Siungi mkono rasimu ya katiba mpya

Siungi mkono rasimu ya katiba mpya

Joined
Aug 10, 2011
Posts
35
Reaction score
13
Yaani mimi binafsi siungi mkono kabisa rasimu hii. Kwa kuwa ukiisoma rasimu nzima hakuna hata sehemu moja imetambua uwepo wa Mhasibu Mkuu wa serikali. Yaani taaluma hii ya uhasibu haikuguswa kabisa ! Nataka katiba mya ilitambue hilo !
 
Hao wako tofauti kabisa. Mkaguzi mkuu kazi yake ni kukagua tu, tena ni mpaka aagizwe kufanya hivyo. Lakini mhasibu mkuu kazi yake ni uhasibu tu. Tena hasubiri mpaka aagizwe kufanya kazi yake hiyo !
 
Mkuu ile ibara ya 207 ya rasimu imemtaja CAG, na kwamba ataidhinisha matumizi kutoka mfuko mkuu wa Hazina ya serikali kulingana na masharti yatakayowekwa. Sasa maombi ya matumizi atakayoyaidhinisha yanatakiwa yafanywe na mtu na huyo mtu ndio PMG. Katiba ina principle ya simplicity bila hivyo nadhani wangetajwa watu wote na kutengeneza kitu kigumu kusomeka na kutumika.
 
Hapo bado wamemtambua CAG tu tunataka tunataka na ACCOUNTANT GENERAL nae awepo kwenye katiba mpya na ijulikane umuhimu wake na wajibu wake ! Haya mambo ya kumtaja indirect ndio yanayoturudisha nyuma wahasibu ! Mpaka mishahara yetu nayo inakuwa nyuma !
 
Back
Top Bottom