Sizitaki Mbichi Hizi!!

Sizitaki Mbichi Hizi!!

Sungura afahamika ujanja kajijazia, wenzake anawacheka sungura huwazomea.... kitambo sana aisee
 
Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia,
Hadithi uliyotaka, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
 
Hem mwaga mistari hapa kuonesha ulipitia enzi zileee


View attachment 53687




Karuka tena karuka, lakini hakufikia

..........................................

Sizitaki mbichi hizi, umenikumbasha mbaaaaaaaaaaali mno!!

Machozi yamenitoka.....nikitazama nyuma wengi siwaoni!!

Enzi za ....

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali

......
 
Mlisoma na zile Hesabu za Kikwetu halafu Highway Mathematics?
 
panzi.jpgpazi2.jpg
 
Sizitaki mbichi hizi, mambo ya hadithi za abunuwasi na alfu ulelaulela kama sikosei. Kulikuwa na zile hadithi za wagagagigikoko!
 
Sungura hafahamika,ujanja kajijazia.
wenzake anawacheka sungura uwazomea.
Ila siku ikafika ya sungura kuumia,ya sungura kuumia,sungura nakuambia.

Endelea
 
Kwanini utese wanyama nawe teseka kidogo. Kijana aliwabeba kuku vichwa chini na kuwapiga, nae sasa anaionja tamu yake.
 
Ilikuwa inaanza hivi wakuu,
Hadithi inayokuja ni sungura sikia, hadithi uliyongoja leo ninakuletea.
Alitoka siku moja njaa aliposikia, njaa aliposikia sungura nakuambia


Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.

"Sizitaki mbichi hizi" Sungura akagumia,
"Naona nafanya kazi, bila faida kujua",
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi
 
Back
Top Bottom