Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mels Dalder raia wa Uholanzi ambaye ni Chief Scout wa Simba ametangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram kujiuzulu wadhfa wake ndani ya Simba huku akiweka wazi kuwa sababu hajioni kama anapita njia moja na mwelekeo wa Klabu kwasasa, yaani yeye ana vision nyingine ila kinachofanyika ni kingine.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kuwa hata uteuzi wa Kocha Dimitr Pundev ulipingwa wazi na Skauti Mkuu maana yeye ndio alikuwa wa kwanza kugundua kuwa Kocha hana vigezo na aliwasilisha Klabuni ila tayari Klabu ilikuwa tayari imefanya maamuzi tena ya Mtu mmoja tu huku tayari wakiwa wamelipa gharama zote.
Taarifa zaidi ni kuwa cheo alichopewa Dimitr ni kuzibia BLANDA iliyofanyika na wala haukuwa mpango wa Klabu baadhi wana mpango wa kujiuzulu.
Daalder amesema kuwa ameamua kujiondoa katika nafasi hiyo kwa vile hajioni kama ana nafasi siku za usoni.
"Nimeamua kujiuzulu nafasi yangu kama Mkuu wa Skauti ndani ya Simba SC kwa vile sijitambui tena katika muelekeo wa klabu.
"Katika safari hii nzima nimekumbana na changamoto nyingi lakini nyakati hizo zote zimenijenga na kufanya mafanikio kuwa ya maana. Jambo muhimu zaidi lilikuwa kufikia Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF msimu wa 2024/2025, kumbukumbu ambayo nitatunza daima.
"Napenda kumshukuru kwa dhati Rais wa Klabu, Mohamed Dewji, Aliyekuwa Kocha Mkuu Fadlu Davids na wafanyakazi wake kwa uaminifu wao na ushirikiano mkubwa. Zaidi ya yote, shukrani zangu ziwaendee mashabiki, damu ya klabu hii kwa mapenzi yao na usaidizi usioyumbayumba.
"Ninaacha jukumu langu, lakini sio kwa upendo wangu. Nitaunganishwa na Simba kama shabiki, na ninatazamia siku zijazo katika soka," amesema Daalder.