Sizitaki Mbichi Hizi!!

Sizitaki Mbichi Hizi!!

1. Hadithi inayokuja
ni ya sungura sikia
hadithi uliyongoja
leo ninakuletea

2. Alitoka siku moja
njaa aliposikia
njaa aliposikia
sungura nakuambia

3. Siku ile akaenda
porini kutembelea
akayaona matunda
mtini yameenea

4. Sungura akayapenda
mtini akasogea
mtini akasogea
sungura nakuambia

5. Sungura karukaruka
lakini hakufikia
matunda hakuyashika
mkononi hakutia
6. Karuka tena karuka
lakini hakufikia
mwisho wake akachoka
kachoka hata mkia

7. Machozi yakamtoka
pembeni akasogea
pembeni akasogea
sungura nakuambia

8. Sizitaki mbichi hizi
sungura akagumia
naona nafanya kazi
bila faida kujua

9. Sio kama hakutaka
sasa nakupasulia
matunda aliyataka
ndiyo kisa akalia

10. Tunajua hakufika
alichoka kurukia ...

Tupieni mistari tumalizie kisa hiki cha rafiki
yetu sungura.
 

Attachments

  • 311448_2571709061396_1514358659_2843420_1412056303_s.jpg
    311448_2571709061396_1514358659_2843420_1412056303_s.jpg
    3.5 KB · Views: 105
  • ready+to+die.jpg
    ready+to+die.jpg
    8.1 KB · Views: 92
hii si alishaleta Asprin hapa.....au hii ni nyengine.....
 
dah! umenikumbusha mbali sana kaka, hivi watoto wa kizazi hiki cha dotcom wanajua hizo hadithi?
 
dah! umenikumbusha mbali sana kaka, hivi watoto wa kizazi hiki cha dotcom wanajua hizo hadithi?
Ni sisi tu wazee mkuu ndiyo tunajua mambo hayo, elimu ya saizi ilishachakachuliwa.
 
Aisee umenipeleka mbali kweli! Je unakumbuka ile hadithi ya LUSI NA DAMASI?
 
Enzi hizo tupo darasa la tatu kwenye matofari tunalazimishwa kukariri lile shairi mweee
 
hv vitabu vinapatikana wapi siku hz..natamani niwe nacho nijkumbushe enzi!
 
Tulikuwa chini ya mti tunaimba mashairi. Kinyonga akadondoka karibu na mwalimu, alikimbia mpaka ofsini. Shughuli akaishia hapo.
 
Back
Top Bottom