Siungi mkono JWTZ kwenda kupigana na Rwanda au M23

Siungi mkono JWTZ kwenda kupigana na Rwanda au M23

NCHI lazima ina uwezo kulinda maslahi yake kidiplomasia na ikibidi kijeshi pia!

Tumefanya investment kubwa sana kwenye ziwa Tanganyika kuyalenga masoko ya Congo! Tunaachaje soko liharibiwe tu!
 
Hii vita Ina siri nyingi sana kuliko tunachokiona, Kuna uwezekano hao askari wa SADC na wakubwa wa hizo nchi za SADC walikuwa na biashara inayoendelea huko DRC nje ya ulinzi wa amani.
 
Nyie Bando la wiki ni my bro, mjeshi naona anajihami kwanza 😅😅😅😅😅 kaka kazi ya jeshi ni kugangamala, hakuna namna. Halafu hii nchi ni tajiri huoni viongozi, wanavyoelewa kwenye bahari ya utajiri? Umasikini uko kwa wananchi wa kawaida, hasa wasio na vyeo Serikalini wala mamlaka zozote. Nenda vitani kaka 😜
 
Hakuna atakayekuwa salama ikiwa mmoja wetu hayupo salama wewe.
Kuna EAC kuna SADC mapinduzi yoyote yanayoenda kinyune na utaratibu wa kikatiba ni haramu.
JWTZ haitaingia kwa jitihada zake pekee, bali kama mwanachama wa EAC au SADC.
Hao M23 wakimaliza DRC wataenda Burundi na wakipata nguvu zaidi watakuja hapa 😅
waje kufanya nini? hayo ni mawazo yasiyo na maana na ya kichochezi! vita siyo nzuri na hatutaki na wala haituhusu kabisa
 
Kuna watanzania wamepanic kuhusu M23 kuchukua eneo la Goma DRC na kauli ya Paul Kagame wa Rwanda.
Ndugu zangu vita sio jambo la mchezo wala la kuliomba. Lakini pia tukumbuke hakuna nchi ndogo kwenye uwanja wa vita.
Wote tumeshuhudia namna Israel taifa dogo kijeografia lakini ilivyo wapelekea moto mataifa makubwa kama Yemen, Lebanon, iran na Syria.

Kuendesha vita ni gharama kubwa ndugu zangu, embu fikiria nchi kama Russia yenye uchumi mkubwa wa karibia trilioni 3 USD na Ukraine yenye uchumi mkubwa karibia dola Billion 200 Leo mwaka wa nne wanapigana lakini kila siku Ukraine anapita huko kwenye mataifa makubwa kuomba msaada.

Sasa nchi yetu maskini yenye uchumi dhoofu chini ya dola bilioni 78 tunataka kuingia kwenye vita visivyo husu mipaka yetu moja kwa moja. Nchi maskini ambayo bado inaangaika kujenga vyoo na madawati mashuleni ikaingia tena kwenye vita. Nchi yetu bado inaugulia vita vya Kagera vya mwaka 1978 ambavyo viliondoka na hazina na vijana wetu wengi waliouwawa kwenye vita hiyo. Bara hata vita ya Kagera tulikuwa tunapigania mpaka wetu kule kagera.

Vita ya DRC na Rwanda (M23) haituhusu moja kwa moja kwa sababu hakuna eneo letu linagombewa kwenye vita hiyo.

Kuhusu biashara yetu kupita hapo Goma kuelekea DRC, ni suala la kufanya mazungumzo ili mizigo ya wateja wetu ipite salama eneo hilo.
Nasisitiza tu serikali iongeze ngome za kisasa za jeshi mipakani hasa mipaka ya Rwanda na Burundi ili hao waasi wasiingie kirahisi ndani ya mipaka ya JMT.
Kwa nini JWTZ iende kupigana na Rwanda au M23?
Ikapigane kwa sababu gani hasa na kwa maslahi ya nani?
 
Back
Top Bottom