JR ZAGAMBA
New Member
- Jun 24, 2023
- 1
- 2
Tunaishi kwenye Jamii ambayo Madoktari hawajali afya,Elimu ni ndoto za vigogo na sheria hupotosha haki. Viongozi wa Dini na Serikali wamejiziba Mdomo hakuna wa kutusemea, na Vyombo vya habari vimegeuzwa kuwa vyombo vya kuzika Utetezi na haki
HADITHI YA KUFIKIRIKA
SKONONDO Mtoto wa miaka (14), Anaishi kwenye mtaa uliokithiri vitendo vya kihaini na matumizi ya madawa ya kulevya ukiongozwa na SIMBA (38) Kiongozi wa Dambo Mob. Anaishi na Mama yake ambae anauza Gongo na mwili wake ili kujikimu kimaisha.
Skonondo ni mtoto mtukutu ila tofauti yake na wengine wa mitaani yeye ana ndoto ya kuwa Mpiga Picha za matukio ya habari. Hivyo hutumia muda mwingi kucheza na watoto wenzake wa Mitaani kwa camera za bandia na kuigiza kama mwanahabari. Watoto wenzake wanamkatalia kucheza nae kwani wamechoshwa kufanya maigizo wanataka wapate camera ya ukweli. Anaamua kutafuta camera ya Ukweli.
Mtaani Kuna MR MAFUKU Kiongozi mwanasiasa ambae ni shujaa kwenye jamii wanayoishi, hutoa misaada kwa watu wenyeshida mbali mbali, wanamwamini sana, na anawaahidi kufufua magodauni na kudumisha huduma za kijamii na kushughulikia kilio cha wananchi kuhusu wimbi la madawa ya kulevya
Siku moja Skonondo anakutana na Masawe ambae ni Mpiga picha wa Mr Mafuku katika moja ya mikutano yake na wananchi. Skonondo anamuomba amfundishe kupiga picha, Masawe anamfukuza. Masawe ni mwandishi anaye eneza Sifa nzuri za Viongozi akiwemo Mr Kafuku
Skonondo anakasirika anaanza kufanya kazi za kuosha magari barabarani na Kuokota makopo matupu ya maji, anauza ili kukusanya pesa na kununua camera. Ila akiwa Dampo anaokota mabaki ya mazeti yaliyotupwa yenye Picha ya style='mso-bidi-font-weight:normal'>SIMBA kiongozi wa Dambo mob chini yake Kumeandikwa kuwa Mapolisi washindwa kudhibiti Madawa ya kulevya kwa kukosa Ushahidi"
Skonondo anaenda kwa Mpemba fundi wa vifaa vya umeme, ambae hununua vifaa tofauti tofauti kama cm,redio mbovu na vifaa vya ndani kisha anavirekebisha na kuuza. Skonondo anataka kununua camera ila pesa yake imepelea kiasi kidogo sana.
Mpemba anamwambia aache pesa ili akamalizie zilizobaki, Skonondoa anakataa na kuondoka na pesa zake ili akaongezee
Skonondo akiwa anarudi nyumbani kwao mida ya Jioni anakatisha mitaa ya Dambo Mob ambapo wahuni huvuta bangi na madawa, Anapokonywa hela za Camera na kumfukuzwa eneo lile
Skonondo anarudi nyumbani akiwa na hasira anakuta Masawe yupo Kilabuni anakunywa pombe na kutoa ofa kwa walevi huku anamchezea makalio mama yake ambae anahudumia walevi wengine, Skonondo anakairika anaondoka zake
Anarudi Usiku pakiwa papo kimya anaingia ndani, pembeni kuna nguo za masawe pamoja na viatu vimelundikwa sehemu moja, Chumba ni kimoja ambacho kimetenganishwa na pazia, Skonondo anatandika mkeka ili anaanze kulala.
Anasikia Miguno ya mahaba ya watu wakifanya mapenzi iliyo ambatana sauti za mlio wa kitanda.Skonondo anaziba masikio kwa viganja vya mikono. Najua unapata taswira ya tukio jinsi inavyouma unapokuwa kwenye condition hiyo
Asubuhi skonondo anafungua masufuria hakuti kiporo, anataka kutoka anaona nguo na begi la Camera, Skonondo anafungua begi la Camera na kufikiria kwa muda anaamua kuiba Camera
Skonondo akiwa mtaani anatembea huku anajaribisha kupiga picha hadi anajua kitufe, anaenda kucheza na watoto wenzake kwa camera ya Ukweli.
Usiku unapofika anakwenda kuificha camera kwenye magodauni na kurudi nyumbani, anafika nyumbani anakuta mama yake amesimama mlangoni,Mama anamfukuza hadi arudishe kamera
Skonondo anafika Godown wakati anachukua Camera, ghafla anamwona Shujaa wake Mr Mafuku akiwa katekwa na kundi la Dambo Mob likiongozwa na Simba, wanatembea nae kuingia kenye Godown.
Skonondo anamua kufwatilia kwa makini,anafanikiwa kupenya na kuingia kwenye Godown, Mara taa inawaka, Skonondo akiwa kajibanza Sehemu, anaona Dambo Mob wamemuweka katikati Mr Mafuku.
Skonondoa anakumbuka kuwa anakamera haraka haraka anawasha camera, anajikuta amebonyeza kitufe cha kurekodi video, anagundua kuwa ameweka sehemu ya kurekodi badala ya photo.Anaanza kuangaika na kujaribu seting.
Ghafla anasikia Sauti ya Mr Mafuku anaongea, anastaajabu baada ya Kugundua kuwa Mr Kafuku ndie anaewacontrol Dambo Mob ndie Bosi wao.
Anaingiwa na simanzi na kuendelea kuseti kamera yake upande wa picha, ananza kuhangaika na kufanya setting, Akiwa anabonyeza bonyeza kwa pupa anajikuta amebonyeza kitufe na Mwanga wa Camera unatoka, Wote wanashtuka Mr Mafuku anaamrisha Wamtafute mtu aliyepiga picha
Skonondo anakimbia Kundi zima la Dambo Mob linamkimbiza Usiku,Skonodo anafanikiwa kuwatoroka na kujificha, anawasikia wahuni wakipita karibu na alipojificha wakisema akikamatwa apotezwe.
Asubuhi Skonondo anarudi nyumbani, anafika nyumbani anakuta kundi kubwa la Dambo mob lipo nyumbani kwao likifanya fujo, mama yake amepigwa na kuumizwa, Dambo mob wanamwona, Skonondo anakimbia nao wanamkimbiza.
Skonondo anapotea na Ushahidi,kwa muda wa siku kadhaa Skonondo anatafutwa Kwa kesi ya kuiba kifaa cha mheshimiwa chenye nyaraka za siri
Juhudi za kumtafuta skonondo zinazaa matunda wanafanikiwa kumwona, skonodo anawachengesha ili kuokoa uhai wake, kundi kubwa likiwa linamkimbiza kwenye vichochoro, Skonondo anakimbia hadi anatokea nje ya Kituo cha Polisi,Dambo mob wanasita, Skonondo anasimama anatabasamu na kuingia ndani kutoa ushahidi
Kundi zima La Dambo Mob linafanikiwa kukamatwa akiwemo Nguli wao Mr Mafuku ambae ni Kitovu cha tatizo. Skonondo anakuwa shujaa katika jamii

Attachments
Upvote
2