Hmaster
JF-Expert Member
- Dec 27, 2010
- 346
- 86
Ukienda baa peke yako kama wewe ni mwanaume utapewa huduma kwa unyenyekevu sana na wahudumu hawa wa kike hadi utajiona kweli wewe ni mfalme kama ule usemi usemavyo "mteja ni mfalme". Kabla hujatulia kwenye kiti, utaona mdada keshafika zamani huku akitabasamu na kukusalimia kabla ya kukuuliza unahitaji huduma gani. Utakapompa order haraka atakuletea kinywaji na kabla hajafungua ataanza kwa kufuta meza kisha atakufungulia kinywaji. Baada ya hapo atasuuza glass kwa kutumia kinywaji hichohicho na kisha atakumiminia kinywaji chako katika glass na mwisho atakukaribisha. Hatakupa change yako kwanza ila ataacha kapu tray lake hapo kwako na kwa maana hiyo hapo ndiyo patakuwa centre yake kuu, ingawa hamuongei. Mtu mwingine akija atamuhudumia kisha anarudi hapohapo kwako.
Cha kushangaza ni pale utakapokwenda baa na mdada! Muhudumu utamwita wewe, akija hana salamu wala nini. Atakuuliza aina ya vinywaji mtakavyo na akileta anakuja na change yote hafuti meza, akishafungua tu anaishia na hutamwona tena hadi umwite ili awaongeze vinywaji. Hata lugha yao huwa ni ya mkato sana wakiona una demu. Ukimweleza glass ina ufa nibadilishie, atakwambia zimeisha au zote zipo hivyo. Siwaelewi ni kwanini wanakuwa hivyo. Nawasilisha!:angry: