Siungi mkono kurudia usahihishaji matokeo kidato cha nne

Mie naona WANAFUNZI WOTE WA 2012 WANGEFANYA MITIHANI MINGINE UPYA.
Na kama kweli Necta walibadili grade za ufaulu bila wadau kufahamu ni WAPUUZI ona imeshagharimu maisha ya watu, na hata uchumi wa nchi.
 

Mkuu unaposema lengo ni kupanga matokeo kuzingatia ufaulu unamaanisha nini hujui kuwa kweli elimu matokeo hayapangwi bali mtu binafsi anayatafuta hata kwenye mpira ni kosa kubwa kupanga matokeo, hali halisi maandalizi kwa vijana wetu ni mbaya kutokana na mfumo mmbovu wa elimu nchi ambayo haina mitaala, hata kama ni standarzation lazima uangalie uwiano wa ufaulu ila kwa sasa kuna gap kubwa sana kati ya shule za serikali zenye watu wengi na binafsi, primary walifanya hivyo tukaona na wasiojua kusoma na kuandika wakifaulu ni vyema tukajifunza kusolve matatizo kwa njia sahihi sio shortcuts pia usiwe mwepesi wa kudanganyika kuwa hiyo standarzation haikufanyika awali sema tu hali ilikuwa mbaya sn wengi hawakujaza kitu halafu tume imeeleza mengi sana mbona hawakuzingatia tunapumbazwa ndugu hali ni mbaya kwenye elimu yetu
 
ni kweli kabisa mzee ila hawarudii kusahosha ila wanataka kucheza na madaraja na mambo mengine watoto wafaulu. hili jambo wanalifanya kisiasa eti wanasema necta ilifanya makosa kuanzisha utaratibu mpya bila kuhusisha wadau. lakini ukizingatia necta ni baraza kubwa na linaongozwa na kanuni na sheria husika za nchi sio rahisi kufanya mistake ndogo kiasi hicho ila hiyo ni njia ya kudanganya watanzania kujipatia umaarufu wa kisiasa
kama necta walifanya kinyume na sheria mbona hakuna yeyote kushtakiwa. ndugu zangu najua mtanichukia kwa kusema hivyo kwa sababu mna ndugu na watoto wenu mnapenda wafaulu; hata mimi ninao pia. ila huku sio kufaulu watanzania ni kudanganywa ni sawa na kumwambia mtoto anayelia "nyamaza ntakununulia ndege". sababu ya kufeli sio necta ila ni mazingira magumu na yasiyo na matumaini kwa watoto wetu... tuwaombea wabunge wetu wapiganie hilo na sio kufahulisha watu waliofeli najua wananchi wanaipenda hiyo lakini hii sio elimu ndugu zangu.
nieleweni watanzania
 
Kama ni hivyo mbona mahesabu rahisi kwa kuwa wengi walipata ziro yaani 60% assume wote hawa walikuwa na wastani wa marks 35 ambayo NECTA waliichukua kama F kwa sasa ni D huoni wataangukia kwenye div 4 ya points 28 sasa ndio malengo ya watahiniwa wengi
 
tume zote zinazoundwa hazina jipya zaidi ya maslahi ya kisiasa.nalo hili litapita kama gari bovu kwa trafic barabarani
 

kwan wamesema wanasahihisha?!!! wamesema watatumia system ya kutunuku iliyokuwa inatumika miaka ya 2011 na kurudi nyuma, ingawa hiyo siyo suluhisho la elimu TZ.
 
NECTA ni wababaishaji, nafikiri kuanzia sasa kuna haja necta waseme kabla ya mitihani kwamba mwaka huu grading system itakuwa hivi. mfano waseme A itaanza 85-100 na F itaanza 0-40 au 49 na ile tume ya kutunuku isiwe[po tukisahihisha palepale tupange matokeo kwenye zile panel, tuache ubabaishaji katika hili.
 
Je unadhani ukitumika huo utaratibu matokeo yatakuwa mazuri? Maana ziro zilkuwa nyingi ambapo walitumia 35 kama F sasa hiyo itskuwa kama D huoni bado watapunguza ziro kdg na kwenda four?

vipi kuhusu A, B, C and D zilianza kwa viwango vilevile walivokuwa wakivijua walimu na wanafunzi kabla ya mtihani kusahihishwa? kuepuka haya mambo necta iwe inatangaza kabla ya mitihani yenyewe kuanza na tungeokoa pesa za kuunda tume ovyoovyo.kwani kuna ubaya gani necta wangetangaza kabla ya watahiniwa kuketi kufanya mitihani kuwa mwaka huu grading system zimebadilika na wakabainisha kwa kutuma waraka kwa kila shule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…