Situation ya wanafunzi waliokuwa wanapandisha majini shuleni imekaaje?

Madarasa Yote niliyo soma, Hatukua na hyo shida. Ila kuna sehemu niliona demu ana mapepo it was so bad.

Na kuhusu kuigiza ni hell no. Maana unakuta ghafla mtu amekua na nguvu x 3 ya anayo kua nayo siku zoote

Yaani how comes, bint mdogo tu ku mtukiza ni watu wa3 na makamba
 
"Psychogenic illnesses"(matatizo ya kimwili yanayosababishwa kisaikolojia) kama hizi zinaweza kuambukizwa na kupelekea kundi kubwa kuathirika.

Mwaka 62' ulitokea mlipuko wa wanafunzi kucheka kuliko kawaida kanda ya ziwa. Ulisababisha shule 14 kufungwa, na watu zaidi ya 1,000 kuathirika.

Mwaka 63' ulitokea mlipuko wa kukimbia hovyo Uganda ambapo watu walikuwa wakikimbia na kupiga kelele hovyo huku wakiharibu mali za watu.

Sayansi yake ni ngumu kuielewa, imekaa kibobezi sana ila kimsingi anaanza mgonjwa mmoja(index patient), halafu wengine wakiona, wanamuonea huruma, wanaingiwa na hofu ya kuhisi wataathirika(nocebo effect) kisha nao wanaanza kuonesha dalili hizo(haya yote yanatokea kwenye ufahamu wa ndani kabisa usiodhibitika kirahisi).
 
Kuna tafiti ya kizungu inaonesha kuwa masikini wana uwezekano wa mara mbili hadi tatu zaidi ya matajiri, wa kupata matatizo ya kiakili.

Pengine ndio maana mambo haya yapo zaidi kwenye shule za serikali. Binafsi nimeona private yapo, ila sio kama serikalini.
 
Waliosoma IST,Feza etc watuambie kama huko kuna hivi visanga vya majini.

Hivi vimbwanga ni vifungashio vya St.Likud pekee.😁
 
Mbona hii ni tofauti sana na cases za kupandisha majini mkuu. Hii unayoongelea inaonekana ni ya kuambukiza, ndio maana umeataja outbreak zilizotokea
Kupandisha majini shuleni inakuwa ni watu specific ndio wanasumbuliwa na matatizo hayo bila kusambaza kwa wengine. Na wengine wanataja maneno ya ajabu mara sijui "Nimetumwa na mtu fulani blah blah blah"
Nimesearch Psychogenic illnesses nimeona ni tofauti kabisa na wanaopandisha majini kwenye shule zetu za Kibongo
 
Sio lazima isambae kwa maelfu ya watu, hata kikundi kidogo tu cha watu kadhaa pia.

Hata huko kuropoka maneno ya ajabu ni dalili.

Ninaweza kwenda mbali zaidi na kusema, kushikwa na majini/mapepo ni mtazamo wa kidini tu wa hili tatizo. Huwezi kukuta mtu kashikwa na mapepo anaongea kistaarabu akiwa ametulia.

Ni pale tu ambapo mtu anapoteza utimamu na kuanza kufanya mambo ya ajabu ndipo tunasema ana mapepo.

Soma kitabu kinaitwa "It's all in your head" cha Suzanne O'Sullivan. Huyu mtaalamu ndo ameeleza kiuandani kabisa.
 
Mazingaumbwe tu!
 
Waliosoma IST,Feza etc watuambie kama huko kuna hivi visanga vya majini.

Hivi vimbwanga ni vifungashio vya St.Likud pekee.😁
Hawana na hakuna ujinga na upumbavu kama huo!
Uvivu wa watoto, hawataki soma na nyege tu!
 
Halafu why hayo majini huwa ni kwa wasichana tuu shuleni au wanakua na yao...
Hata shuleni kwetu alikuwepo mmoja kuna siku aliwashwa kiboko kimoja tuu yakayeyuka...
Balekhe hiyo ,kipind hicho wanawake wanataka kila kitu ..Yaani wanajiona wanajua kila kitu ,unakuta katoka kwao huko maisha magumu .

Wengine ,hawapendi kuchapwa so wanajifanya wana mashetani au kuzimia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…