Siwezi sahau jinsi ambavyo nilidhalilika na Tozo kipindi kile zimeanza

Siwezi sahau jinsi ambavyo nilidhalilika na Tozo kipindi kile zimeanza

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Siku hiyo nimeamka asubuhi wapinzani wanaongoza. Sina kitu mfukoni. Na simu yangu hata ku deeku haiwezi. Nipo majalala kinoma aisee. Nikawaza nikaona hapa nimuibuikie mwanangu wa damu Gilongwe kijiweni kwake Mwenge.

Basi nikaanza kucheza Reggae mdogo mdogo toka Tegeta mpaka Mwenge. Kufika Mwenge mjuba hayupo katika kudodosa jamaa wakaniambia hawajamwona ila mmoja akasema Gilongwe jana kapokea mshiko flani leo sidhani kama atatokea. Nawauliza kama wanaweza mpigia mwana.

Jamaa mmoja akajaribu. Simu haipatikani. Nikamwomba ajaribu tena na tena.mwishowe jamaa akawa mkali kuwa sasa kama amezima nikipiga mara nyingi itajiwasha? Nikaona hapa hatari. Nikaaanza saga Rhumba mpaka Temeke. Nilipofika kwake wakaniambia katoka kaelekea Mbagala mwisho wakanielekeza alipo. Nika dance mpaka Mbagala. Hola. Ishakuwa jioni. Hali mbaya. Nlikuwa nimekunywa maji tu mpaka muda huo.

Nikakumbuka kuna mwanangu mwingine yeye si haba anafanya kazi kwa wahindi. Nikaomba mtu ampigie simu. Nikaongea naye na kumwomba anitumie angaa 2,000 nifanye nauli na kula Miyanga (Mihogo).

Jamaa akatuma dk kadhaa msg inaingia.umepokea tsh 2,000. Basi nikaenda kwa Wakala. Nikamwambia wakala nipatie namba yako nataka toa mshiko. Sikutaka taja kiasi maana kulikuwa na mademu wawili wamesimama pembeni.

Mara kidogo simu yake ika vibrate. Nikawa nasubiri anipe mshiko, daaah akaniambia hakitoki kitu. Yaani kutokana na tozo mimi tena nadaiwa Tsh 1,000. Nikahamaki. Haiwezekani. Akanipigia mahesabu. Yaani nimetoa 2000 kwa wakala nadaiwa tena 1,000.

Hapo jasho likaanza kunitoka.nikainama kuanza vua kandambili nikafunga na shati kiunoni, Wakala akaanza kuita watu kuwa nataka nifanye fujo. Kumbe mwenzie hata nguvu za kufanyia fujo sina. Nikaanza kuondoka mdogodogo kuitafuta Tegeta. Narudi home.

Sina hamu kabisa na haya mambo ya tozo. Mpaka hii leo siwezi sahau siku hiyo.
 
Nikifikiria root hizi zote ulizotembea ni kama unatudanganya. Tegeta mpaka Mbagala tena kwa mguu. Hata muuza viombo anatumia usafiri mda mwengine.
 
Katika maisha kuna changamoto nyingi sana , kuna muda mtu unakwama kabisaaa ila kuna watu watakuona mzembe katika kutafuta,
Utasikia tafuta pesa pesa pesa pesa kauli inayotia hasira sana kwa mpambanaji

Sent from my TECNO KD7h using JamiiForums mobile app
 
Hiyo route ni kilometa ngapi? Hivi bila kudanganya unajisikiaje?
 
Hii chai ningeikuta asubuhi,anyway nimeikuta jioni ni uji wa mchele
 
Back
Top Bottom