Siwezi kukata kiuno hadharani-Johari

Siwezi kukata kiuno hadharani-Johari

Rich Pol

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2013
Posts
7,874
Reaction score
5,685
Blandina Chagula 'Johari' ambaye ni mmoja wa washiriki wa filamu mpya ya Wrong Hope, amewaponda wasanii wa filamu wanaokubali kukatishwa viuno mbele ya hadhara na kueleza kwamba kamwe kwa upande wake hawezi kufanya jambo hilo hata kwa malipo namna gani.

"Siwezi kujidhalilisha mbele ya umati kwa kukata kiuno, ni ulimbukeni tu kukata viuno mbele ya watu, labda niwe nimelewa kiasi cha kutojitambua ndo naweza kufanya madudu kama hayo," alisema Johari.

Aidha, Johari alisema kuwa kuna umuhimu kwa wasanii wa filamu kujitambua na kufanya mambo ya maana kwa jamii kuliko kujigeuza kituko na kufanya mambo ya ajabu.

Mrembo huyo alihitimisha kwa kuwaomba mashabiki wake waipokee kwa mikono miwili filamu yake mpya ya Wrong Hope itakayotoka mwezi ujao ambapo ndani yake yumo Mohammed Nurdin'Chekbudi' na marehemu Sheila Haule 'Recho'.
 
Dada yetu amekongoloka sana sijui ni stress au anagombana na umri?
 
Kwa kiuno kipi sasa?Aseme mengine kiuno awaachie kina Snura
 
Ivi hata kiuno chenyewe anachokweli mmh...
 
hata nayeye ananjia zake za kujidhalilisha, sio mpaka kukata mauno hadharani... she ain't perfect as she is trying to claim..!!!
 
Angekuwa name uwezo kama wa Fifi moto angekionyesha tu hadharani.........shutting down
 
Back
Top Bottom