La haulah hawa jamaa ndio maana wanapata hela sana na faida kubwa sijuagi kama wanakata hizi huwa nachukua tu basi, nilikuwa na current account na savings account, ila current account wanakata sh 10,000 kwa mwezi huduma zingine sijawahi kukagua na sijui labda nichukue statement ya miezi 2 ndio ntajua, ila tatizo lingine nikiwekewa hela kutoka nje ya nchi exchange rate wanayoitumia ni mbovu sana haifai kabisa isitoshe wanakata sh 10,000. nikiwekewa hapa nchini yani ktoka mikoani kiwango mara nyingi ni mil 2 kwenda juu wanakata sh 10,000 yan nakatwa mimi kwa kuingiziwa huwa sielewi hii pesa kwa nini wasisubiri nitoe ndio wakate kweli nitahama nimewasoma sasa ntakuwa nimeshakatwa hela nyingi sana mpaka sasa hivi.