Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,223
- 96,083
Najua wengi mlikuwa bado hamjazaliwa lakini hebu angalieni wazee tulivyokuwa tunapiga mashairi.
Shairi hili nalidediketi kwa vidume vya JF vinaoongoza kwa kupigwa vibuti na mabinti wa JF wakiongozwa na monitor wao The Finest.
TGIF!
Nyie vijana wa sasa, mkitongoza mkakataliwa msibwatuke eti "hamtaki tena kwanza eti mbichi" wakati mnaumia moyoni. Mbona wazee tunajilia vyetu kiulaini?
Kutongoza ni Fani na Kipaji:
Source ODM.
Weekend njema!!
Shairi hili nalidediketi kwa vidume vya JF vinaoongoza kwa kupigwa vibuti na mabinti wa JF wakiongozwa na monitor wao The Finest.
Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia
Sikuile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.
Sungurakarukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.
Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.
Karukatena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.
Sizitakimbichi hizi Sungura akagumia,
Naona nafanya kazi, bila faida kujua,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.
Siokama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.
Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.
TGIF!
Nyie vijana wa sasa, mkitongoza mkakataliwa msibwatuke eti "hamtaki tena kwanza eti mbichi" wakati mnaumia moyoni. Mbona wazee tunajilia vyetu kiulaini?
Kutongoza ni Fani na Kipaji:
Source ODM.
Weekend njema!!