Sky Walker kwa hili la Diamond na Davido umeonyesha udhaifu

Ujinga mwingine bana eti wizkid anatafuta ushkaji na diamond. dogo unaongea utumbo wa kuku.. ngoja niende kusoma hard news huffington post.. wewe mmatumbi bado hujui kinachoendelea

Mkuu kwa vile umekuja mwenyewe humu, si vizuri kukimbia, jibu unachoulizwa. Kule siasa saivi kumedoda. Hata akina Ritz FaizaFoxy tupo nao hapa kwa id zao za 8 huko,. Usikimbie.

Hufington post ndo zipi??
 
Last edited by a moderator:
Ni mchambuzi wa ishu za burudani jina halisi Michael Bundara.....ndio mkuu wa mambo ya content bongo5.com

Eti mchambuzi.. yan kama akina adry towsand ama dr liki abdala?? Sema yeye ni kwenye mahusiano ya maceleb na maisha yao au? Basi ni pimbi.
 
Wewe comment zako zilivyo its obvious una viroba vingi kichwani,pili chuki za kike zmekujaa. Sasa km Davido ana followers wengi Kwahiyo nn sasa. Ndo iweje kwa Nasibu. Unaumwa kweli Wewe

kooooote umepatia ila sasa ulivyokuja kutaja wanawake ndo umenichafua sana sipendi dharau!!
 
Hatuwezi kupingana kimawazo bila matusi jamani?! Mleta mada una mtazamo wako sawa sawa na sky walker alivyokuwa na mtazamo wake,km huafiki jua pia kuna raia wengne hatukuafiki pia. Sasa matusi na lugha za kejeli za nin hapa?! Tujadili hoja kwa hoja na kufanya jukwaa liwe zuri jamani...
 
Diamond kwa sasa hamhitaji Davido,labda amheshimu kwa kazi waliyofanya zamani,Diamond naija tu kafanya collabo na zaidi ya wasanii wanne na wote wana majina,msanii gani mkubwa africa now anaweza kumnyima diamond collabo kwa sasa?labda p square.
tweets za davido zina utata,majibu ya diamond pia hayamfungi kwamba amemlenga davido
 
Ujue Watanzania haka ka ugomvi tukikatumia vizuri kama fulsa kataifikisha mbali sana sanaa yetu, ni muda wa wasanii wa bongo kuitumia hii fulsa jamani, yaani naiona sanaa ya Tanzania ileee inapaa juu endapo tutautumia ugomvi huu kama fulsa(usiniulize kivipi)
 

Tusikuulize wakati we ndo umesema?Haya tuambie kivipi
 
Diamond mtu wa kawaida.. wala hapaswi kulinganishwa na davido
Tunakosea

We bogus kweli, mwenzako Davido anajuta kukubali kufanya collabo nae maana nyota inavyomng'aria huyu jamaa yetu hadi Davido anaogopa
 
hapa si swala la uzungu au utaifa , just reality diamond hamfikii davido hata wimbo walioimba wote diamond kafunikwa mbaya

hila alikiba? Acha chuki....kwa taarifa yako tuzo alizochukua amepata kwa number one original
 
Mbona mimi naona wote hao ujana unawasumbua.
 
NIMESOMA ILE POST YAKE NILIMSHANGAA SANA HUYO SKY, ANALAZIMISHA DIAMOND AMNYENYEKEE DAVIDO! davido katukosea sisi kutuona ni watu ambao hatuwezi kufanikiwa kwa njia za kawaida, kwa mstaarabu nagefuta ile post yake baaada ya reaction kutoka kwa watanzania, lkn aliiacha na kuendelea kutweet vijembe!
SKY anadiriki kuandika uongo kuwa davido aliondoka hotelini uganda baada ya kupigwa wimbo wa diamond akitaka ahalalishe kile anachoona kinafaa(kumlamba miguu davido).....tupo watanzania mil45 je tukubali unyonge wa kuwa hatuwezi kushinda mpaka tufanye hila na tukubali mtu atutukane kwa sababu yeye muziki wake upo juu?nampongeza ommy dimpoz, adam juma, dj choka nk wadau wa muziki waliojitokeza na kusema no hii hapana
sasa hivi miss Tanzania kaingia 10 bora! ni juhudi zetu kama watanzania na wanaotuunga mkono kumpigia kura mpaka kafikia hapo, akipata ushindi atasema tena tumecheat na kuna wap..umbavu watamtetea kuwa hakumaanisha hivyo
WATANZANIA SASA TUMEAMKA MAKUNDI YETU NI NDANI TU LKN KIMATAIFA TUNAUNGANA KWA AJILI YA TANZANIA
 
hila alikiba? Acha chuki....kwa taarifa yako tuzo alizochukua amepata kwa number one original

