Situation ya wanafunzi waliokuwa wanapandisha majini shuleni imekaaje?

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Nimezaliwa wazazi bado hawajajipata kwa hiyo ilibidi nisome shule za serikali primary
Pia nimekulia mkoa wa Lindi sehemu yenye waislamu wengi kwa hiyo marafiki zangu wengi walikuwa waislamu na nilikuwa napenda kuwauliza story za majini maana wao ndio walikuwa wanazijua kiundani

Sasa shuleni kwetu kulikuwa kuna wanafunzi kadhaa wanaopandisha majini na wote walikuwa wa kike. Kuna mmoja alikuwa darasa la juu alikuwa anaitwa Amina, alikuwa akipandisha majini hadi walimu wakijaribu kumzuia wanashindwa kumstopisha, yani alikuwa akianza kuchacharuka ananyanyua hadi ile meza ya walimu anaipigiza chini na uzito wake
Kuna mwingine darasani kwetu nae alikuwepo mmoja, wa kike pia alikuwa anapandisha majini, hatulii hadi aitwe Sheikh amuombee Kiarabu pale ndo anatulia
Honestly kipindi hicho nilikuwa ninaamini uchawi upo. Na case zote mbili za watu wanaopandisha majini kila mmoja alimtaja aliyemroga, na baada ya kukataa sana walioshitumiwa kuwa wamemroga, mfano aliyeambiwa amemroga demu wa darasani kwetu alikuwa ni mwanafunzi mwenzake wa kike na alikiri kuwa ni kweli amemroga, yeye ndio anahusika

Lakini sekondari wazazi walinipeleka shule ya private, miaka yote minne sikuwahi kuona mwanafunzi akipandisha majini. Advance pia, the same case, sikuona anayepandisha majini hadi naingia chuo nako ni hivyohivyo

It makes me wonder. Wale watu waliokuwa wanapandisha majini na kuleta vurugu kipindi cha primary walikuwa na matatizo gani

1. Je, walikuwa na matatizo ya akili? Kama ni matatizo ya akili, ni matatizo gani ambayo yanaweza kupelekea hali hiyo? Yana jina lolote kisayansi?

2. Au ni kweli uchawi upo? Kitu ambacho hakiingii akilini btw

3. Au walikuwa wanaigiza? Na kama walikuwa wanaigiza basi wana kipaji sana. Ile ni talent maana it almost looks real

4. Assume kweli wanaigiza, sasa nguvu wanazitoleaga wapi. Kama huyo aliyekuwa ananyanyua meza nzito tu, huwa ametoa wapi nguvu zote hizi kwa umri mdogo?

5. Wale wanafunzi wanaokiri kweli wamehusika kuwaroga wenzao, kwa nini wanakubali kukiri? Ni kwamba wanakuwa wamelazimishwa na watu wazima wakubali au wanakuwa wanasema ukweli? Na kama wamelazimishwa kwa nini watu wazima wawalazimishe watoto kukiri mambo ya kudhalilisha kama hayo?

Swali langu lingine, kwa nini ni familia masikini ndio zinakumbwa zaidi na haya matatizo? Sijawahi kusikia mtoto wa tajiri amepandisha majini

Na kwa nini wanafunzi wa hivi wapo zaidi shule za serikali badala ya private? Miaka 6 ya kusoma private sijawahi kuona mtu anapandisha majini. In fact toka namaliza primary hadi leo sijawahi tena kukutana na case ya mtu kupandisha majini
Lakini tukiwa chuo, watu waliosoma shule za serikali wanasimulia kuwa walikuwepo watu wanaopandisha majini shuleni kwao

Seriously though, kuna mtu yoyote anayeelewa what exactly is going on kwenye situation kama hii. Maana leo nimekaa nikakumbuka the way primary kulivyokuwa na watu hao na nabaki kujiuliza hadi sasahivi, why did that even happen and if there's a way to explain it in a way that makes sense
 
Nakumbuka enzi hizo nasoma sekondari mkuu wetu ilikuwa mtu akipandisha anaomba wamletee nje pale assemble then anaanza kuwalisha mboko mbona kesi ziliisha 🙌😂
 
