Samico Tanzania
JF-Expert Member
- Feb 6, 2022
- 486
- 1,237
Sijui kama nakosea lakini mimi huo muda wa kumshauri mtu aache ulevi au umalaya huwa sina kabisa hususani kama mtu huyo katika ulevi wake ndo unaodumisha urafiki wetu.
Tangu nikiwa mdogo hii tabia nilikuwa nayo!
Wakati nasoma shule ya msingi kipindi hiko tulikuwa tunakaa kwenye mawe na matofali!
Darasani kulikuwa na benchi bovu dogo ambalo lilikuwa linakaliwa na mtoto mwenzangu ambae alikuwa mbabe sana!
Sasa siku ambazo alikuwa haji shule alipanga nani akae pale akiwa yeye hayupo! Alinichagua mimi rafiki yake nikalie bench lake siku ambazo hayupo maana alikuwa mtoro sana.
Sasa baada ya utoro kukithili sana mwalimu akaandika barua ya wito akauliza darasani nani rafiki yake apeleke hii barua kwao!
Watoto wote wakanichagua mimi niipeleke!
Nikaichukua wakati nikiwa njiani nikawaza hivi huyu akija shule si ndo nitarudi kukaa chini mimi!
Nikasema kwa hili mwalimu atanisamehe! Nikachana nikatupa kule!
Nikaendelea kula kitabu juu ya dawati bovu freshi!
Ikaandikwa nyingine niipeleke! Nayo nikanyoosha mkono fasta ili asipewe mwingine ikafika nikarudi kukaa chini! Sikuipeleka ingawa nilifika kwao nikawasalimia!
Mzazi wake akaniuliza SAMICO vipi shule! Nikamjibu hakuna cha maaana tunacheza tu bora rafiki yangu anavyotega! Nikamwambia hata jina lake huwa namuitikia lakini mwambie angalau awe anakuja mara moja kwa mwezi!
Tangu mtoto niliamini utoro wake ni neema kwangu hivyo kamwe sitakiwi kabisa kumshauri maana hata urafiki wetu ungeisha!
Nilivyomaliza shule msingi nikawa nachunga ng'ombe!
Nako huko nilikutana na mvivu wa kuchunga hili nalo lilipa faida sana! Jamaa aliniletea ng'ombe wao niwachunge akawa ananipa posho na vinguo nguo! Sikumshauri hata siku moja aache uvivu maana katika uvivu wake nilifaidika!
Maisha hayo nimeendelea nayo hadi leo! Siwezi kupoteza muda kumshauri mtu aache kilevi ambacho katika ulevi wake mimi nafaidika!
Kama ulevi wako nikujenga majumba sasa nikikushauri uache kujenga ukanunue mabasi mi pesa za ufundi nitapaje?
Kama una kilevi cha kujenga mimi kama fundi wako ndo nitakuletea madili ya viwanja vya bei rahisi ununue ili nipate tenda!
Kama ukilewa ndo unapoteza kumbukumbu za madeni hivi mimi naanzaje kukushauri uache pombe? Si ndo nitakuletea visungura dabodabo ili urafiki unoge!
Kama katika umalaya wako ndo urafiki wetu unadumu kwanini nisikuoneshe machimbo ya malaya wa mwendokasi?
Siwezi kabisa kumshauri mtu aache kilevi anachopenda maana kumshauri ni kutaka kusambaratisha urafiki wetu!
Yaani mfano kuingia JF hapa kama ndiyo kiunganishi halafu mwenye jamii forum atushauri tusikae sana Forum si huu mtandao utakosa wachangiaji?
Sina muda wa kumshauri rafiki yangu Mlevi labda kama nimemchoka!