Hadi hii leo TAKUKURU haijathubutu hata mara moja kumhoji papa fisadi Rostam Aziz katika ufisadi wake chungu nzima alioufanyia nchi yetu pamoja mafisadi wengine akina Idrissa Rashid, Chenge, Mzindakaya na Mkono kwa kuhusika kwao na kuchota mabilioni ya shilingi pale BoT, lakini wamekuwa na speed ya ajabu kuwahoji Wabunge waliodaiwa kuchukua masurufu mara mbili. Hii inaonyesha wazi jinsi TAKUKURU walivyo na priorities zao kinyumenyume.
Hapa Babu unachanganya mambo:-
1. Ninavyo fahamu mimi Rostam, Idris Rashid, Chenge, Mkono wote wamekwisha hojiwa na Takukuru. I am not sure about Mzindakaya na pia sijui ufisadi wake ni upi?
2. Ninavyoelewa mimi, wabunge wana kinga kwa yale tu wanayoyasema Bungeni kuwa hawawezi kushitakiwa. Hawana kinga nyingine yeyote. Sitta anajaribu ku potray umuhimu usio kuwepo eti kama Mbunge akikosa ahojiwe na ofisa wa ngazi ya juu na ofisi ya Bunge ijulishwe kwanza. Sasa Mbunge kama ni mwizi atasubiriwa IGP ndiye aje kumkamata na yeye Sitta ajulishwe kwanza? Hamna sheria ya namna hiyo nchi. Hapa anataka kutuletea kanuni na kujenga matabaka katika utekelezaji wa haki.
3. Hili sakata la double, triple au quadruplicate allowance payments wala wasilaumiwe Takukuru. Utakumbuka kuwa ni Dk. Mwakyembe huyuhuyu, katika majibishano ya sakata la Dowans, ndiye aliye m-challenge Zitto kuwa kama kweli yeye anauchungu na nchi yake ni vipi anachukua posho Tanesco wakati anapata posho ya Bunge. Hapa ndio kuna ule msemo kuwa mchimba kisima huingia mwenyewe. Mimi sikuamini macho yangu kusoma kuwa Dk. Mwakyembe anaomba kwa maandishi kinga ya Spika asihojiwe. Yeye ni nani? Mbona wabunge wengine walikubali?
4. Suala hili limedhihirisha wazi kuwa hawa wabunge wetu wanaojiita wapiganaji hawana kabisa moral authority. Nilitegemea kutoka kwao kuwa wangelipima jambo hili kama ni haki na sahihi au ni makosa badala ya kujitafutia kinga. Utakumbuka hivi karibuni tu huko Uingereza, wabunge walikuwa wakichukua,
KISHERIA, marupurupu ambayo baadaye yalionekana kuwa yalikuwa si haki kuyafanya. Baada ya kubainika hivyo, walilazimika kwa hiari kurudisha malipo hayo
japo walikuwa na haki ya kuyadai. Sasa hawa ndugu zetu kwanza wamechukua posho hizi kwa udanganyifu kwa kuwaghilibu walipaji kuwa hawajapata posho hizo, na baadaye wanaleta excuses za hovyo hovyo.
5. Kwa kweli matamshi ya Sitta yanasikitisha sana eti posho hizo ni sawa kama wangepewa chakula na mashirika hayo. Kwanza ni kwanini wapewe chakula na mashirika hayo wakati tayari wamekwisha pewa pesa za chakula na Bunge. Shelukindo naye anasema eti pesa hizo ni takrima. Takrima ya nini, na watawalipa vipi watu walio wakirimu? Kwa kuwa wapole katika kuyachunguza mashirika hayo? Hii si ndi maana ya rushwa?
6. Kwangu mimi huu ni wizi wa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na ni criminal offense. Takukuru iendelee na kazi zake. Kama wao watambana Hosea hilo ni jambo jingine. Lakini nao wabanwe tu.
7. Jee mzee Mapesa amefikia wapi na uchunguzi wa ulaji wa Ofisi ya Bunge? i.e Shs. 70.0m. Sitta lazima awajibishwe kama alivyowajibishwa mweziwe Mongella kwenye Bunge la Afrika.