yeah mkuu, wakati huo kulikuwa na shule 2 tu za ufundi za kitaifa: Moshi Technical na Ifunda. na vyuo vilikuwa vitatu tu - Dar Tech, Arusha Tech na Mbeya Tech. kwa hiyo mkimaliza form four kwa mfano moshi Tech basi darasa zima mnajikuta mpo Dar Tech. Wakati huo nchi ilikuwa na mkakati wa kupata mafundi kwa ajiri ya viwanda vyetu, nafikiri ilikuwa ndoto ya Mwalimu. sasa hivi shule hizi zipo hoi bin taaban.
ufundi unasaidia sana usichakachuliwe, kuna siku nikawa nimepeleka kigari changu garage, belt ya engine ilivyatuka, nikanunua belt nyingine sasa wakati wa kufunga nikawa pale nacheki, yule fundi akanitania wewe hata uangalie huwezi elewa kitu -- sasa kumhakikishia mimi si kilaza nikaanza kushuka nondo zangu za Automechanics (somo la unga); wale madogo wakaanza kuelewa timing ni nini na inaathiri vipi mapigo hayo manne ya engine. kwa muda nikawa mwalimu, madogo wakanikubali. sasa hivi nikienda kufanya service wananiita Karibu Fundi ---- interesting....pamoja sana mkuu hata mie nimesoma Moshi Technical, bt nilikimbia ufundi nikaenda Advance PCM, then nikaenda Engineering. one thing naweza kukuambia Moshi Technical imekuwa sehemu muhimu sana katika maisha yangu, huwez nidanganya kitu chochote cha kiufundi, maana ile mambo ya form one kusoma maufundi yote ile...mh inasaidia sana kuwa na idea....halafu UDSM napo miaka hiyo ukiingia Engineering lazima usome maufundi almost yote...sijui kama siku hizi bado wanafanya hivo...
Hakuna kitu kama hicho.If a body is fully or partially immersed in a fluid, it displaces its own weight of the fluid.
Hapana kaka, hiyo sio Archimedes Principle, hakuna kitu kama hicho.Hii ni Archmedes Principle