Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MARTHA FESTO AHOJI UJENZI WA SKIMU YA MWAMAPULI HALMASHAURI YA MPIMBWE
Katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma Martha Festo alielekeza swali Wizara ya Kilimo kutaka kujua ni lini Skimu ya Umwagiliaji ya Mwamapuli itaanza kujengwa katika Halmashauri ya Mpimbwe
"Je, ni lini Mradi wa umwagiliaji wa Mwamapuli uliopo Halmashauri ya Mpimbwe utaanza kujengwa?" - Mhe. Martha Festo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi
"Kitabu cha bajeti Wizara ya Kilimo 2023-2024 kiambatisho namba sita kimeelezea Skimu ambazo tunakwenda kuzifanyia kazi mwaka 2023-2024. Skimu ya Mwamapuli yenye Hekari 12,000 Wilaya ya Mpimbwe ni sehemu ya ujenzi wa mwaka wa fedha unaokuja" - Mhe. Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo