huwa hasemi hayo katika vikao rasmi vya serikali,yeye huzungumzia mtaani anapoalikwa.source ITV habari
 
Amesema hayo katika mahafali ya wanachuo!Kazungumzia suala la wabunge 2 kila jimbo haliwezikani.Pia ma rais 3 katika ncho moja haiwezekani watanzania wasikubali.Kama kawaida yake huwa hasemi hayo katika vikao rasmi vya serikali,yeye huzungumzia mtaani anapoalikwa.source ITV habari

Sitta ni Kama Popo si Ndege wala Si Mnyama hivi hajui sasa hivi Tunalisha Marais Watano (5) na Mawaziri zaidi ya 40 (akiwamo yeye)
 
Wazee wengine ngumu hatakueleweka kwa wazee wenzao itakuwa kwa watanzania wote?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Amesema hayo katika mahafali ya wanachuo!Kazungumzia suala la wabunge 2 kila jimbo haliwezikani.Pia ma rais 3 katika ncho moja haiwezekani watanzania wasikubali.Kama kawaida yake huwa hasemi hayo katika vikao rasmi vya serikali,yeye huzungumzia mtaani anapoalikwa.source ITV habari

Hivi huyu Sitta anataka tumpe orodha ya marais wa Tanzania ndiyo aelewe ya kuwa tunao tayari marais watano, Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi(?)

Rais wa JMT - Kikwete
Makamu wa Rais wa JMT - Mohamed Bilal
Rais wa Zanzibar- Ali Shein
Makamu wa Rais wa Zanzibar - Seif Sharif Hamad
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar - Seif Ali Iddi
Waziri Mkuu - Mizengo Pinda
Waziri Kiongozi - (?)

Baraza la Mawaziri limeongezeka na manaibu mawaziri kibao.
Kweli shida anayoiona yeye ni kuwa na marais watatu ama ana lingine?
 
Huyu mzee ni bonge la ----. Hii ni rasimu ya katiba, watu walitoa maoni kwenye tume, na yeye alitoa maoni yake. Sasa rasimu imekuja, mawazo ya wengi ndio yanapelekwa kwenye mabaraza, lakini bado anataka kuifanya anajua kuliko watu waliotoa maoni. Huyu mzee anazeeka vibaya sana, huenda kuanzia 2015 akishakaa benchi baada ya kukosa vyote kwa kutaka vyote atabakia kuwa MCHAWI tu. Huyu mzee ni janga la kidunia, angekuwa mwanamke huenda angeishia kuuza mwili kwa tamaa zake za madaraka
 
Tuheshimu maoni yake, ndiyo maana ya demokrasia. Tumpinge kwa hoja, na si kwa matusi na kejeli.
 
huyu jamaa anatuchanganya, mi nadhani, rasimu imetokana na maoni ya watu wengi, lakini cha kujiuliza kama anasema maraisi watatu kwa maana ya gharama za uendeshaji, mbona tuna utitiri wa viongozi wengi wasiona umuhimu, mfano
  1. makamu wa raisi, wa muungano,
  2. makamu wawili wa raisi wa serikali ya zanzibar
  3. wizara 26
  4. mawaziri na manaibu kama 60
  5. makatibu wakuu na manaibu wao kibao
kwa rasimu hii naona itapunguza gharama sana
alafu imepenekezwa majimbo ya uchaguzi yapunguzwe mpaka 25tu,sioni mantiki ya yeye kupinga anatakiwa ashauri nini kifanyike,

je yeye kama mwanasiasa nguli. mkongwe na mahiri katika siasa za tanzania anao uwezo wa kuwashawishi wazanzibari wakubali serikali moja? ili tuwe nchi moja serikali moja na raisi mmoja??

vinginevyo tunahisi rasimu imeondoa matarajio ya maslahi yake binafsi si ya watanzania
 
Akizungumza kwenye mahafal ya ualimu kibamba, waziri wa E.A Mh. Samwel sitta pamoja na mambo mengine amesema rasimu ya katiba mpya ni mkakati wa kuwatafutia baadhi ya viongoz ulaji, akitolea mfano mfumo wa Serikal tatu, kwamba itakuwa ni kihoja kuwa na marais watatu, na wakat huo huo kuwa na mawazir 15 tu watakaokuwa wanashughulikia mambo 7 tu ya muungano, isitoshe uwe na mawazir wa Tz bara na visiwani, kuwa ni mzigo kwa serikali na wavuja jasho wa nchi hii.
 
Labda angetuambia ni ulaji wa viongozi gani walioko ccm,Serikalini au upinzani.

Au anaota kuwa raisi wa jamhuri ya sasa.?
 
mbona hajapinga ukubwa wa serikali ambayo hata yeye ni mmoja wao,

kuna haja gani yakuwa ana wizara ya afrikA MASHARIKI badala ya kuwepo wizaraya mambo ya nje.

SI NA YEYE ALIPEWA ULAJI, ASIKAE KIJIWENI BAADAYA YA KUNYIMWA USIPIKA

sasa anaka kutuaminisha kwamba hayo ameyaona leo??

kama anauchungu na jasho la wananchi mbona alipinga Chadema walipoitaka serikali ifute posho kwa watumishi wa umma
 
This Sitta man is a frustrated lot. Waliomdanganya wote wamemruka. Wamemfanyia kama alivyomfanyia Mpendazoe. Malipo ni hapa hapa duniani. Habari za ahera ni baadaye.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Anauhuru wa kutoa mawazo yake katika lolote.
 
6 amechanganyikiwa hajitambui kabisa
This Sitta man is a
frustrated lot. Waliomdanganya wote wamemruka. Wamemfanyia kama
alivyomfanyia Mpendazoe. Malipo ni hapa hapa duniani. Habari za ahera ni
baadaye.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Six kaishiwa...aende zake Urambo Mashariki akahangaike kumalizia kajumba kake(mweyewe anaita uwekezaji) pale Ussoke.

Hatuhitaji kusikiliza mawazo ya mtu mpuuzi kama yeye ambaye kwa miaka zaidi ya arobaini amekuwa mbunge wa Urambo jimbo lake halina hata bara bara ya urefu wa kilomita moja ya lami!!!!
 
Ahamie CHAUMMA kwingine kote nafasi zimejaa
 
Mbona hoja yake ni nzuri tu tatizo liko wapi yeye kama Mtanzania ametumia haki yake ya kutoa maoni na kujieleza kutoa yale anayoyaona na sisi tusipoteze nguvu zetu kwa kubeza kishabiki tupinge hoja kwa hoja na siyo hoja kwa kutusi au kukashifu mawazo yake
 
Back
Top Bottom