Sitti Mtemvu ajivua taji la Miss Tanzania

a/c yenyewe ya facebook imanzishwa 17/10/2014
 
Dah...Mkuu umeongea kwa uchungu sana na inaoneka una hasira sana na Lundenga na Kamati yake...

Kwa nini utumie nguvu kubwa hivo kumvua taji binti Mtemvu?...

Binafsi sioni faida yoyote ya mashindani ya aina ya Miss Tanzania au Big Brother kwa nchi...Mashindano haya hayana faida yoyote kwa nchi zaidi ya mtu binafsi i. e Lundenga, Sitti na wewe(maelezo yako kwenye post nyingi yananifanya nihisi kama una maslahi binafsi na mashindano haya, ama ulikuwa mmojawapo wa washiriki ama una mahusiano ya karibu na mmojawapo wa washiriki ambao unahisi alikuwa na sifa za kushinda)...

Bado sijaona umuhimu wa mashindano haya kiasi cha kuyashikia bango kwamba ushindi wa Sitti unailetea sifa mbaya Tanzania kama nchi..Ni sifa mbaya kwa Lundenga na timu/Kamati yake...
 
Kujivua taji sawa na je zawadi alizopata atazirejesha?
 
Hata mimi nina wasiwasi huo Dr.........hawezi kuvua kirahisi hivyo.......kama kweli itakuwa burudani.........
Bora tumpe dada yetu Miss no,2 kutoka uchagani kwakua alikua anastahili!
 
Akitaka kuvua taji atawaandikia lino agency siyo fbook acheni kupoteza muda na uzushi wa knye kahawa
 
Hii ni aibu kwa Lundenga. Hii inatoa picha ya kwamba kuna udanganyifu wa muda mrefu sasa arobaini imefika.
 
Hii ni aibu kwa Lundenga. Hii inatoa picha ya kwamba kuna udanganyifu wa muda mrefu sasa arobaini imefika.

Na huu udanganyifu upo kwenye kila sekta muhimu ya nchi hii.

Maana kama mtu ana nyaraka zinazotolewa na serikali lakini zenye taarifa tofauti, hapo lazima kuna ujanja ujanja uliofanyika.

Haiwezekani mtu awe na pasi ya kusafiria ambayo inatolewa na serikali yenye tarehe tofauti na iliyopo kwenye cheti (kipya) cha kuzaliwa ambacho nacho hutolewa na serikali.

Hiyo pasi ya kusafiria aliipata pataje? Ni nyaraka gani alizotumia kuipata?

Hili si suala la kupuuzia hata kidogo hata kama hayo mashindano hayana tija sana kitaifa.

Kama kuna udanganyifu unaofanyika kwenye taasisi za kiserikali basi hapo maslahi ya taifa yapo.

Mpaka sasa hakuna maelezo ya kuridhisha juu ya utofauti wa taarifa uliopo kwenye hizo nyaraka (ambazo hutolewa na serikali).

Halafu watu wanataka watu tupuuzie tu bila hata maelezo ya kutosha na kuridhisha?

Nashindwa kuelewa jinsi akili za baadhi ya watu ambavyo hufanya kazi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…