Sitti Mtemvu aibukia Amana Hospital Ilala

Sitti Mtemvu aibukia Amana Hospital Ilala

IPECACUANHA

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2011
Posts
3,226
Reaction score
1,919
Sitti Mtevu ametoa msaada wa vyombo vya kuhifadhia uchafu kwa hospitali ya Ilala kupitia Sitti Foundation. Vifaa hivyo vilipokelewa na mbunge wa Ilala Zungu. Swali hivi kweli watu wanakosa kumbukumbu au Aibu? Hivi kweli media na taasisi zina habarisha kitendo ambacho ni kizuri kutoka kwa mtu "tapeli" aliyegushi cheti cha kuzaliwa? Kwa jamii makini hili haliwezi kutokea kwani ni tendo la aibu kutokea kwenye hadhara kukaa meza kuu katika mazingira haya..wakuu hii imekaaje?
 
So kakosea kutoa hivyo vyombo kama msaada kwa sababu aligushi vyeti ama??
 
So kakosea kutoa hivyo vyombo kama msaada kwa sababu aligushi vyeti ama??
Ni muhimu na wajibu kuangalia unapokea kitu kutoka kwa nani. Huwezi kupokea msaada kutoka kwa mwizi kwa mfano kwakua ulichopewa kitahusishwa na wizi. Kilichofanyika ni kumpromote mtu mwenye tabia mbaya na hiki kinachangia mmomonyoko wa maadili katika jamii.
 
Ule umiss ilikuwa dili kubwa kwa hii foundation, wamenyang'anywa tonge mdomoni.
 
Sitti Mtevu ametoa msaada wa vyombo vya kuhifadhia uchafu kwa hospitali ya Ilala kupitia Sitti Foundation. Vifaa hivyo vilipokelewa na mbunge wa Ilala Zungu. Swali hivi kweli watu wanakosa kumbukumbu au Aibu? Hivi kweli media na taasisi zina habarisha kitendo ambacho ni kizuri kutoka kwa mtu "tapeli" aliyegushi cheti cha kuzaliwa? Kwa jamii makini hili haliwezi kutokea kwani ni tendo la aibu kutokea kwenye hadhara kukaa meza kuu katika mazingira haya..wakuu hii imekaaje?

Hakuna binadamu alie kamilika,yeye amegushi cheti na waloiba mapesa tele mbona wanatembea kwa raha zao? na as long as amefanya jambo zuri kama hilo Mungu amzidishie na amuepushie mahasidi na midomo ya watu........
 
Nyie mnsojiita wasafi mbona hamtoi??? Mimi naamini kwenye usemi huu, hakuna watu wasafi hapa, kuna ambao hawajashikwa na walioshikwa.
 
Back
Top Bottom