Price na Value ni vitu viwili tofauti.Watu wenye pesa hawalipi sababu umetaja bei, bali sababu ya thamani ya kitu. Ndo maana kuna mtu yuko tayari kutoa 3M akanunua full grown GSD....wakati wewe unaona thamani ni mbuzi na ng'ombe.
Kuna mtu ananyumba vyumba viwili na anaona hana huhitaji wa nyumba kubwa na hapo ana watoto watano na kuna mwamba ana mtoto mmoja but ghorofa, sqm 2000, swimming pool etc na wanaishi watu wanne tu..
Kuna watu wanalipia utelezi 3000/= anamshangaa anayetoa 50,000/= na hapo kuna mtu anatoa 500,000/=.
Kuna mtu ana C.C 3600 na kuna mwamba ana C.C 1200 anamashangaa wa 3600 sababu wote wanatembea wamekaa.
Kuna mtu anatoa 300M anachukua plot/nyumba mbezi beach, kuna mwingine anashangaa why huyu asiende Kibaha akachukua plot safi kwa 30M tu nyingine akanunua ng'ombe.
Kuna mtu anakipia ada 7M mwingine 150,000/= huyu anamshangaa huyo wa juu kupoteza pesa..
ISSUE NI VALUE. - THAMANI - THAMANI