Na kumbuka ile RMX ndio ilifanya Mond atusue kule Nigeria

Mnapngana na walker ? Nigeria watawazima na mziki wenu wa kiboya
 
na kumbuka ile rmx ndio ilifanya mond atusue kule nigeria

mnapngana na walker ? Nigeria watawazima na mziki wenu wa kiboya

kwa hiyo unataka watanzania tuiname atutie vi..dole vya ma..tako kisa kafanya colabo na dai?
 
kwa hiyo unataka watanzania tuiname atutie vi..dole vya ma..tako kisa kafanya colabo na dai?

Czungumzii watz nazungumzia mond na davido
Moja unajua Nigeria kimedia wametuzidi TVs station zao zinakita Africa nzima je cc zetu zinaishia wapi ?
 
Diamond asichukue ushauri huu wa kunyanyaswa kisa alisaidiwa!

Watanzania ni mabingwa wa kukuza mambo hakika wameshalichukulia hili jambo kama mtaji!
 
Kwenye hili swala naona baadhi ya watanzania wakiwemo-Bong5.com, wameamua kumfanya mkosaji kuwa ndiye-aliekosewa na aliekosewa kuwa ndiye mkosaji. Huku ni kukosa uzalendo, lakini pia ni kiwango cha hali ya juu cha kuthamini wageni mpaka tukakubali kuwa mabwege!-

Nimejiuliza tu, hivi ingekuwa kauli ile "tata" (wamedanganya tena) kaisema Diamond dhidi ya Wanigeria, jee kweli kuna mnigeria au chombo cha habari cha nigeria kingemkingia kifua Diamond? SI dhani!

Nianze na-Bongo5.com.-Nilishangazwa sana na kukurupuka kuanza kuwa wakili wa Davido. Ni kweli HEKIMA ilihitajika kutafsiri kauli yake tata, LAKINI tafsiri yoyote ambayo mtu angeitumia kutafsiri tungo ile tata bado mtu huyo angebaki kuwa sahihi, mpaka tu pale mtoa kauli ile (Davido) atakapo toa tafsiri sahihi zaidi ya kauli ile. Mathalani nikisema "Juma kapanda mchungwa" Hii ni tungo tata, tafsiri yoyote utakayokuwa nayo ni sahihi. Yaani kama utafahamu kwamba Juma ka kwea mchungwa (kupanda juu ya mchungwa) au Juma kaotesha mchungwa,tafsiri zote hizo mbili zinabaki kuwa sahihi mpaka pale mimi mtoa kauli hiyo ntakapo bainisha ipi sio sahihi.

Bongo5.com-mkaja kwa pupa ile ile waloitumia watafsiri (Watanzania) wa kauli ya Davido, na nyie mkaja na uetetezi kwa Davido, huku uetetezi wenu ukiwa umejaa kauli za "kuwezekana (Possible")" ( 0.05 > P < 1). Huwezi kumwambia mwenzako hayuko sahihi kwa utetezi wa kauli ya " inawezekana"

Bongo5.com-ningewaona mna busara na wamaana pia katika swala hili kama mmngeandika makala kumlaumu Davido kwa kutokufafanua kauli yake mpaka leo hii. Yeye Davido akiwa kama msaniii anaeheshimika na Watanzania, ambao pamoja na umaskini wetu tumechangia katika utajiri wake, kwa kodi zetu analetwa hapa nchini, analipwa ma milioni ya fedha (mara kumi zaidi ya walipwavyo wasanii wetu), kwa kwa viingilio vyetu tunahudhuria matamasha yake kwa wingi. Hilo tu lilitosha kwake yeye Davido kuona umuhimu wa kufafanua kauli yake, ili kuondoa sintofahamu kama hakuwa na nia mbaya.

Bongo5.com-kwa chuki zenu, mmelalia upande wa Davido ambae kutokana na ukimya wake, tafsiri pekee yenye nguvu kwa sasa "Probable" (0.05 < P < 1) ni hiyo iliyotafsiriwa na Watanzania walowengi mpaka sasa. Kama Davido alikuwa na maana zaidi ya hiyo, basi ukimya wake unamaanisha "he does not care" watazania watachukuliaje.-Kwa maana watanzania si lolote si chochote kwake, "They (Tanzanians) are nothing". Ama kwa lugha ya mwambao anamanisha " watanzania "hawazimi hawawashi". Wakikasirika au wakifurahi hawana athari yoyote katika maisha ya muziki wake. Hii ni dharau, ni matusi makubwa zaidi.

