kwani wabunge wana kinga yoyote kisheria??, au wao wako juu ya sheria??, huyu 6 vipi!.
Hosea alishawambia wabunge siku mmoja kwenye kikao live, kuwa "wanamfuata fuata sana" nayeye atawachunguza wanavyochukua posho mbili mbili za serikali ofisi ya bunge na kwenye mashirika ya umma.
Lakini hii kama alifikiri litamsaidia waogope kumsulubu bungeni , basi amechemcha, Hosea ameingia choo ya kike!!! Ajaribu kupima ufisadi unaoongelewa hapa ni wa Bilions of money, nayeye anaongelea viposho vya vikao havizidi laki 2!!! wapi na wapi!!!!!!!!!!!!
wellsaid Mkuu maana naona watu wengi wanawatetea wabunge hizi si pesa kidogo ati! Ishu hapa ni kua mtu kaenda kinyume na taratibu so haijalishi kama ni hosea au mbunge...vilevile naomba niulize ivi Kinga ya Mbunge ni akiwa bungeni akijadili hoja ua hata Nje ya Bunge bado inaapply?Nilikuwa mtu wa mwanzo humu kulizungumzia hili suala la posho haramu wanazopewa Wabunge na Mawaziri wetu kutoka kwenye taasisi za UMMA. Msidhani ni posho za kawaida ni mamilioni. Jumla yake kwa mwaka ni zaidi ya pesa za EPA mnazopigia kelele humu. Kwa Mawaziri na taasisi na zilizo chini ya wizara zao ni kufuru kabisa.
Hivyo ndivyo unaweza ukaueleza utajiri wa wanasiasa wetu wengi kama akina Prof Kapuya na NSSF yake; Mwandosya na mamlaka za maji mijini; Kawambwa na mameneja wa TANROADS, THA,...;
Hizi "posho" ndizo zimemtoa Sumaye wakati ule na Tume ya JIJI.
"Niliwaambia kuwa kweli nimechukuwa posho hiyo kama takrima na wala si kosa kwani ni taasisi tofauti kama ingekuwa ni ofisi moja hili lingekuwa ni kosa.
Hii issue ya posho kwanini itokee wakati huu wakiwa wanajiandaa kwenda bungeni kwenye mambo ya Richmond?? Huyu Hosea kwanini hajaanza na Mawaziri wanaoongoza kupokea hizi posho mara mbili ya hawa wabunge??
Nimesoma gazeti la Rostam (Mtanzania) akikoleza hii issue kuwa Mwakyembe abanwa, ni Amri kutoka kwa Rais ndo aliyeagiza wachunguzwe!
Huyu RA bila kumrudisha kwao alikozaliwa nchi hii haitakuja kupata amani.
Ameendeshana na Mengi huko huko TAKUKURU, sasa anapitia mgongo wa nyuma kuwaburuza wabunge wanaopokea viposho sababu ni kuisema richmond. Kwanini wasipokee posho hizi kamati zimefanya mambo makubwa kwani serikali ilishakufa kama siyo hizi kamati.
Chukulia kamati inayoongozwa na Slaa, Zitto, Sherukindo, n.k wamefanya magauzi makubwa, sasa hivi wanataka kuwapaka matope!
Hadi hii leo TAKUKURU haijathubutu hata mara moja kumhoji papa fisadi Rostam Aziz katika ufisadi wake chungu nzima alioufanyia nchi yetu pamoja mafisadi wengine akina Idrissa Rashid, Chenge, Mzindakaya na Mkono kwa kuhusika kwao na kuchota mabilioni ya shilingi pale BoT, lakini wamekuwa na speed ya ajabu kuwahoji Wabunge waliodaiwa kuchukua masurufu mara mbili. Hii inaonyesha wazi jinsi TAKUKURU walivyo na priorities zao kinyumenyume.
Elewa hoja hajasema hawawezi kushitakiwa.Amesema lazima ofisi yake itaarifiwe na anayehoji lazima awe ofisa wa ngazi za juu. full stop.Mbona unakuja kishabikkwani wabunge wana kinga yoyote kisheria??, au wao wako juu ya sheria??, huyu 6 vipi!.
