Siwezi kukuoa Kwa sababu nimekupa ujauzito!

Siwezi kukuoa Kwa sababu nimekupa ujauzito!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
SIWEZI KUKUOA KWA SABABU NIMEKUPA UJAUZITO!

Anaandika, Robert Heriel.

Jilengeshe! jibebeshe! jitegeshe! Utajua mwenyewe. Oooh! Kama ulikuwa hutaki mtoto si ungetumia Mpira, ooh! Kama hukuwa unanipenda mbona ulinifuata ukanitongoza, ooh! Kwa nini hukupiga shut fyongo likaenda nje, wewe ukalenga Golini. Oooh! Kama ulikuwa humpendi mtoto wetu nini kilikufanya umfuate?
Seriously!!

Unasemaje? Embu rudia!
Yaani unauliza paka shume Kwa nini Kala mboga kwenye jungu lililoachwa wazi. Seriously!! Come on!

Sikiliza, nisikilize vizuri Sana! Hutaki Acha!
Ulijibebesha! Utajibeba. Ulijitegesha! Utajitegua! Mimi simo.
Kizazi cha nyoka na kenge alafu bado ukaacha mayai yako waziwazi unategemea nini.
Hutaki Yai lako lirutubishwe na Majoka na Kenge maji basi ficha mayai yako. Eboo!

Mimi sijakuoa Mimi, Mimi sio mume wako Mimi! Sisi sio wanandoa Sisi. Sisi ni wahuni Wawili Sisi! tunaofanya mambo ya kihuni.
Ushaambiwa wahuni sio Watu ukadhani masikhara!
"Samahani usiniite mhuni, mhuni labda ni wewe unayekataa mimba yako, sijui likoje"
Sawa! Mimi mhuni! Vipi wewe, niambie wewe ni Nani?

Mimi sijakataa mimba. Lakini hiyo sio kisingizio cha kukuingiza katika uzio wa ndoa baina yangu.

Siwezi kukuoa Kwa sababu ati umejiamulia kujibebesha mimba, umejitegeshea mtego wako ukadhani utakamata Nguchiro. Mimi sio Nguchiro.
Ungeniuliza Kwanza Kabla hujachukua maamuzi hayo.
"Nikuulize kwani wewe hujui?"
Nijue nini? Ulifikiri nilikufuata ili nijue mambo ya mimba sio?

Sikiliza, mambo tuliyoyafanya ni mabaya Sana. Hata ndio matokeo yake.
Hatukuwa na adabu na hii imegeuka adhabu kwetu.
Tulifanya mambo ya aibu gizani sasa tunapata tabu mwangani.

Mimi sina Mpango wa kukuoa, sio wewe tuu hata wengine sijafikiria kuwaoa. Yaani ndoa kwangu haipo Akilini.
Kiukweli nimekosa maadili, sio Mimi tuu hata wewe uliyenikubalia katika shauri la mtenda mabaya.

Tumewaasi wazazi, tumezikimbia Mila na desturi zetu. Tumefanya mambo ya ajabuajabu yenye aibu katika jamii yetu.
Sasa Nani ataumia, wote! Mimi, wewe na mtoto. Jamii yote itaumia kwaajili ya mambo yetu ya kihuni.

Siku Ile nilivaa kibrazameni, raba Kali ya kitasha, Tsheti ya kisharobaro na Jeans matata, usoni nikaweka Ile Miwani ya Wackojacko ili nifanye Smoothly Criminal kwako. Nilifanya! Kwa sababu wewe badala unione kama Bedui mharibu ndoto, ukanisifu ati nimependeza kama Msanii WA Kimataifa, ATI uliniambia unapenda Vijana kama Mimi wenye pigo za kijanja.

Yule jamaaako ambaye ulimtukana sio wahadhi yako, ukamuita majina ya hovyohovyo, mara mashamba, mara anapigo za Kilokole, mavazi ya kisabato Sauti ya Kilokole.
Hukujua Yule ndiye alikuwa na Nia ya kukuoa? Eeh! Hukujua nakuuliza?

