Siwezi kuwapigia makofi mashujaa FC kwa ushindi wao wa mchongo ulioaandaliwa na lazima wapande ligi kuu

Siwezi kuwapigia makofi mashujaa FC kwa ushindi wao wa mchongo ulioaandaliwa na lazima wapande ligi kuu

TFF na Bodi ya ligi sijui masuaala ya Michezo Kama hii huwa mnayabariki??

Mbeya City walinyongwa hadharani marefa walikua upande wa mashujaa (hakuna haki kwa Mbeya City)

Hakuna offside lakini kibendela kinanyanyuka.

Kuna kipindi Mbeya City walishituka kuwa kila wakisogea kwenye box la mashujaa lazima iwe offside hata Kama siyo offside na wakaanza kupiga mashuti nje ya box.

Kosa siyo kosa lakini Mbeya City wanaadhibiwa Ila kwa mashujaa hakuna kitu (mama nibebe)

Wachambuzi wengi wamefumba midomo kwa kua hii ni Mbeya City lakini matukio Kama haya yangetokea kwenye timu za kariakoo (Simba na Yanga) hakika zingepigwa kelele mwezi mzima.

Kwa hili NALIA NGWENA siwezi kupiga makofi na kuwapongeza Mashujaa kwa janja janja zilizowafanya wapande ligi kuu.

View attachment 2668228
huwezi amini mdau hao wanambeya wenyewe wameshukuru sana ile timu ishuke daraja maana siasa ilishaingia pale...eti timu kakabidhiwa tulia wakati enzi ya sugu walitaka kumkabidhi timu akawakatalia ila michango na kwenda uwanjani kuwashangilia aliwasapoti sana...........baada ya miaka kumi mbeya city byebye
 
Back
Top Bottom