Elewa hoja hajasema hawawezi kushitakiwa.Amesema lazima ofisi yake itaarifiwe na anayehoji lazima awe ofisa wa ngazi za juu. full stop.Mbona unakuja kishabik
Usipindishe hoja.Au hujui maana ya priorities? Mchangiaji ( babu) amesema mbona kipaumbele cha PCCB ni kushughulikia pesa za vitumbua na siyo wahujumu uchumi waliyotusababishia umaskini. Hujui tuna hasira na hawa mapapa!!.Hajakataa kwamba walichofanya wabunge si kosa.Tunataka mapapa washughulikiwe kwanza ndo iwe first priorities.Hapa Babu unachanganya mambo:-
1. Ninavyo fahamu mimi Rostam, Idris Rashid, Chenge, Mkono wote wamekwisha hojiwa na Takukuru. I am not sure about Mzindakaya na pia sijui ufisadi wake ni upi?
2. Ninavyoelewa mimi, wabunge wana kinga kwa yale tu wanayoyasema Bungeni kuwa hawawezi kushitakiwa. Hawana kinga nyingine yeyote. Sitta anajaribu ku potray umuhimu usio kuwepo eti kama Mbunge akikosa ahojiwe na ofisa wa ngazi ya juu na ofisi ya Bunge ijulishwe kwanza. Sasa Mbunge kama ni mwizi atasubiriwa IGP ndiye aje kumkamata na yeye Sitta ajulishwe kwanza? Hamna sheria ya namna hiyo nchi. Hapa anataka kutuletea kanuni na kujenga matabaka katika utekelezaji wa haki.
3. Hili sakata la double, triple au quadruplicate allowance payments wala wasilaumiwe Takukuru. Utakumbuka kuwa ni Dk. Mwakyembe huyuhuyu, katika majibishano ya sakata la Dowans, ndiye aliye m-challenge Zitto kuwa kama kweli yeye anauchungu na nchi yake ni vipi anachukua posho Tanesco wakati anapata posho ya Bunge. Hapa ndio kuna ule msemo kuwa mchimba kisima huingia mwenyewe. Mimi sikuamini macho yangu kusoma kuwa Dk. Mwakyembe anaomba kwa maandishi kinga ya Spika asihojiwe. Yeye ni nani? Mbona wabunge wengine walikubali?
4. Suala hili limedhihirisha wazi kuwa hawa wabunge wetu wanaojiita wapiganaji hawana kabisa moral authority. Nilitegemea kutoka kwao kuwa wangelipima jambo hili kama ni haki na sahihi au ni makosa badala ya kujitafutia kinga. Utakumbuka hivi karibuni tu huko Uingereza, wabunge walikuwa wakichukua, KISHERIA, marupurupu ambayo baadaye yalionekana kuwa yalikuwa si haki kuyafanya. Baada ya kubainika hivyo, walilazimika kwa hiari kurudisha malipo hayo japo walikuwa na haki ya kuyadai. Sasa hawa ndugu zetu kwanza wamechukua posho hizi kwa udanganyifu kwa kuwaghilibu walipaji kuwa hawajapata posho hizo, na baadaye wanaleta excuses za hovyo hovyo.
5. Kwa kweli matamshi ya Sitta yanasikitisha sana eti posho hizo ni sawa kama wangepewa chakula na mashirika hayo. Kwanza ni kwanini wapewe chakula na mashirika hayo wakati tayari wamekwisha pewa pesa za chakula na Bunge. Shelukindo naye anasema eti pesa hizo ni takrima. Takrima ya nini, na watawalipa vipi watu walio wakirimu? Kwa kuwa wapole katika kuyachunguza mashirika hayo? Hii si ndi maana ya rushwa?
6. Kwangu mimi huu ni wizi wa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na ni criminal offense. Takukuru iendelee na kazi zake. Kama wao watambana Hosea hilo ni jambo jingine. Lakini nao wabanwe tu.
7. Jee mzee Mapesa amefikia wapi na uchunguzi wa ulaji wa Ofisi ya Bunge? i.e Shs. 70.0m. Sitta lazima awajibishwe kama alivyowajibishwa mweziwe Mongella kwenye Bunge la Afrika.
Usipindishe hoja.Au hujui maana ya priorities? Mchangiaji ( babu) amesema mbona kipaumbele cha PCCB ni kushughulikia pesa za vitumbua na siyo wahujumu uchumi waliyotusababishia umaskini. Hujui tuna hasira na hawa mapapa!!.Hajakataa kwamba walichofanya wabunge si kosa.Tunataka mapapa washughulikiwe kwanza ndo iwe first priorities.