Bongo5.com-mlitakiwa muingalie hali hii katika usawa (mkiweka uzalendo mbele). Badala ya kuanza kumuandama Diamond ili ajione kakosea, eti amuombe samahani Davido. Duh ubegwe wa kiasi gani huo, Hivi inamaana mtu akikusaidia ndio unakuwa mtumwa kwake? Hivi mtu akikusadia ndo anapewa kibali cha kusema atakacho juu yako kisa tu alikusadia? No way! Kila mtu katika fani yoyote alisaidiwa na alisadia kwa namna moja ama nyengine, na bado unae msaidia unatakiwa umpe heshima yake, wala huna kibali cha dharau juu yake.

Davido kweli alimsidia Diamondkwa kumfanya ajulikane huko Magaharibi mwa afrika, lakini ni sahihi pia Diamond nae alifamya Davido ajulikane zadi huku mashariki mwaAFRIKA hasa Tanzania (mimi binafsi si mpenzi wa Music wa nigeria na sikuwa namjua huyu jama kabisaaa, baada ya No 1 remix ndo nikaanza kumfatilia kazi zake, I hope wapo wengi kama mimi huku east africa). Zaidi, Davido hakufanya collabo bure, alilipwa, so kuna faidia ya kifedhai pia aliipata, pia nominations zilizotakana na nyimbo hiyo, ziliendelea kumueka Davido kwenye ramani ya muziki Afrika na duniania, hivyo basi mwisho wa siku ushirikiano wao ulikuwa na "mutual benefit" or "win-win collobaration" Si sahihi hata kidogo kumsimanga na ´kumuapiza Diamond.

Na nani hasa aliesema kwamba kwa Diamond kurudia kuandika "Ahsante Allah tumedanganya tena...." alimaanisha kumjibu Davido katika hali ya kumaanisha (kwamba alikuwa serious)! Kwanini tusiamue basi kutumia busara hiyo hiyo mnayotumia kumtetea Davido kwa kauli yake, basi tumtete Diamond kwamba pengine na yeye alikuwa ana "joke" (mzaha tu). Yaani aliandika sentensi hiyo katika hali ya kuendeleza mzaha uloanzishwa na rafiki yake. Ni mara ngapi tumeona Diamond akiandika mizaha (kufuraisha mashabiki zake) kwenye akaunti yake ya instagram na facebook! Kwani si juzi tu aliaomba asemehewe gharama za picha alizopiga studio flani, jee alimaanisha? Hapana ulikuwa mzaha tu!

Tuwe wazalendo na mapenzi na wasanii wetu. Tuachekujidhalilisha na kuwa mabwege hata kwa haki iliyoyetu. Davido kama ni muungwana na mstaarabu, na kama si "egotism" inayomsumbuwa basi anapaswa awaombe radhi Watanzania. Au atoe ufafanuzi wa kauli yake (alimaanisha nini), hapo ndo kama nikuombwa msamaha ataombwa kwa kutokueleweka! Kukaa kimya na kuendelea kuandika mafumbo, nimuendelezo wa DHARAU na MATUSI kwa watanzania. Diamond does not owe Davido an apology,HOWEVER, we (Tanzanians) are owed an apology by DAVIDO, unless he (DAVIDO) clarifed his ambiguous sentence into a plain and clear message!

Diamond kama kufika mbali atafika tu, who is Davido by the way? Iliandikwa tu na Mungu kwamba kupitia yeye (Davido) Diamond ajulikane huko West, lakini angeweza kuwa WIZKID, IYANYA au yoyote yule. Diamond kwa juhudi zake na kama bado Mungu amempangia aendelee kwenda juu atakwenda tu! Diamond bado ana Connection na wasanii kibao wanijeria, na nchi nyengine. Napia naamini iko siku watayamaliza na Davido (wao wenyewe) sio kwa kuandamwa na-Bongo5.com na wengine .
 

Mkuu pamoja na urefu wote nimejitahidi kusoma na kuelewa Tanzania tungekua na watu wenye upeo kama ww hakika tungefika mbali sana.....tatizo watanzania ushamba umetuzidi kuona vya nje ni bora zaidi ndio maana anywae like la nguvu kwako
 

Diamond is Diamond and Davido mambo ya kutegemeana yanatoka wapi? Diamond katoka kivyake na kafika hapo alipo bila Davido. Tuache inferiority complex.
 
time will tell...sisi kama mashabiki tuwaombee kheri tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…