Ukadhani Ile kapero yangu ya NY ndio italeta ndoa, seriously?

Sikiza!
Mrudie Yule jamaa yako Kabla hiyo mimba haifika mbali. Mrejelee, mwambie nimerejea Kutoka Misri. Mueleze upo tayari kusaini Contract. Najua atakubali.
Mimi najua nakuambia!

"Taikon umelogwa? Unaongea manini hapa. Unataka nimsingizie mkaka wawatu mimba?"
Leo amekuwa mkaka wa Watu sio, unamuonea huruma sio.
Kama unataka ndoa nenda Kwa mshikaji maana kwangu hakuna Ndoa.
Ila kama unataka tuendeleze uhuni Baki.
Nimemaliza!

Binti zangu, jihadharini Sana. Hiki kizazi ni cha nyoka. Kuweni Makini mno. Kupata mimba au kuzaa mtoto sio kisingizio cha kuolewa. Ila ni matunda ya Matendo mlioyafanya.
Jitahidini mfuate utaratibu, jueni kuwa kutofuata utaratibu inakula upande wenu zaidi kuliko Kwa Sisi Vijana.

Mimi nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ila wanaumeee
Na maswala ya mimba jamani

Tuendelee kula pipi zenye maganda ebooh
 
Hata mie juzi kuna demu anakuja huku analia eti nikajutambulishe kwao kisa amenasa (mimba) nikamuuliza, nitakuwa na uhakika gani kama ni ya kwangu? Halafu suala la ndoa kwa sababu una mimba kwangu halipo! Potea. Naona ameni block. Halafu hawa mabinti siku hizi wana mchezo wa kubambikia watu mimba wkaizinguliwa na me zao waliowapa mimba
 
Hata mie juzi kuna demu anakuja huku analia eti nikajutambulishe kwao kisa amenasa (mimba) nikamuuliza, nitakuwa na uhakika gani kama ni ya kwangu? Halafu suala la ndoa kwa sababu una mimba kwangu halipo! Potea. Naona ameni block. Halafu hawa mabinti siku hizi wana mchezo wa kubambikia watu mimba wkaizinguliwa na me zao waliowapa mimba
Ambavyo hampendi kusikia hizo mambo, basi msipende kula dry
 
Ninyi ndio mnatakiwa msipende kuliwa Dry.
Hii ishu Ipo juu yenu zaidi hasa mkiwa hamjaolewa
Japokuwa wote tunatakiwa kuwa makini , ila wanawake wanatakiwa kuwa makini zaidi.

Ikiwezekana wawe wanatembea na ndom kama wale wadada wauzaji.
 
Na mkitoa mimba mtazidi kukoma sisi hatukuwaambia tunatk watoto tutawalisha Nini ikiwa hata matumbo yetu yanatupa tabu kuyahudumia hatutaki mizigo mtawatesa ndugu na wazazi wenu Bure tu
 
Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza, wakinadada hili nalo mkalitizame.
 
Unazingua mkuu,
Ukijua huna mpango wa kumuoa,
Chonde chonde Usimmwagie ndani

Wengi hawakumwagia ndani na mimba zimetunga.
Njia salama ya kujikinga na mimba ni Kutumia kondomu, au kutokufanya Kabisa.
Au Kutumia zile njia zingine za Uzazi wa Mpango.

Kumwagia ndani hakujawahi kuwa mbinu ya kuzuia mimba. Na hii imewagharimu wengi Mno.
 
Binafs naamini sio kila mwanamke ni wa kuzaa nae, hasa yule ambae unajua kabisa huna mpango wa kumuoa.

Tusiwachezee mabinti na kuwafanya singo mother Kisha tuje kuwasimanga humu
 
Back
Top Bottom