Siwa ya Bunge Maalum la Katiba yakataliwa! Ingeligharimu Taifa 500mil

Siwa ya Bunge Maalum la Katiba yakataliwa! Ingeligharimu Taifa 500mil

ablood8

Senior Member
Joined
Aug 12, 2010
Posts
181
Reaction score
90
Kamati ya Bunge la katiba imesitisha siwa kutokana na gharama kubwa ya utengenezaji wake. Eti wananchi hawatawaelewa

=================================
Maelezo ya Mjadala huo wa Fimbo hiyo Fuata | https://www.jamiiforums.com/katiba-...a-zaidi-ya-milioni-500-kutengeneza-fimbo.html

Nazidi kuamini zaidi Kwamba kuna Mtu/Watu wamesaidia kutengeneza Shimo la Fedha ambazo Ni Nyingi mno zinazosaidia Bunge la KATIBA Kufanya kila inalojisikia kufanya hususani Matumizi ya Fedha pasipo Kujali mustakabali wa maisha ya Leo ya Mtanzania.

Kama Bunge (bila Aibu) Leo wanajadili kutengeneza FIMBO Kama Kinyago flan wanachokiita SIWA, Yenye uzito wa kilo Nne Na Nusu ya Dhahabu (4,500gram Kama gram moja Ni 97,000/= hapo tuna (97,000 x 4,500 = 436,500,000) hapo ukitia ufundi (Artist ambayo Ni 1/3 ya gharama hiyo nadhani Hii Ni Fedha ya Kutisha mno.. Naskia PATAKUWA NA SIWA MBILI hapo Ni zaidi ya Bilioni Moja..

Nadhani Kama wanaamini FIMBO Ni muhimu watengeneze FIMBO ya Mbao hasa mpingo Yenye thamani ya Chini ya Laki Nane ambayo in mbao ya Tanzania. Na endapo wanataka Alama Za historia ujengwe mnara Kama alivyoshauri Professa Tibaijuka ambao hauta gharimu zaidi ya Milioni 20.

Kama wakiitengeneza hiyo SIWA YA dhahabu ya zaidi ya Milioni 500 wakaandika hayo majina yako ...najiuliza nani atalinda dhahabu hiyo Baada ya Bunge hili. Je itahifadhiwa Ndani ya CHUMBA imara (STRONG ROOM) nani Atasoma majina hayo. Sidhani Kama wabunge wanawaza Ni Nini wanakijadili Unless watufafanulie huyo aliyewatengenezea shimo la Fedha ndiye anayewalazimisha Kufanya matumizi hayo kufuru..!!!!!

---------

8667No2.JPG
 
Afadhali maana zingeondoka km millioni mia 6
 
Na kwanza hiyo siwa ya nini? Watanzania wanakula siwa?

Posho TZ shs 300,000/per day...jamani jadilini hoja iliyomileta na mfanye maamuzi magumu ya kumuongezea fursa na neema mlala hoi na mrudi makwenu ndugu wabunge.

Nakubaliana na kauli ya Mtikila kuwa hili ni Bunge la hovyo...kupita mabunge yote.
 
kwani hii iliyopo inamatatizo gani?
 
Na kwanza hiyo siwa ya nini? Watanzania wanakula siwa?

Posho TZ shs 300,000/per day...jamani jadilini hoja iliyomileta na mfanye maamuzi magumu ya kumuongezea fursa na neema mlala hoi na mrudi makwenu ndugu wabunge.

Nakubaliana na kauli ya Mtikila kuwa hili ni Bunge la hovyo...kupita mabunge yote.

Mtikila ametisha sana
 
CCM was Born to Lead, It Leads by Demonstrate Good governance.
 
Hayo ni maamuzi ya busara sana. kwa kuwa hiyo siwa ingetumika kwa miezi mitatu tu kwa ajili ya bunge hilo tu. Kimsingi watu ndio wa muhimu katika bunge hili la katiba na nimefurahi sana kwa uamuzi huo.
 
Wangeikubali ningewashangaa,, hili bunge lakatiba nijanga la jk
 
Waipe wizara ya afya hizo hela wanunue machine ya ct scan ifungwe hospitali ya Mbeya
 
Hii ingepatikana bila ya kutoa hata senti tano ,hata kama wangetaka kuwekea almasi na tanzanite ila viongozi wetu hawajiamini juu ya maliasili zilizopo nchini ,hawana uhuru nazo ,hivi wangeweka pembe ya ndovu kungeharibika kitu.

Isipokuwa hapo palikuwa na wajanja na ni hao waliobuni kutaka kukwapua ,wacheni mchezo nchi hii kuna watu shapu ile noma !
 
Si wampe kazi mmakonde yeyote awachongee rungu ya mpingo?
 
ilikua deal ya watu wapige hela. Tunahitaji katiba bora na si siwa bora!
 
Back
Top Bottom