Za leo wapendwa,
Jamani mimi napenda sana ngozi yangu iwe light na smooth, naona wanawake wengi wenzangu wanavutia sana... nimejaribu kutumia baadhi ya skin lightening cream ila naungua kwenye mashavu na uso umejaa pimples nyeusi zilizojaa uchafu ule mweupe kwa ndani. Niliamua kuacha hizo cream na nimerudia rangi yangu ya kawaida ila naona sipendezi tena. Naomba munisaidie ni nini naweza kutumia ili nin´gae na niwe smooth. Sitaki kuchubuka tena, je kuna cream zozote ambazo hazichubui? Asanteni kwa ushirikiano wenu.