Siwema wa Nay wa Mitego atiwa mbaroni, kisa ni kumpiga picha za uchi na kigogo wa Serikali

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Mzazi mwenzake staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson (27) ametiwa mbaroni na kusota rumande kwa siku kadhaa akidaiwa kujipatia mali kwa njia ya vitisho kutoka kwa kigogo mmoja serikalini (jina linahifadhiwa kwa sasa).

Mei 2, mwaka huu, Siwema alilala ‘nyuma ya nondo’ (mahabusu) kwa siku mbili katika Kituo Kikuu cha Polisi, Wilaya ya Nyamagana jijini hapa baada ya kukamatwa nyumbani kwake Lumala, Manispaa ya Ilemela.

Kwa mujibu wa chanzo, awali ilidaiwa kuwa, Siwema aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kigogo huyo jijini hapa kwa ahadi ya kufunga naye pingu za maisha kufuatia kigogo huyo kufiwa na mkewe.

Ikazidi kusemekana kwamba, wawili hao wakiwa ndani ya uhusiano, Siwema hakuwahi kumfahamisha kuwa ana mchumba ambaye ni Nay. Ikafika mahali, kigogo akamvisha pete ya uchumba, picha zikatoka kwenye gazeti moja .

Ilizidi kuelezwa kuwa Nay baada ya kugundua kuwa Siwema amevishwa pete ya uchumba na kigogo huyo, alihamanika kiasi kwamba taarifa zilimfikia kigogo huyo wa serikali naye akaamua kujitoa kwa Siwema, akaoa mwanamke mwingine.

“Tatizo Siwema hakuwa muwazi kwa kigogo kwamba, Nay ni mchumba wake. Lakini kabla ya kigogo kumtema Siwema, kumbe alishawahi kumpiga picha za utupu mwenyewe akiwa hajui.”

“Sasa baada ya Siwema kumwagwa kutokana na kelele za Nay kwamba demu ni mchumba wake, ndipo zile picha Siwema alizitumia kumtishia amnunulie gari vinginevyo angemwanika kwa kuzitupia kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook,” kilieleza chanzo hicho.

Ikazidi kuelezwa kuwa, aliposikia vitisho hivyo, kigogo huyo aliamua kumweleza mkewe juu ya sakata zima ambapo walikubaliana kumnunulia Siwema gari na akampa na kiasi cha fedha kwa masharti ya kuzifuta picha hizo kutoka kwenye simu yake


“Lakini Siwema licha ya kununuliwa gari aina ya Honda CRV na akapewa na kiasi cha fedha alichotaka, bado hakuzifuta picha hizo kwenye simu yake.

“Kana kwamba haitoshi, aliendelea kumtishia tena ambapo safari hii alitaka atumiwe kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya mtaji wa biashara, jambo lilimnyong’onyeza kigogo huyo na kuamua kwenda kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola kwa hatua za kisheria,” kilisema chanzo.

Akizungumza na gazeti la Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, Charles Mkumbo alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Alisema Siwema alikamatwa baada ya mlalamikaji kutoa taarifa kwa jeshi hilo ambapo walifungua jalada la uchunguzi Mei 2, mwaka huu na siku hiyohiyo walimkamata mtuhumiwa akiwa nyumbani kwake, Lumala Manispaa ya Ilemela.

“Ni kweli tulimkamata Siwema Edson (27), mkazi wa Lumala. Ametuhumiwa kujipatia mali kwa njia ya vitisho. Awali alikuja mlalamikaji kabla ya kukamatwa.

“Hawa watu awali walikuwa wapenzi. Katika mapenzi yao, siku moja, Siwema alimpiga picha za utupu mlalamikaji bila yeye kujitambua wala ridhaa yake,” alisema DCP Mkumbo.

Alisema baadaye uhusiano wao ulivunjika, ndipo Siwema akatumia picha hizo kumtishia kuwa kama hatatimiza matakwa yake kwa kumnunulia gari na kumpa fedha, basi angezisambaza picha hizo kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook.

“Mlalamikaji alitimiza matakwa ya mtuhumiwa kwa kumnunulia gari aina ya Honda CVR lenye namba za usajili T103 DDU na akamtumia na fedha. Lakini Siwema aliendelea kumtumia vitisho, akimtaka amtumie kiasi kikubwa cha fedha za mtaji, ndipo mlalamikaji akaja kutoa taarifa polisi, likafunguliwa jalada la uchunguzi na siku hiyohiyo akakamatwa,” alisema DCP Mkumbo.

