Binti siku moja mzee mmoja aliwahi niambia kuwa siku wanawake wangekuja kujua umuhimu wa kazi wanazozifanya wasingetaka hata siku moja mwanaume azijue akajifanyia. Rafiki yangu mmoja alitengana na mkewe kwa muda hivi, kabla hawajarudiana nilimuuliza ni kitu gani kinacho miss kwenye maisha yake tangu aachane na mpezi wake, jibu alilolitoa lili nifanya nimpigie simu yule mzee kukubali usemi wake..eti jamaa hawezi kupata soksi zake asubuhi kwani siku zote mkewe ndio alikuwa anampangia soksi..and that small things ndivyo vinavyowafanya wanawake muwe spesho kuliko viumbe wengine huku duniani( oni siriasi noti)