Sizitaki Mbichi Hizi!!

Sizitaki Mbichi Hizi!!

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, nakutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli, iwafae maishani.

Akatamka mgonjwa, Ninaumwa kwelikweli,
Ata kama nikichinjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa, kifo kinanikabili,
Kama mnataka mali, .......................
.
.
.
.
.
Kama tunataka Mali, tutapataje Shambani?

.
.
Baba aliyekufani, akajibu lile swali,
Jambo moja lishikeni,kama mnataka Mali,
Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi Shambani, mwisho mtapata Mali.


..............,Roho ikaacha mwili,
Na Watoto kwa umoja , wakakumbuka kauli,
Kama tunataka mali, tatayapata Shambani.
 
sio mchezo kaka umetukumbusha mbali sanaaaa!!!!.... kipindi hicho kweli elimu ilikuwa elimu!!!!
 
.....Kama tunataka Mali, tutapataje Shambani?..Baba aliyekufani, akajibu lile swali,Jambo moja lishikeni,kama mnataka Mali,Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli, Fanyeni kazi Shambani, mwisho mtapata Mali...............,Roho ikaacha mwili,Na Watoto kwa umoja , wakakumbuka kauli,Kama tunataka mali, tatayapata Shambani.
Teh teh teh teh! Nimefurahisana mkuu.
 
Kuna siku moja tukiwa class Prof. Mbonile wa UDSM ( Demography) alituchekesha eti yeye enzi zake alisoma kitabu cha someni bila shida na moja ya ukurasa ulisomeka hivi:"Baba baba baba. Mama mama mama. Baba ana mche. Mama ana kinu. Baba anatwanga kwenye kunu ncha mama"Jamaa alituchekesha sana!!!
 
...ilifika mahali kila mkuu wa shule ndio ana uamuzi wa kuchagua vitabu vya wanafunzi wake!!!

Mkuu sio mwalimu mkuu peke yake. Hata serikalini nako ikawa vituko kila waziri anaekuja anaibuka na style yake ya taaluma, huyu anafuta michezo, yule ana changanya masomo kuwa moja, mwingine analeta tehama. Yani mambo ni vurughu tupu.

Cha ajabu wao hawaoni matunda ya vijana wetu kuna migomo na kiwango cha ufaulu kuzidi kushuka na hawatafuti chanzo ni nini.

Nilishangaa sana siku ya kutangaza matokeo ya form IV eti yule mama wa baraza la mitihani anasoma kitu alichoandika mwanafunzi kwa waandishi wa habari, na jamii inaungana na hao wajinga kuwalaumu wanafunzi wakati kumbe ni aibu yetu wenyewe kwa kile tunachowapa watoto ndio wanatupa matunda yake.
 
Du! Mkuu umetukumbusha mbali!! Wakati huo shuleni tunakula bulga. Daftari ikiisha mwalimu anasaini unapewa nyingine
wakati huo wazazi hamuitwi shuleni kila kukicha eti mkutano kumbe kuna kamchango kanahitajika.
 
hii picha imenikumbusha mbali! Sitaki mbichi hizi
 
Nakumbuka enzi hizo tunajifunza kiinglish. Mwalimu anafundisha opposite words:

Near===far

Nyaturu translation.

Near----kunya
far........hapa

Mwalimu kakazana, near--far...near...far....anataka watoto wafuatishe lakini hakuna mtu anaitikia!

Mara, salaaale!...akasema, nyie wanyaturu wajinga kweli...hiki ni kiingereza sio kikwenu...watu mbavu hatuna...
 
mweka nadhiri na shetani...la saba
Lindu amukoa kapilima....la tano
Kibanga ampiga mkoloni....la tatu
Mpapai na matete....la pili
Watoto wageuka mawe...la kwanza
Bila kusahau hadith za kina bulicheka....
....
....
....
Saa ya babu mzee yaenda vizuri sasa miaka tisini...............
 
karuka tena karuka mtini akarukia......
ahhh nimesahau mashairi yake, dah mkuu umenikumbusha mbali sana.
 
Back
Top Bottom