Aliendelea kusema kuwa, kwa sasa gari hilo linashikiliwa kituoni hapo huku Siwema akiachiwa kwa dhamana wakati upelelezi ukiendelea. Ukikamilika atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alisaini sheria ya makosa ya mtandao.

Sheria hiyo, inakataza mtu kutumia mitandao kwa nia ya kumchafua mtu au kuanika picha zake, hasa za utupu bila ridhaa yake.
 
Mbona kuna hbr nyingine ilikuwa humu ikidai,siwema kanunua gari kwa pesa yake mwenyewe.kumbe nyuma ya pazia pako namna hii?duh!wacha picha liendeleee.
 
mi nashindwa elewa....,siwewa alimpga picha enzi izooo...akaja kuishi na ney wakazaa jamaa akaoa mwingine
baada ya kuachana na ney ndo kapeleka picha na jamaa kakubali kuingia gharama za gari?????
 
Mbona kuna hbr nyingine ilikuwa humu ikidai,siwema kanunua gari kwa pesa yake mwenyewe.kumbe nyuma ya pazia pako namna hii?duh!wacha picha liendeleee.

hahaaaaaa huwajui wadada wa mjini eeehh
 
mi nashindwa elewa....,siwewa alimpga picha enzi izooo...akaja kuishi na ney wakazaa jamaa akaoa mwingine
baada ya kuachana na ney ndo kapeleka picha na jamaa kakubali kuingia gharama za gari?????

Ah ah Ndo uwezo wako wa kufikiri umefika hapo... Nay alimuacha siwema baada ya kigogo kumvalisha Pete..kigogo naye akaamua oa mwanamke mwengine Ndo siwema akamaliza hasira kwa kumblackmail kigogo
 
hahaaaaaa huwajui wadada wa mjini eeehh
kweli wadada wa mjini kiboko.ila naona kigogo alitumia busara kumueleza mkewe kuliko angemficha.ss siwema akatafute mwingine wa kumtisha mana huyu ashamkomesha.
 
Wasichana wa Tanzania baadhi yao wana akili ndogo sana hata sisimizi wanazo kubwa
 
Ana miaka 27 umri nao umemtupa bdo anaonekana mbichi!
 
Siwema mwenyewe ana sifa ya kuzoa zoa waume za wenyewe.....
 

nifah rudi uisome vizuri utaelewa...Uko wazi kabisa na inajieleza vizuri
 
Last edited by a moderator:
kuna aya inaeleza Hivi haada ya kumvisha Pete huyi siwema na picha kutoka gazetini na ney akaziona ndipo akalianzisha na hatimae kigogo hivyo akamwacha siwema na kuoa mwanamke mwingine.....na hivyo ndiye aliyeelzwa Lisa na wakaamua kumnunulia gari siwema ili yaishe......
 
Last edited by a moderator:
nifah Kuna aya inaeleza Hivi haada ya kumvisha Pete huyo siwema na picha kutoka gazetini na ney akaziona ndipo akalianzisha na hatimae kigogo huyo akamwacha siwema na kuoa mwanamke mwingine.....na huyo ndiye aliyeelzwa kisa na wakaamua kumnunulia gari siwema ili yaishe......
 
Last edited by a moderator:
Mwanamke ambaye simwelewagi ni huddah the boss chick,ni mwigizaji au?nini kinamwingizia hela maana Insta na pics za kula bata tu
 

I got you, sorry for misunderstood.
 
Last edited by a moderator:
huyo kigogo mjinga kwanini na yeye asimtie adabu dume zima limeonga gari kwa kutishwa tuu mi mbona angenisoma shenzi zake kazi ataki anataka njia nyepesi tuu
 
Ah ah Ndo uwezo wako wa kufikiri umefika hapo... Nay alimuacha siwema baada ya kigogo kumvalisha Pete..kigogo naye akaamua oa mwanamke mwengine Ndo siwema akamaliza hasira kwa kumblackmail kigogo

unadhani hayo siyajui????nayajua mengi zaidi yako...na nimeyajua kabla yako wewe......umekalili kila sehemu unaquote eeh.....!usidandie dandie ovyo elewa kwanza!
 
Mwanamke ambaye simwelewagi ni huddah the boss chick,ni mwigizaji au?nini kinamwingizia hela maana Insta na pics za kula bata tu

Kazi yake kubwa anajiuza ,niliwai pata namba yake nikawa namjaribu akaniambia nimtumie ticket ya ndege biznes class na gharama dolla 5000 kwa siku mwisho dolla 3000 nilikuwa nataka kuprove tu,ndio nikaamini Dinazarde
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…