It might be kwamba wanaigiza. Ila kama wanaigiza basi kuna wanafunzi wana vipaji sana
 
Hawakuwa na matatizo ya akili bali walikuwa kwenye mazingira yaliyoruhusu wapatwe na mambo hayo kwani ulozi upo ila sio kila mtu anaweza kulogwa. inategemea mazingira, imani na ufahamu wa mtu.
2. Au ni kweli uchawi upo? Kitu ambacho hakiingii akilini btw
Hakika uchawi upo.
3. Au walikuwa wanaigiza? Na kama walikuwa wanaigiza basi wana kipaji sana. Ile ni talent maana it almost looks real
Hawakuwa wanaigiza na jambo halisi liliwakumba kutokana na mazingira na hali zao kiimani na kisaikolojia.
4. Assume kweli wanaigiza, sasa nguvu wanazitoleaga wapi. Kama huyo aliyekuwa ananyanyua meza nzito tu, huwa ametoa wapi nguvu zote hizi kwa umri mdogo?
Hawakuwa wanaigiza. Walipata nguvu kutoka kwenye roho zilizofanya kazi ndani yao kwa namna ya ajabu.
Walikiri kuhusika kwasababu kweli walihusika. Wapo wanafunzi wengi tu ni wachawi kwa kujua na kutokujua pia.
Swali langu lingine, kwa nini ni familia masikini ndio zinakumbwa zaidi na haya matatizo? Sijawahi kusikia mtoto wa tajiri amepandisha majini
Uchawi wa kijinga upo zaidi kwenye familia na jamii maskini. Sio kwamba jamii tajiri hawana uchawi, upo ila wanatumia kwenye mambo makubwa zaidi na sio kuwaangusha watu.
Umiliki ni kitu chenye nguvu sana! Himaya yako inafanywa na umiliki wako na ndio maana si kila nyumba wachawi wanaweza kufanya mambo yao. Shule za serikali ni kama hazina umiliki binafsi na zinakosa ulinzi wa kiroho na hugeuka shamba la bibi kwa wachawi hadi mtu aamue kumiliki na kuzuia mambo ya hovyo.
Kwa ujumla uchawi hufanya kazi na kusitawi vizuri pale penye ujinga, imani potofu na hofu. Ukiondoa mambo hayo basi uchawi wa kijingajinga huishiwa nguvu.
 
unafundishia mkoa gani mkuu?
 
Majini haya kuwepo ulikuwa ni namna ya kutaka kupelekewa moto kwa hao mademu walio kuwa wanapevuka. It was so insane
 
Duh......
 
Hiyo shule itakua tabora, kigoma, rukwa..
 
kutokana na mazingira na hali zao kiimani na kisaikolojia.
Kuna mstari mwembamba Sana Kati ya urozi Na saikolojia, wachawi wengi akitaka akuroge Kwa urahisi anacheza kwanza Na akili yako, Kile usichoamini kukupata hakiwezi kukupata,
 
PNES(Psychogenic Non-epileptic Seizures) inawapata zaidi mabinti wa balehe. Wanaonesha dalili za degedege bila ugonjwa wowote ule wa kiufahamu.

Vyanzo ni changamoto mbalimbali za kiakili zikiwemo sonona, kiwewe na wasiwasi. Yawezekana binti anapitia matatizo kifamilia, kitaaluma na hata kwenye marika yake, mfano anafeli shuleni na wazazi wanamhukumu sana...

Kuigiza kupo pia kwa sababu mbalimbali.

Mtoto kusema kamloga mwenzie ni uongo, mtoto huyo anatafuta sifa/kuonekana. Binadamu tunajifunza mapema sana kuwa tukifanya vitu vya ajabu tunapewa sifa. Na pia umri wa balehe ni muda ambao watu hutafuta sana kuonekana ili wajihisi ni muhimu.
 
Alaumiwe aliyemuumba ABDALLAH KICHWA WAZI!
Wasichana na wanawake wakimkosa huyo NI SHIDA!
 
Sema huwa napata shida kuamini kama uchawi upo. Cause it doesn't make sense how all this idea of witchcraft works
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…