Siungi mkono kurudia usahihishaji matokeo kidato cha nne

daah,,,jamani tuwe waelewa,,hawasahishi karatasi bali wanarudia upangaji wa grade ambao huwa unatumika mashuleni sio ule ambao necta wametumia kwenye mtihani huo bila taarifa,,,,,tuwe waelewa,,,,
Wengi wao walipa ziro kama itatumika grade ya zamani wengi watapata div 4 kwa ku assume wote waziro walikuwa na wastani wa marks 35 ambayo itakuwa D kwa sasa je ndio dhumuni la watahiniwa?
 
Mimi siungi mkono kusahihisha upya mtihani uliokwisha sahihishwa.Ushauri wangu wangetoa mtihani mwingine na kuwapatatia wanafunzi waliofeli ili kuona kama kweli hawakuwa vizuri kiakili.KInachofanyika sasa ni Siasa kwenye elimu
 
Achen kupotosha... Hakuna mtihan utakosahihishwa upya bali kuna upangaji mpya wa alama za ufahulu ambao hauchukui muda na almost ni kama mwezi mmoja tu.
kama ni hivyo,hiyo ni kazi ya masaa machache tu,ni kuweka comment mpya tu kwenye software na matokeo yanabadilika
 
Mkuu naona ww bado unasomeshwa hujui uchungu wakumsomesha mtoto na akafeli, wazee wenzangu watakuelimisha zaidi. Hapo kwenye red, inaonyesha kiwango cha upopompo wako.

Ukweli utabaki palepale.Elimu bora na yenye tija haiwezi patikana kwa mambo yanayofanya kwa sasa,kusahisha upya sio suluhisho kwa matokeo mabovu,wadau mtu kaandika mfano 2+1=21,yani hapo hata waitwe kina nani waje kusahihisha matokeo yatabaki yale yale tu
 
Hapo inatafutwa haki halali ya mtu na sio vinginevyo.Mitihani haisahihishwi upya ila alama alizopata mtu zinawekwa ktk madaraja yaliyotumika ktk kuwaandaa wanafunzi.Mitihani ya shule na mock watoto walipimwa kwa viwango vya ufaulu vinavyojulikana lkn mtihani wa taifa viwango vikapandishwa zaidi.HAKI ITENDEKE
 

Je unadhani ukitumika huo utaratibu matokeo yatakuwa mazuri? Maana ziro zilkuwa nyingi ambapo walitumia 35 kama F sasa hiyo itskuwa kama D huoni bado watapunguza ziro kdg na kwenda four?
 
Mkuu naona ww bado unasomeshwa hujui uchungu wakumsomesha mtoto na akafeli, wazee wenzangu watakuelimisha zaidi. Hapo kwenye red, inaonyesha kiwango cha upopompo wako.

hata kama ukiwa na uchungu wa kusomesha ndo mwanao afeli na kustandadize kwa nia ya kuondoa aibu ya taifa then mtakapopata hasara nyingine ya kuwalipia five na six mnatarajia watawaletea matokeo gani angali msingi ni mbovu? Yani nafananisha kuanza kujenga nyumba kwa msingi wa nyumba ya udongo then ukifika level ya lenta unajemgea tofali sidhani kama wewe mwenyewe utathubutu kuingia ktk hiyo nyumba
 
Kama kuna watahiniwa waliomba kurudia kusahihishiwa mitihani baada ya kulipa ada, na wakafeli zaidi. Leo hii wakionekana wamefaulu, je usahihishaji si usanii dhahiri. Na je wale waliojinyonga watafidiwaje?
 
usahihishaji,umechangia vipi kufeli?naomba alosikiliza riporti anijuze

Nilisikliza ila nilishtushwa na nilichokuwa nasikia. Wanasema hawakufanya standardisation ndo maana wamefeli. Mimi sijui sana hesabu ila sijui kama hili litawezaje kuinua kiwango cha ufaulu. Only in TZ.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Nikwambie tu na mitusi yako haionyeshi unanitukana inaonyesha ni kiasi gani ziro haikwepeki kwako!! Unaogopa kurudia mtihani sababu utakosa wa kumpa lawama!!
 
Je unadhani ukitumika huo utaratibu matokeo yatakuwa mazuri? Maana ziro zilkuwa nyingi ambapo walitumia 35 kama F sasa hiyo itskuwa kama D huoni bado watapunguza ziro kdg na kwenda four?

Mkuu, hapo haingaliwi nani atafaulu na kwa kiwango gani.Nia sio kupunguza ziro na kufurahisha wananchi.Lengo la kupanga viwango vya ufaulu kwa kuzingatia maandalizi ni muhimu sana.Kama mtu alistahili ziro basi aipate baada ya kuhukumiwa kwa haki na sio kwa kuviziwa bila kujua.
 
Mtihani hausahihishwi upya bali NECTA wameagizwa kugrade marks za wanafunzi upya kwa kufuata viwango vilivyotumiwa 2011 na miaka ya nyuma. Imeonekana kuwa mwaka 2012 walitumia viwango vipya ambavyo wamebadili wenyewe bila kushirikisha wadau wengine wa elimu. Mfano F katika somo hutolewa kwa alama 0 hadi 20. Wao walibadilisha na kufanya iwe 0 hadi 34 bila kuwashirikisha wadau wengine wa elimu.
 
usiombe kupata alama usizotarajia kwa mfano kuna watu walokuwa na juhudi na katika masomo yao ya mtihan wa mock wamepata dv 2 au 1.Ila necta wamepata four za 26 up tu 29.kuna huwiano wowote hapo??UNGA MKONO WEWE

What is mtihani wa mock? Kama mtihani wa mock ni kitu, kwanini tuwasumbue watoto kufanya mtihani wa taifa? Acheni serikali yenu icheze na akili za watoto wenu ili baadae watoto wenu watawaliwe vizuri. Kama hizo shule ni kitu, kwanini viongozi aw serikali wao hawawasomeshi watoto katika shule hizo?!
 

Lakini trend ya kufeli imeonyesha mwaka 2012 ilikuwa wafeli kuliko 2011. Kilichofanyika hapo serikali inataka kuonyesha kuwa 2012 wanafunzi walifaulu kuliko 2011. Swali, serikali imefanya juhudi gani kubadili hiyo trend ya kufeli tangu ilipoanza kuonekana? Tusiwe wajinga kukubali kila tunapodanganywa na viongozi dhaifu na waongo kama hawa!
 
Mi naona wangeacha tu maana wanavozidi kupanga kurudia upangaji wa grade upya ndo wanavozidi kutucheleweshea matokeo yetu ya A_level.
 
Necta walitoa tamko hawakutumia grade mpya ni oungo wao walitumia grade za zamadi huu ni mchezo wa magamba mafisadi kukwepa lawama na kurudisha lawama necta. Hapa tusubirie tamka la necta. Kwa tetesi ile tume ya pindi ripoti haikutoa maoni ya kuweka grade za zamani ila ripoti imechakachuliwa ile wajiondoe lawamani. Tuwe makini huu mchezo tunachezewa na wanasiasa ktk elimu yetu. Ukweli wanafunzi walifeli na hawataki kusoma sasa serikali inapokuja kuwapa tena kiburi hata wakifeli inawaonea huruma hawa walio mashuleni hasa shule za kata hawatasoma kabisa na ujumbe kwa walimu hii ni kuwadharau.
 
Jamani kinachofanyika sio kusahihisha upya hapana!!....kinachofanyika ni upangaji mpya wa "grades" za ufaulu!

Kutokana na utafiti uliofanyika,iligundulika kwamba NECTA walipandisha grades kimyakimya,hivyo basi watahiniwa walipandishiwa grades badala ya alama A kua 81,mwaka wao A ilikua 85 hali hii ilipelekea wengi wao kufeli!...

So kinachofanyika ni upangaji mpya wa hizo grades na kuzirudisha kwenye mfumo wa awali uliokuepo yaan alama A iwe ileile 81 iliyozoeleka!!

Mm binafsi napongeza uamuzi huu lakin pia naomba NECTA ichukuliwe hatua za kinidham kwa kufanya uhuni huu wa kupandisha grades bila kuwashirikisha wadau wa elim ambao ni walim,wanafunz na wazazi!!
 

nyie ndo mliochora mazombie na kuandika matusi kwenye pepa!hata wakipanga upya grades bado utalamba zero tu ww kijana prof wa matusi tanzania!
 
Ntonga nakushangaa sana....kama wangesema wanafuta masifuri na kuwapa alama nzuri ningekubaliana na wewe....lakini kurudia kusahihisha mtihani kwa kuzingatia mtaala ulivyotekelezwa? Je kama wewe ungekuwa unasoma chuo kikuu na mwalimu akakuonea kwa kukufelisha...je 'hutakata rufaa" kukata 'rufaa' au 'appel kwa kimombo ni njia pekee inayompa mtu haki yake kama alisahihishiwa kibatili...kwa kuonewa.
Kwa hiyo kurudia kusahihisha mitihani ni safi sana....naunga mkono hoja.
Wakisahihishiwa kwa haki...watakaofeli ni wale ambao kweli walistahili kufeli...lakini walioonewa watavuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…